35-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Majimaji Yanayomtoka Mwanamke Mara Kwa Mara Ni Tohara Au Najisi Je Afanye Achukue Wudhuu?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
35-Majimaji Yanayomtoka Mwanamke Mara Kwa Mara Ni Tohara Au Najisi
Je Afanye Achukue Wudhuu?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Je majimaji yanayomtoka mwanamke yawe ni manjano au meupe ni tohara au yana najisi? Na je yampasa kuchukua wudhuu pamoja na kufahamu kuwa yanatoka mara kwa mara? Na ipi hukumu yake ikiwa yanakatika na haswa ya kuwa wanawake wengi zaidi wale wasomi wanaona ni majimaji ya kawaida hayahitaji wudhuu?
JIBU:
Kilichonidhihirikia mimi ni kuwa majimaji yanayotoka kwa mwanamke ikiwa hayatotoka katika kinena bali yanatoka katika fuko la uzazi basi ni tohara, lakini yanatengua wudhuu hata kama ni tohara kwa kuwa haishurutishi kwa kinachotengua wudhuu kuwa ni najisi. Kwa mfano upepo unaotoka katika duburi ambao ni lazima utoke pamoja na hayo unatengua wudhuu na kwa hiyo ikitoka kwa mwanamke mwenye wudhuu basi utatengua wudhuu wake na aufanye upya wudhuu wake.
Ikiwa yataendelea mara kwa mara basi hayatotengua wudhuu, lakini atatawadha kwa ajili ya Swalaah itakapoingia wakati wake na wakati huu ataswali Swalaah yake ya faradhi na za Sunnah na kusoma Qur-aan na yaliyoruhusiwa kama walivyosema ‘Ulamaa. Kwa mfano kama huu, kwa yule ambaye mkojo unamtoka mara kwa mara bila kuwa na uwezo wa kuuzuia. Hii ni hukmu ya muulizaji kwa njia ya utohara basi tohara. Na kwa upande wa wudhuu ni kuwa yanatengua wudhuu isipokuwa kama yataendelea. Kama yatakuwa yanaendelea basi hayatengui wudhuu wake isipokuwa kwa mwanamke atatakiwa achukue wudhuu wake pale tu inapoingia wakati wa kuswali au auhifadhi. Ama kama yatakuwa ni ya kukatika katika na ilikuwa ada yake kukatika tu wakati wa Swalaah, basi atachelewesha wakati wa Swalaah hadi katika wakati ambao yanakatika kama hatohofia kutoka kwa wakati, akihofia kutoka kwa wakati basi atatawadha na kuuhifadhi na kuswali. Wala hakuna tofauti yoyote kati ya kidogo na kingi kwa kuwa yote yanatoka katika njia (ya uchi) na yote yanatengua wudhuu yawe ni kidogo au kingi, tofauti na yanayotoka katika sehemu zingine katika kiwiliwili kama vile damu, matapishi; hizi hazitengui wudhuu wa mtu yawe mengi au kidogo.
Ama itikadi ya baadhi ya wanawake kuwa hayatengui wudhuu mimi sijui asili ya maneno haya isipokuwa kauli moja tu ya Ibn Hazm (Rahimahu-Allaah) yeye amesema, “Haya hayatengui udhu.” Lakini hakutaja dalili yake, na lau akiwa na dalili katika Kitabu na Sunnah au kauli za Maswahaba, ingekuwa ni hoja. Ni juu ya mwanamke kumcha Allaah na kujali sana tohara yake, kwa kuwa Swalaah haifai bila ya tohara na hata mtu akiswali mara mia moja, bali baadhi ya ‘Ulamaa wanasema: “Yule ambaye anaswali bila ya tohara hufanya mambo ya ukafiri.” kwani hii ni katika istihzai ya kwa Aayah za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).