032-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila Za Waislamu Wanyonge, Mafakiri Wasiojulikana

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب فضل ضعفة المسلمين والفقراء والخاملين

032-Mlango Wa Fadhila Za Waislamu Wanyonge,Mafakiri Wasiojulikana

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ عَنْهُمْ تُرِيدُ زِينَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُ عَن ذِكْرِنَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ وَكَانَ أَمْرُهُ فُرُطًا ﴿٢٨﴾

Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Rabb wao asubuhi kabla jua kucha na jioni, wanataka Wajihi Wake. Na wala macho yako yasiwavuke kwa kutaka pambo la uhai wa dunia. Na wala usimtii Tuliyemghafilisha moyo wake na Ukumbusho Wetu akafuata hawaa zake, na jambo lake limekuwa la kuzidi kuvuka mipaka. [Al-Kahf: 28]

 

 

Hadiyth – 1

وعن حارثة بن وهْبٍ رضي الله عنه ، قَالَ : سمعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، يقولُ :(( ألاَ أُخْبِرُكُمْ بِأهْلِ الجَنَّةِ ؟ كُلُّ ضَعِيف مُتَضَعَّف، لَوْ أقْسَمَ عَلَى اللهِ لأَبَرَّهُ ، أَلاَ أُخْبِرُكُمْ بِأهْلِ النَّارِ ؟ كُلُّ عُتُلٍّ جَوّاظٍ مُسْتَكْبِرٍ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .  

Imepokewa kutoka kwake Haarithah bin Wahb (Radhwiya Allaahu 'anhu) aliyesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: " Je, niwajulishe nyinyi watu wa peponi? Kila mnyonge na mwenye kunyongeshwa, lau atakula yamini kwa Allaah basi atakubaliwa. Je, niwapashe habari ya watu wa motoni? Kila msusuwavu, mgumu na mwenye kiburi katika kutembea kwake." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي عباس سهل بن سعد الساعِدِيِّ رضي الله عنه، قَالَ : مَرَّ رَجُلٌ عَلَى النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ لرَجُلٍ عِنْدَهُ جَالِسٌ : (( مَا رَأيُكَ في هَذَا ؟ )) ، فَقَالَ : رَجُلٌ مِنْ أشْرَافِ النَّاسِ ، هَذَا واللهِ حَرِيٌّ إنْ خَطَبَ أنْ يُنْكَحَ ، وَإنْ شَفَعَ أنْ يُشَفَّعَ . فَسَكَتَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم، ثُمَّ مَرَّ رَجُلٌ آخَرُ ، فَقَالَ لَهُ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: (( مَا رَأيُكَ في هَذَا ؟ )) فَقَالَ : يَا رَسُولَ الله ، هَذَا رَجُلٌ مِنْ فُقَراءِ المُسْلِمِينَ ، هَذَا حَرِيٌّ إنْ خَطَبَ أنْ لا يُنْكَحَ ، وَإنْ شَفَعَ أنْ لا يُشَفَّعَ ، وَإنْ قَالَ أنْ لاَ يُسْمَعَ لِقَولِهِ . فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( هَذَا خَيْرٌ مِنْ مِلءِ الأرْضِ مِثْلَ هَذَا )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abil 'Abbaas Sahl bin Sa'ad As-Saa'idiyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa mtu mmoja alipita mbele ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) naye akamuuliza mtu aliyekuwa ameketi pamoja naye: "Ni Yepi maoni yako kuhusu mtu huyu?" Akasema: "Mtu huyu ni miongoni mwa watu watukufu. Wa-Allaahi, huyu anastahiki akienda kuposa aozeshwe na akiombea akubaliwe ombi lake. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akanyamaza, halafu akapita mtu mwingine, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza tena: "Ni Yepi maoni yako kuhusu mtu huyu?" Akasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Huyu mtu ni miongoni mwa mafakiri wa Waislamu, naye anafaa akienda kuposa asiozeshwe na akiombea asikubaliwe ombi lake na akizungumza asisikilizwe." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Huyu (fakiri) ni bora kuliko kuijaza ardhi na watu mfano wake (mtu wa kwanza). [Al-Bukhaariy na Muslim]

