38-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Anayetokwa Majimaji Je Inasihi Aswali Qiyaamul-Layl Kwa Wudhuu Wa ‘Ishaa?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
38-Anayetokwa Majimaji Je Inasihi Aswali Qiyaamul-Layl Kwa Wudhuu Wa ‘Ishaa?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Je inasihi kwa mwanamke huyu (anayetokwa majimaji) kuswali Qiyaamul-Layl itapokatika nusu ya pili ya usiku kwa wudhu wa ‘Ishaa?
JIBU:
Hapana, itakapokatika usiku wa nusu ya pili inapasa kuchukua wudhu mwingine. Na imesemwa pia halazimiki kurejea kuchukua wudhu, na hii ndiyo rai iliyokubaliwa.