03-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Hukumu ya Udhwhiya kwa Maiti
Hukumu ya Udhwhiya kwa Maiti
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah) amesema:
a-Udhwhiya ni kwa walio hai. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na ndugu waliokufa kabla lakini hakuwachinjia.
b-Atakapousia mtu kabla ya kufa kwake achinjiwe basi usia wake utafuatwa na atachinjiwa.
c-Achinje mtu kwa ajili yake na watu wa nyumbani kwake na anuie hilo walio hai na waliokufa.
d-Maiti kupwekeka na Udhwhiya si katika Sunnah.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/11]