36-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Mwanamke Anayetokwa Majimaji Anafaa Kusoma Qur-aan Na Kuswali Swalaah Za Sunnah?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
36-Mwanamke Anayetokwa Majimaji Anafaa Kusoma Qur-aan
Na Kuswali Swalaah Za Sunnah?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Mwanamke akitawadha ambae hutokwa na majimaji haya kwa ajili ya Swalaah ya faradhi je ni sahihi kwake aswali anachotaka kwa ajili ya Sunnah na kusoma Qur-aan kwa wudhu wa faradhi ile kwa ajili ya faradhi nyingine?
JIBU:
Akitawadha kwa ajili ya Swalaah ya faradhi kwa wakati wake wa mwanzo basi ni juu yake kuswali faradhi, Sunnah au kusoma Qur-aan hadi wakati mwingine wa Swalaah nyingine.
