40-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Anayetokwa Majimaji Akatawadha Yakakatika Kisha Yakarudia Afanyeje?

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

40-Anayetokwa Majimaji Akatawadha Yakakatika Kisha Yakarudia Afanyeje?

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Mwenye kutoka na majimaji haya akitawadha hali ya kuwa yamekatika na baada ya kumaliza wudhu wake na kabla ya Swalaah yake ikateremka tena, je afanye nini?

 

 

 

JIBU:

 

 

Ikiwa ni yenye kukatikakatika basi na asuburi hadi yatakapokatika. Ama ikiwa hali yenyewe haipo wazi yaani muda inateremka na muda inaacha. Basi huyu anatakiwa atawadhe ule muda tu wa kuingia Swalaah.

 

Share