02-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Akinunua Mnyama Wa Udhwhiyah Kisha Akapata Maradhi Achinjwe
Akinunua Mnyama Wa Udhwhiyah Kisha Akapata Maradhi Achinjwe
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Atakayenunua kichinjwa na kumchunga kisha akapata maradhi au kuvunjika mguu wake je, huchinjwa?
JIBU:
Atakayeainisha kichinjwa na kusema: “Hiki ndicho kichinjwa changu huwa ndio kichinjwa.”
a-Akipatwa na maradhi au kuvunjika na ikiwa wewe ndiye uliyesababisha basi hatochinjwa na yapasa kununua mbadala wake au kilicho bora zaidi.
b-Na ikiwa wewe hukusababisha basi atafaa.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/99)]