01-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Ukombozi: Mlango Wa Mudabbar, Al-Mukaatab Na Ummul-Walad

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْعِتْقِ

Kitabu Cha Ukombozi

 

بَابُ اَلْمُدَبَّرِ وَالْمُكَاتَبِ وَأُمِّ اَلْوَلَدِ

01-Mlango Wa Mudabbar,[1] Al-Mukaatab[2] Na Ummul-Walad[3]

 

 

 

1229.

عَنْ جَابِرٍ رضى الله عنه {أَنَّ رَجُلًا مِنْ اَلْأَنْصَارِ أَعْتَقَ غُلَامًا لَهُ عَنْ دُبُرٍ، لَمْ يَكُنْ لَهُ مَالٌ غَيْرُهُ، فَبَلَغَ ذَلِكَ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم .‏ فَقَالَ: "مَنْ يَشْتَرِيهِ مِنِّي؟" فَاشْتَرَاهُ نُعَيْمُ بْنُ عَبْدِ اَللَّهِ بِثَمَانِمَائَةِ دِرْهَمٍ} مُتَّفَقٌ عَلَيْه ِ‏ وَفِي لَفْظٍ لِلْبُخَارِيِّ: فَاحْتَاج َ‏ وَفِي رِوَايَةٍ لِلنَّسَائِيِّ: {وَكَانَ عَلَيْهِ دَيْنٌ، فَبَاعَهُ بِثَمَانِمَائَةِ دِرْهَمٍ، فَأَعْطَاهُ وَقَالَ: " اِقْضِ دَيْنَكَ"}

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Mtu mmoja miongoni mwa Answaar aliahidi uhuru wa mtumwa wake[4] baada ya kufa hakuwa na mali isipokuwa mtumwa huyo. Habari hiyo ikamfikia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: ‘Ni nani atakayemnunua?’ Nu’aym bin ‘Abdillaah[5] akamnunua kwa dirhamu mia nane.” [Bukhaariy, Muslim, katika tamshi lingine la Al-Bukhaariy: ‘akahitajia’]

Katika Riwaayah ya An-Nisaaiy: “Alikuwa ana deni akamuuza kwa dirhamu mia nane na akampa mwenyewe akamuambia: ‘lipa deni lako’.”

 

 

1230.

وَعَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم {قَالَ: " اَلْمُكَاتَبُ عَبْدٌ مَا بَقِيَ عَلَيْهِ مِنْ مُكَاتَبَتِهِ دِرْهَمٌ"} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ بِإِسْنَادٍ حَسَن ٍ‏ وَأَصْلُهُ عِنْدَ أَحْمَدَ، وَالثَّلَاثَةِ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِم ُ

Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb amepokea kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Al-Mukaatab ni mtumwa madamu katika mkataba wake imebakia dirhamu moja.”[6] [Imetolewa na Abuu Daawuwd kwa Isnaad Hasan. Asili yake imo kwa Ahmad na Ath-Thalaathah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd) na akaisahihisha Al-Haakim]

 

 

 

1231.

وَعَنْ أَمِّ سَلَمَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم {إِذَا كَانَ لِإِحْدَاكُنَّ مُكَاتَبٌ، وَكَانَ عِنْدَهُ مَا يُؤَدِّي، فَلْتَحْتَجِبْ مِنْهُ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَة ُ‏ وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيّ ُ

Kutoka kwa Ummu Salamah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Iwapo mmoja wenu ana Mukaatab naye anacho cha kutoa basi ajisitiri kwake.”[7] [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na akaisahihisha At-Tirmidhiy]

 

 

 

1232.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ اَلنَّبِيَّ  صلى الله عليه وسلم قَالَ: {يُودَى اَلْمُكَاتَبُ بِقَدْرِ مَا عَتَقَ مِنْهُ دِيَةَ اَلْحُرِّ، وَبِقَدْرِ مَا رَقَّ مِنْهُ دِيَةَ اَلْعَبْدِ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيّ ُ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Al-Mukaatab hufidiwa fidiya ya muungwana kiasi alicholipia katika mali ya kuandikiana na hufidiwa fidiya ya mtumwa kiasi kilichobakia katika deni.”[8] [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd na An-Nisaaiy]

 

 

 

1233.

وَعَنْ عَمْرِو بْنِ اَلْحَارِثِ أَخِي جُوَيْرِيَةَ أُمِّ اَلْمُؤْمِنِينَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {مَا تَرَكَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم عِنْدَ مَوْتِهِ دِرْهَمًا، وَلَا دِينَارًا، وَلَا عَبْدًا، وَلَا أَمَةً، وَلَا شَيْئًا، إِلَّا بَغْلَتَهُ اَلْبَيْضَاءَ، وَسِلَاحَهُ، وَأَرْضًا جَعَلَهَا صَدَقَةً} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيّ ُ

Kutoka kwa ‘Amr bin Al-Haarith[9] nduguye Juwayriyah Ummul-Mu-miniyna (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipofariki hakuacha dirhamu wala dinari wala mtumwa wala mjakazi wala chochote isipokuwa nyumbu wake mweupe, silaha yake na ardhi aliyoitoa swadaqah.”[10] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

