53-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Amehirimia Hajj As-Sayl Akaenda Jeddah Akatoharika Huko Akatekeleza Hajj Je Hajj Yake Sahihi?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
53-Amehirimia Hajj As-Sayl Akaenda Jeddah Akatoharika Huko
Akatekeleza Hajj Je Hajj Yake Sahihi?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Mwanamke amehirimia Hajj kutokea (Miyqaat ya) As-Sayl nae akiwa ni mwenye hedhi na pindi alipofika Makkah alikwenda Jeddah kwa kwa haja zake na akapata tohara huko Jeddah na kuoga na kuchana nywele zake kisha akatimiza Hijjah yake je, Hijjah yake ni sahihi je itamuhitajia kitu?
JIBU:
Hijjah yake ni sahihi na haihitajii lolote baada ya hapo.