   

Hadiyth – 3

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( احْتَجَّتِ الجَنَّةُ والنَّارُ ، فقالتِ النَّارُ : فِيَّ الجَبَّارُونَ وَالمُتَكَبِّرُونَ . وَقَالتِ الجَنَّةُ : فِيَّ ضُعَفَاءُ النَّاسِ وَمَسَاكِينُهُمْ ، فَقَضَى اللهُ بَيْنَهُمَا : إنَّكِ الجَنَّةُ رَحْمَتِي أرْحَمُ بِكِ مَنْ أشَاءُ ، وَإنَّكِ النَّارُ عَذَابِي أُعَذِّبُ بِكِ مَنْ أشَاءُ ، وَلِكلَيْكُمَا عَلَيَّ مِلْؤُهَا )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Pepo na Moto zilizozana. Moto ukasema: 'kwangu ni majabari na wenye kiburi'. Na ikasema Pepo: 'Kwangu ni wanyonge na maskini wao'. Allaah Akahukumu baina yao: "Hakika wewe pepo ni rehma Yangu, kwako Ninamrehemu Nimtakaye. Na hakika wewe Moto ni adhabu Yangu, kwako Ninamuadhibu nimtakaye, na nyote Nitawajaza." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( إنَّهُ لَيَأتِي الرَّجُلُ السَّمِينُ العَظِيمُ يَوْمَ القِيَامَةِ لاَ يَزِنُ عِنْدَ اللهِ جَناحَ بَعُوضَةٍ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika atakuja mtu mkubwa na mnene siku ya Qiyaamah, hatakuwa na uzito mbele ya Allaah siku hiyo (japo uzito wa) ubawa wa mbu." [Al-Bukhaariy na Muslim]

   

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ امْرَأَةً سَوْدَاءَ كَانَتْ تَقُمُّ المَسْجِدَ ، أَوْ شَابّاً ، فَفَقَدَهَا ، أَوْ فَقَدَهُ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم، فَسَأَلَ عَنْهَا ، أو عنه ، فقالوا : مَاتَ . قَالَ : (( أَفَلا كُنْتُمْ آذَنْتُمُونِي )) فَكَأنَّهُمْ صَغَّرُوا أمْرَهَا ، أَوْ أمْرهُ ، فَقَالَ : (( دُلُّونِي عَلَى قَبْرِهِ )) فَدَلُّوهُ فَصَلَّى عَلَيْهَا ، ثُمَّ قَالَ : (( إنَّ هذِهِ القُبُورَ مَمْلُوءةٌ ظُلْمَةً عَلَى أهْلِهَا ، وَإنَّ اللهَ تعالى . يُنَوِّرُهَا لَهُمْ بِصَلاتِي عَلَيْهِمْ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Kutoka kwake Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa kulikuwa na mwanamke mweusi au kijana aliyekuwa akisafisha Msikiti. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamkosa, akamuulizia. Wakasema: "Amefariki." Akasema: "Kwanini hamukunieleza?" Hiyo ni kama kwamba jambo lake waliliona dogo. Akasema: "Nionyesheni kaburi yake." Wakamuonyesha, naye (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaswali hapo kaburini. Kisha akasema: "Hakika haya makaburi yamejaa kiza kwa watu wake na kuwa Allaah Aliyetukuka Anayatia mwangaza kwa mimi kuwaswalia." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 6

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( رُبَّ أشْعَثَ أغبرَ مَدْفُوعٍ بالأبْوابِ لَوْ أقْسَمَ عَلَى اللهِ لأَبَرَّهُ )) رواه مسلم .

