Imaam Ibn ‘Uthaymin: Adhabu Si Katika Mwili Mali Na Ahli Bali Ni Kuwa Na Maradhi Ya Moyo
Adhabu Si Katika Mwili Mali Na Ahli
Bali Adhabu Mbaya Kabisa Ni Kuwa Na Maradhi Ya Moyo
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah) amesema:
“Watu wengi wanadhania kwamba adhabu inahusiana katika siha ya mtu, afya, mali na watoto, bali kuwa na maradhi ya moyo na moyo uliofisidika ndio adhabi mbaya zaidi.”
[Ahkaam Min-Al-Quraan (1/87)]
Faida: Maradhi ya moyo yaliyokusudiwa ni yale yaliyotajwa katika Qur-aan kama shirki, bid’ah, unafiki, uhusuda, chuki, mafundo na vinyongo na kila aina ya maasi.