54-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Alikuwa Na Hedhi Hakuhirimia Miyqaat Bali Ameharimia Makkah Je Inajuzu?

 

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

54-Alikuwa Na Hedhi Hakuhirimia Miyqaat Bali Ameharimia Makkah  Je  Inajuzu?

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Muulizaji anauliza: Mimi nakwenda ‘Umrah na nikapitia Miyiqaat nami nikiwa ni mwenye hedhi, hivyo sikuhirimia na nikabakia Makkah hadi nilipotoharika hivyo nikahirimia Makkah je hili linajuzu? Au nifanye nini au yanipasa nini?

 

 

JIBU:

 

 

Jambo hili halifai, mwanamke ambaye anataka kufanya ‘Umrah haimpasi kuwa karibu na Miyqaat isipokuwa ni baada ya kuhirimia hata kama akiwa ni mwenye hedhi. Dalili ya hilo ni kuwa Asmaa bint Khumays ambaye ni mke wa Abuu Bakr (Radhwiya-Allaahu ‘anhumaa) alizaa wakati huo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  akiwa Dhul-Hulayfa akikusudia kufanya Hajj Al-Wadaa’i hivyo Asmaa bint Khumays akatuma mjumbe kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  akiuliza afanye nini? Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:

اغتسلي واستثفري بثوب وأحرمي

“Koga (ghuslu) na jifunge kwa nguo na uhirimie.”

 

Damu ya hedhi ni kama damu ya nifaas, hivyo mwanamke mwenye hedhi atasema kuwa akipita Miyqaad akiwa anakusudia kufanya ‘Umrah au kufanya Hajj, tunamwambia, Koga (ghuslu) na jifunge kwa nguo na uhirimie. Maana yake atafunga vizuri sehemu zake za siri kwa nguo na kufunga vizuri kisha atahirimia iwe ni kwa ajili ya Hajj au kwa ajili ya ‘Umrah lakini akihirimia na akafika Makkah haendi kwenye Nyumba (Al-Ka’bah)  au kutufu hadi atoharike na kwa hilo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema alipomwambia Mama ‘Aaishah alipokuwa na hedhi wakati wa ‘Umrah:

 

 افعلي ما يفعل الحاج غير أن لا تطوفي في البيت حتى تطهري

 “Fanya yote ayafanyayo hujaji isipokuwa usitufu katika nyumba hadi utoharike.” Hii ni riwaayah ya Al-Bukhariy na Muslim.

 

Katika Swahiyh Al-Bukhariy imetajwa kuwa alipotoharika Mama ‘Aaishah alitufu nyumba na akafanya Sa’yi kati ya Swafaa na Marwah na hii ikawa ni dalili kuwa mwanamke akihirimia Hajj au ‘Umrah ilhali ana hedhi au ikamjia hedhi kabla ya kutufu basi hatoweza kutufu wala hatofanya Sa’yi hadi atoharike na akoge. Ama lau akitufu nae akiwa ni mwenye tohara na baada ya kukamilisha Twawaaf ikamjia hedhi basi ataendelea na kufanya Sa’yi na hata akiwa ni mwenye hedhi na atapunguza nywele zake na hivyo atamaliza ‘Umrah yake kwa sababu Sa’yi kati ya Swafaa na Marwah haishurutishi tohara.

 

Share