00-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Kuhukmu
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَاب اَلْقَضَاءِ
00-Kitabu Cha Kuhukumu
1188.
عَنْ بُرَيْدَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {"اَلْقُضَاةُ ثَلَاثَةٌ: اِثْنَانِ فِي اَلنَّارِ، وَوَاحِدٌ فِي اَلْجَنَّةِ. رَجُلٌ عَرَفَ اَلْحَقَّ، فَقَضَى بِهِ، فَهُوَ فِي اَلْجَنَّةِ. وَرَجُلٌ عَرَفَ اَلْحَقَّ، فَلَمْ يَقْضِ بِهِ، وَجَارَ فِي اَلْحُكْمِ، فَهُوَ فِي اَلنَّارِ. وَرَجُلٌ لَمْ يَعْرِفِ اَلْحَقَّ، فَقَضَى لِلنَّاسِ عَلَى جَهْلٍ، فَهُوَ فِي اَلنَّارِ"} رَوَاهُ اَلْأَرْبَعَةُ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
Kutoka kwa Buraydah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Maqaadhwi ni watatu, wawili[1] ni wa motoni na mmoja ni wa katika Jannah. (Wa kwanza) Ni mtu amejua haki akahukumu kwayo; huyo ni wa katika Jannah. (Wa pili) ni mtu amejua haki wala hakuhukumu kwayo, na akafanya jeuri katika hukumu, huyo ni wa motoni. (Wa tatu) ni mtu ambaye hakujuwa haki, akahukumu watu kwa ujinga, huyo ni wa motoni.” [Imetolewa na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) na akaisahihisha Al-Haakim]
1189.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم : {"مَنْ وَلِيَ اَلْقَضَاءَ فَقَدْ ذُبِحَ بِغَيْرِ سِكِّينٍ"} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ، وَابْنُ حِبَّانَ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kutawalia ukadhi, kwa hakika amechinjwa bila ya kisu.”[2] [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na akaisahihisha Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan]
1190.
وَعَنْهُ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {"إِنَّكُمْ سَتَحْرِصُونَ عَلَى اَلْإِمَارَةِ، وَسَتَكُونُ نَدَامَةً يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ، فَنِعْمَ اَلْمُرْضِعَةُ، وَبِئْسَتِ اَلْفَاطِمَةُ"} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika nyinyi mtapupia uongozi, na utakuwa majuto siku ya Qiyaamah. Ni neema iliyoje (kwa mnyonyeshaji (duniani)! Na ubaya ulioje wa muachishaji (kunyonya).”[3] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
1191.
وَعَنْ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ رضى الله عنه أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: {"إِذَا حَكَمَ اَلْحَاكِمُ، فَاجْتَهَدَ، ثُمَّ أَصَابَ، فَلَهُ أَجْرَانِ. وَإِذَا حَكَمَ، فَاجْتَهَدَ، ثُمَّ أَخْطَأَ، فَلَهُ أَجْرٌ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa ‘Amr bin Al-‘Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa amemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Hakimu akihukumu akajitahidi akapatia, ana (malipo mawili), na akihukumu akajitahidi akakosea, ana ujira mmoja.” [Bukhaariy, Muslim]
1192.
وَعَنْ أَبِي بَكْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: {" لَا يَحْكُمُ أَحَدٌ بَيْنَ اِثْنَيْنِ، وَهُوَ غَضْبَانُ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa amemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Asihukumu yoyote baina ya wawili huku ameghadhibika.”[4] [Bukhaariy, Muslim]
1193.
وَعَنْ عَلِيٍّ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {" إِذَا تَقَاضَى إِلَيْكَ رَجُلَانِ، فَلَا تَقْضِ لِلْأَوَّلِ، حَتَّى تَسْمَعَ كَلَامَ اَلْآخَرِ، فَسَوْفَ تَدْرِي كَيْفَ تَقْضِي" . قَالَ عَلِيٌّ: فَمَا زِلْتُ قَاضِيًا بَعْدُ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ، وَقَوَّاهُ اِبْنُ اَلْمَدِينِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ
وَلَهُ شَاهِدٌ عِنْدَ اَلْحَاكِمِ: مِنْ حَدِيثِ اِبْنِ عَبَّاسٍ
Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Watu wawili wakishtakiana kwako, usimhukumu wa kwanza mpaka usikie maneno ya mwingine[5] pengine ndio utajua utakavyo hukumu. ‘Aliy akasema ‘baada ya mafundisho haya nikawa nahukumu hivyo.” [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy ameifanya ni Hasan na akaipa nguvu Ibn Al-Madaniyy. Na akaisahihisha Ibn Hibbaan]
Na ina ushahidi kwa Al-Haakim kutoka katika Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas
1194.
