01-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Kuhukumu: Mlango Wa Ushahidi

 

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَاب اَلْقَضَاءِ

Kitabu Cha Kuhukumu

 

بَابُ اَلشَّهَادَاتِ

01-Mlango Wa Ushahidi

 

 

 

 

 

 

1201.

عَنْ زَيْدِ بْنِ خَالِدٍ اَلْجُهَنِيِّ رضى الله عنه‏ أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {"أَلَا أُخْبِرُكُمْ بِخَيْرِ اَلشُّهَدَاءِ ؟ اَلَّذِي يَأْتِي بِشَهَادَتِهِ قَبْلَ أَنْ يُسْأَلَهَا"} رَوَاهُ مُسْلِم ٌ

Kutoka kwa Zayd bi Khaalid Al-Juhaniyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Je nikuambieni shahidi bora? Ni yule anayetoa ushahidi kabla hajaulizwa.”[1] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

1202.

وَعَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ  رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{"إِنَّ خَيْرَكُمْ قَرْنِي، ثُمَّ اَلَّذِينَ يَلُونَهُمْ، ثُمَّ اَلَّذِينَ يَلُونَهُمْ، ثُمَّ يَكُونُ قَوْمٌ يَشْهَدُونَ وَلَا يُسْتَشْهَدُونَ، وَيَخُونُونَ وَلَا يُؤْتَمَنُونَ، وَيَنْذُرُونَ وَلَا يُوفُونَ، وَيَظْهَرُ فِيهِمْ اَلسِّمَنُ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa ‘Imraan bin Huswayn (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika wabora wenu ni karne yangu, kisha wanaowafuatia, kisha wanaowafuatia. Kisha kutakuwa na watu wanaotoa ushahidi (wa uongo) wala hawakutakiwa kutoa ushahidi,[2] wanakhini wala hawaaminiwi, wanaweka nadhiri wala hawatekelezi, unene utadhihiri ndani yao.” [Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

1203.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{"لَا تَجُوزُ شَهَادَةُ خَائِنٍ، وَلَا خَائِنَةٍ، وَلَا ذِي غِمْرٍ عَلَى أَخِيهِ، وَلَا تَجُوزُ شَهَادَةُ اَلْقَانِعِ لِأَهْلِ اَلْبَيْتِ"} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Haufai ushahidi wa mfanya khiyana mwanamme wala mwanamke, wala mwenye chuki dhidi ya nduguye, wala haufai ushahidi wa mtumishi wa nyumbani.”[3] [Imetolewa na Ahmad na Abuu Daawuwd]

 

 

 

1204.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {"لَا تَجُوزُ شَهَادَةُ بَدَوِيٍّ عَلَى صَاحِبِ قَرْيَةٍ"} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَابْنُ مَاجَهْ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa amemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Ushahidi wa bedui dhidi ya mtu wa kijijini (au mjini) haufai.”[4] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na Ibn Maajah]

 

 

 

1205.

وَعَنْ عُمَرَ بْنِ اَلْخَطَّابِ رضى الله عنه ‏ {أَنَّهُ خَطَبَ فَقَالَ: إِنَّ أُنَاسًا ‏ كَانُوا يُؤْخَذُونَ بِالْوَحْيِ فِي عَهْدِ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏وَإِنَّ اَلْوَحْيَ قَدْ اِنْقَطَعَ، وَإِنَّمَا نَأْخُذُكُمْ ‏ اَلْآنَ بِمَا ظَهَرَ لَنَا مِنْ أَعْمَالِكُمْ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa ‘Umar bin Al-Khatwaab (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alikhutubia akasema: “Hakika baadhi ya watu katika zama za Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) walipatilizwa kutokana na Wahyi. Na Wahyi umekatika si vinginevyo. Sasa tutawapatiliza kutokana na matendo yenu yanayotudhihirikia.”[5] [Imetolewa na Al-Bukaariy]

 

 

 

1206.

وَعَنْ أَبِي بَكْرَةَ  رضى الله عنه ‏ {عَنِ النَّبِيِّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏أَنَّهُ عَدَّ شَهَادَةَ اَلزُّورِ فِي أَكْبَرِ اَلْكَبَائِرِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ فِي حَدِيثٍ

Kutoka kwa Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Aliuhesabu ushahidi wa uzushi katika dhambi kubwa.” [Bukhaariy, Muslim katika Hadiyth]

 

 

 

1207.

وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، {أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ لِرَجُلٍ: "تَرَى اَلشَّمْسَ  ؟" قَالَ: نَعَمْ.‏ قَالَ: "عَلَى مِثْلِهَا فَاشْهَدْ، أَوْ دَعْ"} أَخْرَجَهُ اِبْنُ عَدِيٍّ بِإِسْنَادٍ ضَعِيفٍ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ فَأَخْطَأ َ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Alimuambia mtu mmoja: Unaona jua? Akasema: ‘Ndiyo’ akamuambia: kwa mfano wake toa ushahidi au wacha.”[6] [Imetolewa na Ibn ‘Adiyy kwa isnaad dhaifu. Akaisahihisha Al-Haakim lakini alikosea]

 

 

 

1208.

وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَضَى بِيَمِينٍ وَشَاهِدٍ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ.‏ وَأَبُو دَاوُدَ.‏ وَالنَّسَائِيُّ وَقَالَ: إِسْنَادُهُ جَيِّد ٌ

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ‏ رضى الله عنه ‏ مِثْلَهُ.‏ أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّان َ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Alihukumu kwa yamini na wa shahidi mmoja.”[7] [Imetolewa na Muslim na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy na amesema: ‘Isnaad yake ni nzuri’

Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amepokea Hadiyth kama hii. Imepokewa na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan

 

 

 

1209.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه مِثْلَهُ. أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّان َ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) Hadiyth mfano wake imepokewa na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan

 

[1] Hawa ni wale wanaotoa ushahidi kwa ajili ya Allaah na kwa lengo la kupatikana kwa haki. Hawasubiri hadi dhalimu awakabili na kutoa ushahidi.

[2] Hawa ni wale wenye kutoa ushahidi tu kwa njia yoyote iwe ni haki au batili. Haya yanatoka katika undani wao ili kuupoteza ukweli. Hawa ni mashahidi wa aina mbaya sana.

 

[3] Ushahidi unaotolewa na mtu asiyekuwa mwaminifu haukubaliki, adui au mtu atakayetoa ushahidi kwa kumpendelea jamaa yake haukubaliki, kwani ushahidi kama huo mara nyingi unaelemea upande mmoja. Vivyo hivyo, hairuhusiwi kwa mtu kutoa ushahidi kwa mtu anayemkirimu kwa uwezekano mkubwa wa kumpendelea katika ushahidi wake. Ushahidi unatakiwa utolewe na mtu mwaminifu ambaye hatompendelea mmoja dhidi ya mwengine.

[4] Hii ni kwa sababu bedui hajui hali na mazingira ya watu wa mjini au kijijini na ndiyo maana wamekatazwa kutoa ushahidi kwao (kwa ajili au dhidi yao). Kwa mtu wa mjini kutoa kwa watu wa mjini mfano wao inaruhusiwa kwa kufahamu kwao mazingira ya wenzao wanaokaa mjini. Ikiwa bedui anafahamu vizuri mazingira ya watu wa mjini basi anaruhusiwa kutoa ushahidi.

[5] Hadiyth hii inaelezea kuwa hukumu itatolewa kwa lililodhaniwa kuwa ni sawa. Ikiwa katika mashahidi kuna aliyesema uongo (pamoja na kuwa aliapa kuwa atasema kweli) dhambi itakuwa ni kwa yule aliyesema uongo. Kadhi au jaji hatohusika na makosa yale.

[6] Mtu anatakiwa atoe ushahidi kwa kile alichokuwa na hakika nacho au vinginevyo aache kutoa ushahidi wake. Kwa hali hiyo hatakiwi atoe ushahidi kwa kukisia au kudhania au kwa kusikia maneno yasiyokuwa ya uhakika.

 

[7] Tunapata uthibitisho wa Hadiyth hii kuwa kama hakuna mashahidi wawili basi mmoja anatosheleza pamoja na kiapo cha mdai. Ikiwa katika hali ambayo hakuna shahidi, wakati huo kiapo cha madai hakitotosheleza katika kusimamisha madai yake. Katika hali hiyo, mdaiwa atatakiwa kuleta kiapo cha kukana mashtaka dhidi yake.

Share