Abuu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: "Huenda mwenye nywele timtim, aliyejaa vumbi anayefukuzwa milangoni, lau atamuapia Allaah (amfanyie jambo lolote lile) Angemfanyia." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 7

وعن أسامة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( قُمْتُ عَلَى بَابِ الجَنَّةِ ، فَإِذَا عَامَّةُ مَنْ دَخَلَهَا المَسَاكِينُ ، وَأصْحَابُ الجَدِّ مَحْبُوسُونَ ، غَيْرَ أنَّ أصْحَابَ النَّارِ قَدْ أُمِرَ بِهِمْ إِلَى النَّارِ . وَقُمْتُ عَلَى بَابِ النَّارِ فَإِذَا عَامَّةُ مَنْ دَخَلَهَا النِّسَاءُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Usaamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "NIlisimama katika mlango wa Peponi, wengi waliokuwa wakiingia ni maskini, matajiri wamefungwa, ila watu wa Motoni wameamriwa motoni. Na nikasimama kwenye mlango wa Motoni; wengi waliokuwa wakiingia humo ni wanawake." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 8

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لَمْ يَتَكَلَّمْ في المَهْدِ إلاَّ ثَلاثَةٌ : عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ ، وَصَاحِبُ جُرَيْجٍ ، وَكَانَ جُرَيْجٌ رَجُلاً عَابِداً ، فَاتَّخَذَ صَوْمَعَةً فَكَانَ فِيهَا ، فَأَتَتْهُ أُمُّهُ وَهُوَ يُصَلِّي ، فَقَالَتْ : يَا جُرَيْجُ ، فَقَالَ : يَا رَبِّ أُمِّي وَصَلاتِي فَأَقْبَلَ عَلَى صَلاتِهِ فَانْصَرَفَتْ . فَلَمَّا كَانَ مِنَ الغَدِ أتَتْهُ وَهُوَ يُصَلِّي ، فَقَالَتْ : يَا جُرَيْجُ ، فَقَالَ : أيْ رَبِّ أمِّي وَصَلاتِي ، فَأقْبَلَ عَلَى صَلاتِهِ ، فَلَمَّا كَانَ مِنْ الغَدِ أتَتْهُ وَهُوَ يُصَلِّي ، فَقَالَتْ : يَا جُرَيْجُ ، فَقَالَ : أيْ رَبِّ أمِّي وَصَلاتِي ، فَأقْبَلَ عَلَى صَلاَتِهِ ، فَقَالَتْ : اللَّهُمَّ لاَ تُمِتْهُ حَتَّى يَنْظُرَ إِلَى وُجُوهِ المُومِسَاتِ . فَتَذَاكَرَ بَنُو إسْرائِيل جُرَيْجاً وَعِبَادَتَهُ ، وَكَانَتِ امْرَأةٌ بَغِيٌّ يُتَمَثَّلُ بحُسْنِهَا ، فَقَالَتْ : إنْ شِئْتُمْ لأَفْتِنَنَّهُ ، فَتَعَرَّضَتْ لَهُ ، فَلَمْ يَلْتَفِتْ إِلَيْهَا ، فَأتَتْ رَاعِياً كَانَ يَأوِي إِلَى صَوْمَعَتِهِ ، فَأَمْكَنَتْهُ مِنْ نَفْسِهَا فَوقَعَ عَلَيْهَا ، فَحَمَلَتْ ، فَلَمَّا وَلَدَتْ ، قَالَتْ : هُوَ مِنْ جُريج ، فَأتَوْهُ فَاسْتَنْزَلُوهُ وَهَدَمُوا صَوْمَعَتَهُ ، وَجَعَلُوا يَضْرِبُونَهُ ، فَقَالَ : مَا    شَأنُكُمْ ؟ قَالُوا : زَنَيْتَ بهذِهِ البَغِيِّ فَوَلَدَتْ مِنْكَ . قَالَ : أيْنَ الصَّبيُّ ؟ فَجَاؤُوا بِهِ فَقَالَ : دَعُوني حَتَّى أصَلِّي ، فَصَلَّى فَلَمَّا انْصَرفَ أتَى الصَّبيَّ فَطَعنَ في بَطْنِهِ ،  وَقالَ : يَا غُلامُ مَنْ أبُوكَ ؟ قَالَ : فُلانٌ الرَّاعِي ، فَأَقْبَلُوا عَلَى جُرَيْجٍ يُقَبِّلُونَهُ وَيَتَمَسَّحُونَ بِهِ ، وَقَالُوا : نَبْنِي لَكَ صَوْمَعَتَكَ مِنْ ذَهَب . قَالَ : لاَ ، أعِيدُوهَا مِنْ طِينٍ كَمَا كَانَتْ ، فَفَعلُوا . وبَينَا صَبِيٌّ يَرْضَعُ منْ أُمِّهِ فَمَرَّ رَجُلٌ رَاكِبٌ عَلَى دَابَّةٍ فَارِهَةٍ وَشَارَةٍ حَسَنَةٍ ، فَقَالَتْ أُمُّهُ : اللَّهُمَّ اجْعَل ابْنِي مِثْلَ هَذَا ، فَتَرَكَ الثَّدْيَ وَأقْبَلَ إِلَيْهِ فَنَظَرَ إِلَيْهِ ، فَقَالَ : اللَّهُمَّ لاَ تَجْعَلْنِي مِثْلَهُ ، ثُمَّ أقْبَلَ عَلَى ثَدْيه فَجَعَلَ يَرتَضِعُ )) ، فَكَأنِّي أنْظُرُ إِلَى رَسُول الله r وَهُوَ يَحْكِي ارْتضَاعَهُ بِأصْبَعِهِ السَّبَّابَةِ في فِيه ، فَجَعَلَ يَمُصُّهَا ، قَالَ : (( وَمَرُّوا بِجَارِيَةٍ وَهُم يَضْرِبُونَهَا ، ويَقُولُونَ : زَنَيْتِ سَرَقْتِ ، وَهِيَ تَقُولُ : حَسْبِيَ اللهُ ونِعْمَ الوَكِيلُ . فَقَالَتْ أمُّهُ : اللَّهُمَّ لاَ تَجْعَل ابْنِي مِثْلَهَا ، فَتَركَ الرَّضَاعَ ونَظَرَ إِلَيْهَا ، فَقَالَ : اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي مثْلَهَا ، فَهُنَالِكَ تَرَاجَعَا الحَديثَ، فَقَالَتْ : مَرَّ رَجُلٌ حَسَنُ الهَيْئَةِ ، فَقُلْتُ : اللَّهُمَّ اجْعَلْ ابْنِي مِثْلَهُ ، فَقُلْتَ : اللَّهُمَّ لاَ تَجْعَلْنِي مِثْلَهُ ، وَمَرُّوا بهذِهِ الأمَةِ وَهُمْ يَضْرِبُونَهَا وَيَقُولُونَ : زَنَيْتِ سَرَقْتِ ، فقلتُ : اللَّهُمَّ لاَ تَجْعَلِ ابْنِي مِثْلَهَا ، فَقُلْتَ : اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي    مِثْلَهَا ؟! قَالَ : إنَّ ذلك الرَّجُل كَانَ جَبَّاراً ، فَقُلْتُ : اللَّهُمَّ لا تَجْعَلْنِي مِثْلَهُ ، وَإنَّ هذِهِ يَقُولُونَ : زَنَيْتِ ، وَلَمْ تَزْنِ وَسَرقْتِ ، وَلَمْ تَسْرِقْ ، فَقُلْتُ : اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي مِثْلَهَا )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hawakuzungumza ulezini (uchangani) ila watatu: 'Iysa bin Maryam, Saahibu wa Jurayj. Jurayj alikuwa mtu mwenye kuabudu, naye akajenga kihekalumchake, akakaa humo, Alipokuja mamake akiwa anaswali Akamwuita: "Ee Jurayj." Akasema: "Ee Mola wangu! Mamangu na Swalaah yangu." Hivyo, akaendelea kuswali, basi akaondoka. Kesho yake alikuja akiwa anaswali. Akamuita: "Ee Jurayj." Akasema: "Ee Mola wangu! Mamangu na Swalaah yangu." Akaendelea kuswali, Akaondoka. Kesho yake akaja akiwa anaswali. Akamuita: "Ee Jurayj." Akasema: "Ee Mola wangu! Mamangu na Swalaah yangu." Akasema (mama): Ee