وَعَنْ أُمِّ سَلَمَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم: {" إِنَّكُمْ تَخْتَصِمُونَ إِلَيَّ، وَلَعَلَّ بَعْضَكُمْ أَنْ يَكُونَ أَلْحَنَ بِحُجَّتِهِ مِنْ بَعْضٍ، فَأَقْضِيَ لَهُ عَلَى نَحْوٍ مِمَّا أَسْمَعُ، مِنْهُ فَمَنْ قَطَعْتُ لَهُ مِنْ حَقِّ أَخِيهِ شَيْئًا، فَإِنَّمَا أَقْطَعُ لَهُ قِطْعَةً مِنَ اَلنَّارِ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ummu Salamah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika nyinyi mnakuja kwangu kushtakiana na huenda mmoja wenu akawa fasaha zaidi katika hoja yake kuliko mwingine, hivyo nikamhukumu yeye kulingana na nilivyosikia. Basi nitakayemkatia chochote katika haki ya nduguye hakika ninamkatia kipande cha moto.”[6] [Bukhaariy, Muslim]
1195.
وَعَنْ جَابِرٍ رضى الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: {" كَيْفَ تُقَدَّسُ أُمَّةٌ، لَا يُؤْخَذُ مِنْ شَدِيدِهِمْ لِضَعِيفِهِمْ ؟"} رَوَاهُ اِبْنُ حِبَّانَ
وَلَهُ شَاهِدٌ: مِنْ حَدِيثِ بُرَيْدَةَ، عِنْدَ اَلْبَزَّارِ
وَآخَرُ: مِنْ حَدِيثِ أَبِي سَعِيدٍ عِنْدَ اِبْنِ مَاجَه
Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema nimemsikia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Vipi ummah utasafishwa ilhali haki ya mnyonge haichukuliwi kutoka kwa mwenye nguvu?”[7] [Imetolewa na Ibn Hibbaan]
Na ina ushahidi kutoka katika Hadiyth ya Buraydah kwa Al-Bazzaar.
Na ina ushahidi mwingine kutoka katika Hadiyth ya Abuu Sa’iyd kwa Ibn Maajah.
1196.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: {" يُدْعَى بِالْقَاضِي اَلْعَادِلِ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ، فَيَلْقَى مِنْ شِدَّةِ اَلْحِسَابِ مَا يَتَمَنَّى أَنَّهُ لَمْ يَقْضِ بَيْنَ اِثْنَيْنِ فِي عُمْرِهِ"} رَوَاهُ اِبْنُ حِبَّانَ وَأَخْرَجَهُ اَلْبَيْهَقِيُّ، وَلَفْظُهُ: { فِي تَمْرَةٍ }
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema amemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Siku ya Qiyaamah ataitwa Qadhwi muadilifu, kutokana na ugumu wa hesabu atatamani kuwa asingehukumu baina ya watu wawili katika umri wake.” [Imetolewa na Ibn Hibbaan,na Al-Bayhaqiyy ameitaja kwa tamko: ‘hata kama ni tende’]
1197.
وَعَنْ أَبِي بَكْرَةَ رضى الله عنه عَنِ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {"لَنْ يُفْلِحَ قَوْمٌ وَلَّوْا أَمْرَهُمْ اِمْرَأَةً"} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Watu hawatafaulu watakapomtawalisha mwanamke jambo lao.”[8] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
1198.
وَعَنْ أَبِي مَرْيَمَ اَلْأَزْدِيِّ رضى الله عنه عَنِ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم أَنَّهُ {قَالَ: "مَنْ وَلَّاهُ اَللَّهُ شَيْئًا مِنْ أَمْرِ اَلْمُسْلِمِينَ، فَاحْتَجَبَ عَنْ حَاجَتِهِمْ وَفَقِيرِهِم، اِحْتَجَبَ اَللَّهُ دُونَ حَاجَتِهِ"} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ
Kutoka kwa Abuu Maryam Al-Azdiyy[9] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema kuwa: “Ambaye Allaah Atamtawalisha katika chochote cha Waislaam, akajificha dhidi ya haja zao na mafukara wao, Allaah Atajitenga naye katika haja zake.”[10] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
1199.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: {لَعَنَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم اَلرَّاشِيَ وَالْمُرْتَشِيَ فِي اَلْحُكْمِ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَحَسَّنَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ
وَلَهُ شَاهِدٌ: مِنْ حَدِيثِ عَبْدِ اَللَّهِ بنِ عَمْرٍو. عِنْدَ اَلْأَرْبَعَةِ إِلَّا النَّسَائِيَّ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amemlaani[11] mtoa rushwa na mchukua rushwa katika hukumu.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na At-Tirmidhiy amesema ni Hasan. Na akaisahihisha Ibn Hibbaan]
Na ina ushahidi wa Hadiyth ya Abdullaah bin ‘Amr kwa Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) isipokuwa An-Nasaaiy.
1200.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بنِ اَلزُّبَيْرِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {قَضَى رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنَّ اَلْخَصْمَيْنِ يَقْعُدَانِ بَيْنَ يَدَيِ اَلْحَاكِمِ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Az-Zubayr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amehukumu kuwa watesi wawili wanakaa[12] mbele ya hakimu.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na akaisahihisha Al-Haakim]
[1] Hadiyth hii inaelezea nukta mbili: Nukta ya kwanza, mtu ambaye hajui ukweli. Na mtu mwingine, ambaye hatekelezi ukweli ule pamoja na kuujua, mtu huyu ataadhibiwa. Hii ina maana kuwa elimu isiyokuwa na utekelezaji haina maana. Pili, kuna uwezekano wa kukosea katika kutoa hukumu. Kama isingekuwa hivyo basi watu wasingegawanyika katika hali ile na kila mmoja kujiona yuko sawa.
