59-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Akiwa Katika Hedhi Baada Ya Jamarah Kabla Ya Twawaaf Al-Ifaadhwah Na Hawezi Kurudi Baada Ya Safari
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
59-Akiwa Katika Hedhi Baada Ya Jamarah Kabla Ya
Twawaaf Al-Ifaadhwah Na Hawezi Kurudi Baada Ya Safari
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Mwanamke akiwa na hedhi baada ya Jamarah (Kurushwa vijiwe) katika Al-‘Aqabah na kabla ya Twawaaf Al-Ifaadhwah, nae akiwa katika kundi pamoja na mumewe na marafiki wake, juu yake ni nini afanye pamoja na elimu ya kuwa hawezi kurejea baada ya safari yake?
JIBU:
Kama hawezi kurudi basi atajihifadhi vizuri kisha atatufu kwa hali ya dharura wala isiwe kitu juu yake, na kukamilisha baki ya ‘ibaadah za matendo ya Hijjah.