37-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Mwanamke Anayetokwa Majimaji Je, Inajuzu Aswali Swalaah Ya Adhw-Dhwuhaa Kwa Wudhuu Wa Alfajiri?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
37-Mwanamke Anayetokwa Majimaji
Je, Inajuzu Aswali Swalaah Ya Adhw-Dhwuhaa Kwa Wudhuu Wa Alfajiri?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Je, ni sahihi mwanamke (anayetokwa majimaji)
kuswali Swalaah ya Adhw-Dhwuhaa kwa udhuu wa (Swalaah ya) Alfajiri?
JIBU:
Haisihi kwa kuwa Swalaah ya Adhw-Dhwuhaa imewekwa muda maalum hivyo basi hapana budi kuchukuwa wudhuu unapoingia wakati wake kwa sababu mwanamke huyu ni kama vile mustahaadhah, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamrisha Mustahadhah achukue udhu katika kila Swalaah.
Wakati wa Adhuhuri ni: Pindi jua linapokuwa katikatika hadi wakati wa Alasiri.
Wakati wa Alasiri ni: Kutoka kwa wakati wa Adhuhuri hadi jua linapokuwa la njano au mpaka linapokaribia kuzama. Katika hali yake ya dharura ni kuzama kwa jua.
Wakati wa Magharibi ni: Kuzama kwa jua hadi kuondoka wekundu wa jua.
Wakati wa ‘Ishaa ni: Kupotea wekudu wa jua hadi katikati ya usiku.