60-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Mwenye Nifaas Akitoharika Nifaas Kabla Ya Siku Arubaini Hijjah Yake Sahihi? Na Kama Hakupata Utohara?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
60-Mwenye Nifaas Akitoharika Nifaas Kabla Ya Siku Arubaini Hijjah Yake Sahihi?
Na Kama Hakupata Utohara?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Mwenye nifaas akitoharika kabla ya siku arubaini je Hijjah yake inasihi? Na kama hakuona tohara basi afanye nini pamoja na elimu kuwa amenuia Hajj?
JIBU:
Akitoharika mwenye nifaas kabla ya arubaini basi atakoga (ghuslu) na kuswali na kufanya yale ayafanyayo waliokuwa na tohara hadi Twawaaf kwani nifaas haina ukomo wa uchache wake.
Ama kama hakuona tohara basi Hijjah yake ni sahihi vile vile lakini hatotufu katika Nyumba (Al-Ka’bah) hadi apate tohara kwani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amemkataza mwenye hedhi kutufu Nyumba na nifaas ni kama vile mwenye hedhi.