Allaah, usimfishe mpaka aone nyuso za kahaba." Banu Israaiyli wakazungumza habari ya Jurayj na Ibada zake, Kulikuwa na mwanamke kahaba aliyepigiwa mfano kwa uzuri wake, akasema: "Mkitaka nitamfitini. Akamjia, hakumtazama. Akaja kwa mchungaji aliyekuwa akilala kwenye kihekalu chake, akammakinisha katika nafsi yake, akajamiiana naye. Akabeba mimba, Alipozaa, alisema: "Huyu ni mtoto wa Jurayj." Watu wakaja kwake, wakamteremsha na kuvunja kihekalu chake huku wanampiga. Akawauliza: "Mna nini nyinyi?" Wakasema: "Umezini na huyu malaya, naye kakuzalia mtoto." Akasema: "Mtoto yuko wapi?" Wakamleta akawaambia:"Niacheni ni swali." Akaswali,alipomaliza Swalaah yake akaja kwa mtoto na kumchua kwenye tumbo lake, akamuuliza:"Ee kijana! Nani baba yako?" Akasema: "Fulani mchungaji." Watu wakamkabili Jurayj kumbusu na kumwuomba msamaha. Wakasema: "Tunakujengea kihekalu chako kwa dhahabu." Akasema: "Hapana, irudisheni kama ilivyokuwa ya udongo." (Wa tatu); Mtoto akiwa ananyonya kwa mamake, akapita mtu mwenye kupanda mnyama, umbile na hali yake nzuri, na vazi lake zuri. Mamake akasema: "Ee Allaah , mjaalie mwnangu mfano wa huyu.: Mtoto akaacha kunyonya, akamtazama yule mtu, akasema: "Ee Allaah, usinijaalie kama huyu." Kisha akaelekea kwenye nyonyo na akaendelea kunyonya. Ni kana kwamba mimi namtazama Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiingiza kunyonya kwake (mtoto huyo) kwa kidole chake cha shahada mdomoni mwake. Akasema mara wakapita kwa kijakazi huku wanampiga,
wakisema: "Umezini, umeiba," naye anasema: "Allaah Ananitosha Naye ni Mbora wa kutegemewa." Mamake akasema: "Ee Allaah, usimjaalie mwanangu mfano wake." Akaacha kunyonya, akatazama, kisha akasema: "Ee Allaah , nijaalie mfano wake." Hapo mazungumzo yakajiri; Mama akasema: "Alipita mtu mwenye umbo zuri, nikasema: Ee Allaah, mjaalie mwanangu kama huyu, ukasema: 'Allaah usinifanye hivyo.' Akapita huyu kijakazi, nao wanampiga huku wakisema: Umezini, umeiba. Nikasema: 'Ee Allaah, usimjaalie mwanangu kama huyu.' Ukasema: 'Ee Allaah, nijaalie kama yeye.' Akasema mtoto: "Hakika yule mtu alikuwa jabari, hivyo nikasema: 'Ee Allaah usinijaalie kama yeye.' Na hakika huyu (kijakazi), wanamwambia: Umezidi, hajazini, Umeiba, hajaiba Nikasema: 'Ee Allaah, nijaalie kama yeye." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]
 
 
 
 

 

Share