[2] Kwa kusoma Hadiyth hii adhabu na ukali ulio dhidi ya Qadhwi anayekwenda kinyume na maamrisho. Kila anayepewa nafasi ya Qadhwi ameiweka nafsi yake katika kichinjo. Ikiwa Qadhwi ni mwenye taqwa ni juu yake kutafuta hukumu yenye uadilifu zaidi. Vinginevyo anatarajiwa kupata hukumu kali mbele ya Allaah huko Aakhirah. Hadiyth nyingine inaelezea kuwa Qadhwi mwenye taqwa ataitwa na kuulizwa maswali katika Siku ya Hukmu, kiasi cha yule Qadhwi kusema: ‘Wa-Allaahi ni bora ningehukumu walau kati ya watu wawili’. Ikiwa Qadhwi huyo atakuwa ni dhalimu, mla rushwa, mara noja atatupwa motoni.
[3] Hii ina maana kuwa utawala huo unawaridhia watawala wengi hapa duniani. Hata hivyo, anapokufa anaachishwa, anakosa raha zile na anasubiri hukumu yake. Ubaya ndio mwisho wake kwa aliyeshindwa kutekeleza majukumu yake.
[4] Qadhwi au jaji asitoe hukumu yake akiwa ameghadhibika, au mfano wa hali kama hizo; kusikia kiu, njaa, ugonjwa, wasiwasi, kusikia usingizi na mfano wa hayo. Akifanya hivyo huenda akatoa hukumu isiyo adilifu. Jambo hili ni katazo la uharaam katika istwilahi ya kishariy’ah. Ikiwa Qadhwi ametoa hukumu katika hali ya ghadhabu hukumu hiyo itakuwa na utata wa kuzingatiwa uhalaal wake.
[5] Hadiyth hii inatahadharisha kutoa hukumu kwa kumsikiliza mlalamikaji pekee kuwa si sahihi, ila atakapopewa anayelalamikiwa nafasi ya kujitetea. Katika kesi ambayo mlalamikiwa amekaa kimya, anakataa kujibu maswali au hajibu, kujieleza na hajali chochote na haji kusikiliza kesi yake hapo ni ruhusa kwa Qadhwi, hakimu au jaji kutoa hukumu ya kesi ile.
[6] Hadiyth hii inabainishia nukta muhimu zifuatazo: ikiwa Qadhwi atatoa hukumu kinyume na hukumu yenyewe basi Allaah Ataiandika kuwa ni hukumu batili na hukumu sahihi Allaah Ataitoa siku ya Hukmu (Aakhirah). Pili, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakuwa na elimu ya ghaibu. Vinginevyo, asingetoa maneno kama hayo.
[7] Hadiyth hii inasisitiza haki za wanyonge kutoka kwa watu wenye nguvu na mamlaka kuwa haki zao ni wajibu kupewa. Ikiwa kuna dhuluma inayofanyika katika nchi, basi watu wote watawajibika na dhulma ile.
[8] Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema maneno hayo pindi watu wa Iran walipomtawalisha Khosru (binti wa Kisrah) akiwa kama mtawala wao. Suala la mwanamke kutawazwa kuwa ni jaji katika mahakama ni suala lenye utata miongoni mwa Wanazuoni. Hata hivyo, Wanazuoni wengi wana rai kuwa mwanamke hawezi kuwa jaji katika mahakama ya jinai.
[9] Swahaba anaitwa Al-Asadi, alikuwa Mhadhramiy. Alimtembelea Mu’aawiyah Shaam na akamsomea Hadiyth hii.
[10] Hadiyth hii inatupa fundisho kuwa ni haraam kwa mtawala kuwazuia watu wake na haja zao. Vivyo hivyo, hatakiwi kufunga milango ya hukumu kwao, badili yake watu wote, maskini kwa tajiri waweze kuingia kwake katika mashauri yao bila kuzuiwa.
[11] Wote kwa pamoja mtoa rushwa na mpokea rushwa wamelaaniwa. Hali hii inajumuisha hali zote. Hali ya kwanza kwa anayetoa rushwa ili apate haki zake zinazomuhusu. Katika hali hii uharaam ni kwa anayechukuwa si kwa anayetoa. Hali ya pili ni ya yule mtu anyetoa rushwa ili apate zaidi ya kile anachostahiki kupata na kwa hiyo anatwaa haki ya mwingine. Rushwa katika hali hii inakuwa ni haraam kwa anayetoa na anayepokea.
[12] Tunapata mafundisho yafuatayo: (a) Kuwa mlalamikaji na mlalamikiwa wafanyiwe usawa, yeyote asipendelewe. (b) Kila mmoja kati ya mlalamikaji na mlalamikiwa watoe maelezo yao kwa hakimu hali wakiwa wamekaa.