34-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Mwenye Hedhi Kuweko Msikitini Kwa Ajili Ya Kusikiliza Hadiyth Na Khutbah
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
34-Mwenye Hedhi Kuweko Msikitini Kwa Ajili Ya Kusikiliza Hadiyth Na Khutbah
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Nini hukumu ya kuwepo mwanamke katika Masjid Al-Harama naye ni mwenye hedhi kwa ajili ya kusikiliza khutbah au Hadiyth?
JIBU:
Haijuzu kwa mwanamke mwenye hedhi kukaa Masjid Al-Haraam au katika Msikiti mwingine wowote, bali inapasa kupita Msikitini na kuchukua haja yake na mfano wake kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kumwambia ‘Aaishah alipomwambia alete kilemba naye ‘Aaishah akasema: “Kipo Msikitini nami ni mwenye hedhi.” Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Hedhi yako haipo mikononi mwako.”
Ikiwa mwenye hedhi atapita Msikitini na akaaminisha kutokuteremka kwa damu ya hedhi pale Msikitini sio tatizo.
Ama akitaka kuingia na kukaa, basi hii haijuzu, na dalili juu ya hilo ni kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipowaamrisha wanawake watoke kwenda kwenye Mswalla wa ‘Iyd isipokuwa wenye hedhi waliambiwa wasikae kwenye Muswalla.
Hii ni dalili kuwa mwenye hedhi hatakiwa kukaa Msikitini kwa kusikiliza khutbah au darsa au Hadiyth.