00-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Ukombozi

 

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

 

كِتَابُ اَلْعِتْقِ

00-Kitabu Cha Ukombozi

 

 

 

 

 

 

1220.

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏{"أَيُّمَا امْرِئٍ مُسْلِمٍ أَعْتَقَ اِمْرَأً مُسْلِماً، اِسْتَنْقَذ َ‏ اَللَّهُ بِكُلِّ عُضْوٍ مِنْهُ عُضْوًا مِنْهُ مِنَ النَّارِ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَلِلتِّرْمِذِيِّ وَصَحَّحَهُ، عَنْ أَبِي أُمَامَةَ: {"وَأَيُّمَا امْرِئٍ مُسْلِمٍ أَعْتَقَ اِمْرَأَتَيْنِ مُسْلِمَتَيْنِ، كَانَتَا فِكَاكَهُ مِنَ النَّارِ"}

وَلِأَبِي دَاوُدَ: مِنْ حَدِيثِ كَعْبِ بْنِ مُرَّةَ: {"وَأَيُّمَا اِمْرَأَةٍ أَعْتَقَتْ اِمْرَأَةً مُسْلِمَةً، كَانَتْ فِكَاكَهَا مِنْ اَلنَّارِ}

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Muislaam yeyote atakayemkomboa Muislaam mwenzake, Allaah Atamuacha huru na moto,[1] kila kiungo chake kwa kila kiungo cha mtu huyo.” [Bukhaariy, Muslim]

At-Tirmidhiy amepokea na ameisahihisha kutoka kwa Abuu Umaamah: “Na mtu yeyote Muislaam atakayekomboa wanawake wawili Waislaam basi watakuwa ni kuokoka kwake dhidi ya moto.”

Abuu Daawuwd amepokea kutoka katika Hadiyth ya Ka’b bin Murrah[2]: “Na mwanamke yeyote Muislaam atakayemkomboa mwanamke Muislaam basi atakuwa ni kuokoka kwake dhidi ya moto.”

 

 

 

1221.

وَعَنْ أَبِي ذَرٍّ رضى الله عنه ‏ {قَالَ: سَأَلْتُ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏أَيُّ اَلْعَمَلِ أَفْضَلُ؟ قَالَ: "إِيمَانٌ بِاَللَّهِ، وَجِهَادٌ فِي سَبِيلِهِ" .‏ قُلْتُ: فَأَيُّ اَلرِّقَابِ أَفْضَلُ؟ قَالَ: " أَعْلَاهَا ‏ ثَمَنًا، وَأَنْفَسُهَا عِنْدَ أَهْلِهَا"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Dharr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilimuuliza Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ni amali gani bora zaidi? Akasema: ‘Ni kumuamini Allaah na jihaad katika njia yake’ Nikasema: ni kuacha kupi mtumwa huru kuliko bora? Akasema: “Mwenye thamani kubwa na mzuri zaidi kwa watu wake.” [Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

1222.

وَعَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{"مَنْ أَعْتَقَ شِرْكًا لَهُ فِي عَبْدٍ، فَكَانَ لَهُ مَالٌ يَبْلُغُ ثَمَنَ اَلْعَبْدِ، قُوِّمَ قِيمَةَ عَدْلٍ، فَأَعْطَى شُرَكَاءَهُ حِصَصَهُمْ، وَعَتَقَ عَلَيْهِ اَلْعَبْدُ، وَإِلَّا فَقَدْ عَتَقَ مِنْهُ مَا عَتَقَ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْه ِ

وَلَهُمَا: عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رضى الله عنه {"وَإِلَّا قُوِّمَ عَلَيْهِ، وَاسْتُسْعِيَ غَيْرَ مَشْقُوقٍ عَلَيْهِ"} وَقِيلَ: إِنَّ اَلسِّعَايَةَ مُدْرَجَةٌ فِي اَلْخَبَر ِ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuacha huru fungu lake katika mtumwa akawa na mali inayofikia thamani ya mtumwa (yule), atathaminishwa thamani ya uadilifu awape washirika wake mafungu yao na atamuacha huru mtumwa.[3] Vinginevyo atakuwa ameacha huru katika fungu lake.” [Bukhaariy, Muslim]

Wamepokea kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “La si hivyo atathaminishwa na aombwe kufanya kazi ili alipie ushuru wake bila kumtia uzito.” Imesemwa haya ya kufanya kazi ni maneno Mudrajah (yaliyoingizwa na siyo ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ

 

 

 

1223.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏{" لَا يَجْزِي وَلَدٌ وَالِدَهُ، إِلَّا أَنْ يَجِدَهُ مَمْلُوكًا فَيُعْتِقَهُ"} رَوَاهُ مُسْلِم ٌ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mtoto hawezi kumlipa mzazi wake isipokuwa amkute ni mtumwa amnunue na amuache huru.”[4] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

1224.

وَعَنْ سَمُرَةَ ‏ رضى الله عنه أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {"مَنْ مَلَكَ ذَا رَحِمٍ مَحْرَمٍ، فَهُوَ حُرٌّ"} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَة ُ وَرَجَّحَ جَمْعٌ مِنَ الْحُفَّاظِ أَنَّهُ مَوْقُوف ٌ

Kutoka kwa Samurah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kumiliki mwenye kizazi ambaye ni maharimu,[5] basi yuko huru.” [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah). Kundi la wahifadhi Hadiyth wametilia nguvu kuwa ni Mawquwf]

 

 

 

1225.

وَعَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، {أَنَّ رَجُلاً أَعْتَقَ سِتَّةً مَمْلُوكِينَ لَهُ، عِنْدَ مَوْتِهِ، لَمْ يَكُنْ لَهُ مَالٌ غَيْرَهُمْ، فَدَعَا بِهِمْ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏فَجَزَّأَهُمْ أَثْلَاثًا، ثُمَّ أَقْرَعَ بَيْنَهُمْ، فَأَعْتَقَ اِثْنَيْنِ، وَأَرَقَّ أَرْبَعَةً، وَقَالَ لَهُ قَوْلاً شَدِيدًا} رَوَاهُ مُسْلِم ٌ

Kutoka kwa ‘Imraan bin Huswayn (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Mtu mmoja aliwaacha huru watumwa sita wakati wa kifo chake wala hakuwa na mali zaidi ya hiyo.[6] Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akawaita akawagawa mafungu matatu kisha akapiga kura miongoni mwao, akawaacha huru wawili na wanne akawabakisha kwenye utumwa. Na akamuambia maneno mazito yule mwenyewe.”[7] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

1226.

وَعَنْ سَفِينَةَ رضى الله عنه {قَالَ: كُنْتُ مَمْلُوكًا لِأُمِّ سَلَمَةَ فَقَالَتْ: أُعْتِقُكَ، وَأَشْتَرِطُ عَلَيْكَ أَنْ تَخْدِمَ رَسُولَ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏مَا عِشْتَ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَالْحَاكِم ُ

Kutoka kwa Safiynah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilikuwa mtumwa wa Ummu Salamah akaniambia: ‘Nitakuacha huru na nitakupa sharti uwe ukimtumikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika maisha yako.”[8] [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy na Al-Haakim]

 

 

 

1227.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا، أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {"إِنَّمَا اَلْوَلَاءُ لِمَنْ أَعْتَقَ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ فِي حَدِيث ٍ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika Al-Walaau ni wa mwenye kuacha huru.”[9] [Bukhaariy, Muslim katika Hadiyth ndefu]

 

 

 

1228.

وَعَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{" اَلْوَلَاءُ لُحْمَةٌ كَلُحْمَةِ اَلنَّسَبِ، لَا يُبَاعُ وَلَا يُوهَبُ"} رَوَاهُ اَلشَّافِعِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِم ُ‏ وَأَصْلُهُ فِي "اَلصَّحِيحَيْنِ" بِغَيْرِ هَذَا اَللَّفْظ ِ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Al-Walaau ni undugu kama undugu wa nasaba, hauuzwi wala hautolewi bure (hiba/zawadi).” [Imetolewa na Ash-Shaafi’iy na akaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim. Asili yake imo katika Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Al-Muslim kwa tamshi lingine lisilokuwa hili]

 

[1] Malipo na thawabu ayapatayo mtu ni yale ya kumuacha huru mtumwa Muumini, Pamoja na kuwa kuna malipo na fadhila za kumuacha huru mtumwa kafiri. Hata hivyo kumuacha huru mtumwa Muumini kuna malipo makubwa zaidi.

[2] Ka’b bin Murrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alikuwa ni Swahaba na inasemekana kuwa alikuwa akiitwa Murrah bin Ka’b. Aliishi Basra kisha akahamia Jordan hadi yalipomkuta mauti yake mwaka 57 au 59 Hijriyyah.

[3] Hadiyth hii inatujulisha kuwa mtumwa ambae ameacha huru nusu ana hadhi ya dhamana iliyozuiwa hawezi kuuzwa au kutolewa kama zawadi.

[4] Kulingana na Hadiyth hii Wanazuoni wa Zahiriyah wana muono kuwa baba hawezi kuzingatiwa kuwa yuko huru kwa sharti la kulipiwa na mwanae, bali atakuwa huru hadi mwanae atakapotamka hivyo. Wanazuoni wengine wanaona kuwa baba keshakuwa huru madamu amenunuliwa na mwanae. Hukumu hii pia inamhusu mama. Hadiyth hii kwa upande mmoja inatuelezea nafasi za wazazi wawili na kwa upande mwingine inaelezea fadhila za kumuacha huru mtumwa.

 

[5] Ndugu wa karibu kama vile baba, mtoto, kaka, dada, ndugu ya baba, kaka wa mama n.k. ambao wapo karibu kiasi cha kuwa huwezi kuoa (au kuolewa) hawawezi kuwa katika hadhi ya mtumwa na bwana wake. Ikiwa aliyekuwa utumwani ni mwanamke, basi hukumu inakuwa ni wazi zaidi. Katika hali hiyo itaangaliwa kama wanaweza kuoana au sivyo. Kama ni sawa, basi hukumu ile inatumika kwao, kwani watakuwa ni Mahram.

[6] Mafundisho tunayoyapata katika Hadiyth hii ni kuwa swadaqah inayotolewa na mtu mgonjwa ni kama vile kuacha wasia. Mtu haruhusiwi kuacha wasia zaidi ya theluthi ya mali yake au kama ni zawadi au wakfu. Maneno makali aliyoyasema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kwa mtu yule yalikuwa: “Kama ningejulishwa habari za mtu yule hapo kabla basi nisingeruhusu kuzikwa katika makaburi ya Waislaam.”

 

[7] Kwa sababu theluthi mbili za mali ya marehemu yanatakiwa kuenda kwa warithi wake.

[8] Kuwa inawezekana kuweka sharti unapoacha huru mtumwa kama alivyofanya Ummu Salamah kuwa aendelee kumtumikia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kwa muda uliokubaliwa. Uhalaal wa hili unaonekana pale Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa hakulikataza jambo hili.

 

[9] Al-Walaau ni mirathi ya mtumwa aliyeachwa huru inamilikiwa na aliyemuacha huru. Haitakiwi kuuzwa wala kutolewa zawadi.

Share