58-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Mwenye Hedhi Siku Ya ‘Arafah Afanye Nini?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
58-Mwenye Hedhi Siku Ya ‘Arafah Afanye Nini?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Mwanamke akiwa na hedhi siku ya ‘Arafah afanye nini?
JIBU:
Mwanamke akiwa na hedhi siku ya ‘Arafah basi ataendelea na Hijjah yake na kufanya wanaofanya watu wala haruhusiwi kutufu katika Nyumba (Al-K’abah) hadi atoharike.