1234.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم {أَيُّمَا أَمَةٍ وَلَدَتْ مِنْ سَيِّدِهَا، فَهِيَ حُرَّةٌ بَعْدَ مَوْتِهِ} أَخْرَجَهُ اِبْنُ مَاجَهْ، وَالْحَاكِمُ بِإِسْنَادٍ ضَعِيف ٍ

وَرَجَّحَ جَمَاعَةٌ وَقْفَهُ عَلَى عُمَرَ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mjakazi yeyote aliyezaa na bwana wake, basi yuko huru baada ya kufa kwake.” [Imetolewa na Ibn Maajah na Al-Haakim kwa Isnaad Dhaifu. Kundi la Wanazuoni wa Hadiyth wana mtazamo kuwa Hadiyth hii ni Mawquwf kwa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)]

 

 

 

1235.

وَعَنْ سَهْلِ بْنِ حُنَيْفٍ رضى الله عنه أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم قَالَ: {مَنْ أَعَانَ مُجَاهِدًا فِي سَبِيلِ اَللَّهِ، أَوْ غَارِمًا فِي عُسْرَتِهِ، أَوْ مُكَاتَبًا فِي رَقَبَتِهِ، أَظَلَّهُ اَللَّهُ يَوْمَ لَا ظِلَّ إِلَّا ظِلُّهُ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِم ُ

Kutoka kwa Sahl bin Hunayaf (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kumsaidia mpigana jihaad katika Njia ya Allaah, au mwenye deni katika uzito wake, au Mukaatab katika utumwa wake, Allaah Atamfunika kivuli siku ambayo hakuna kivuli isipokuwa kivuli Chake.” [Imetolewa na Ahmad na akaisahihisha Al-Haakim]

 

 

[1] Ni maneno anayoambiwa mtumwa na bwana wake, “Uko huru baada ya kufa kwangu.”

 

[2] Mtumwa anapoingia katika mkataba na bwana wake ili anunue uhuru wake.

 

[3] Kijakazi anayemzalia bwana wake.

 

[4] Tumejifunza katika Hadiyth hii kuwa bwana anaweza kumuacha mtumwa wake Mudabbar, maadamu ya kuwa hayuko katika hali ya ugonjwa. Wanazuoni wana muono kuwa ichukuliwe kutoka katika theluthi ya mali yake kama usia. Wanazuoni wengine wanaona kuwa ruhusa kumuuza Mudabbar ila kwa mahitaji, au kulipa madeni ya bwana wake.

 

[5] Kun-ya yake ilikuwa ni An-Nakhkham, alikuwa Mqurayshi wa ukoo wa ‘Aad. Alisilimu mda mrefu akafanya kuwa ni siri, alipotaka kuhama watu wa kabila lake wakamtaka akae na afuate dini aitakayo, kwani alikuwa akiwasaidia wajane wao na mayatima wao, hivyo alibaki. Alihama katika mwaka wa Hudaybiyah. Aliuwawa katika Fat-hi ya Shaam wakati wa Ukhalifa wa Abuu Bakr Asw-Swidiq au wa ‘Umar Al-Faruwq.

 

[6] Ina maana kuwa ikiwa Al-Mukaatab hajamaliza deni lake kulipa dhamana yake, ataendelea kubaki kuwa ni mtumwa. Hili linathibitisha nukta moja kuwa mtumwa anamiliki anachopata. Haina maana kuwa mtumwa hawezi kumiliki kitu. Al-Mukaatab ni mwanamme au mwanamke mtumwa ambaye anaingia katika mkataba na bwana wake kuwa iwapo atamuacha huru atampa kadha na kadha kwa ajili ya uhuru wake. Aina hii ya mkataba unaitwa Mukaatabah na mtumwa anayeingia katika mkataba huu anaitwa Al-Mukaatab.

 

[7] Bi mkubwa kishariy’ah hana haja ya kuficha uso wake kwa mtumwa wake, kwani anakuwa kama mtoto wake. Lakini ikiwa Al-Mukaatab ameshakusanya kiasi cha fedha cha kujikomboa, itabidi aanze kuvaa hijab kamili kwake. Hadiyth hii inabainisha kuwa maadamu Al-Mukaatab hajakamilisha malipo kamili katika mkataba wake bado anahesabiwa kuwa ni mtumwa.

[8] Al-Khatwaab amesema: “Makubaliano ya Wanazuoni wa Fiqh ni kuwa Al-Mukaatab ni mtumwa kulingana na adhabu pamoja na fidiya, muda wa kuwa bado hajakamilisha dirhamu moja. Hata hivyo, Ibraahiym An-Nakhai na rai kutoka kwa ‘Aliy wanakubaliana na maana ya wazi yaliyopokewa kutoka kwenye Hadiyth hii.”

 

[9] Huyu ni Al-Haarith bin Abuu Dhirar bin Habib Al-Khuza’i Al-Mustwaliqi. Alikuwa ni Swahaba na ana Hadiyth moja tu kulingana na Wanazuoni wa Hadiyth.

 

[10] Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipofariki, Maria Qibtwiyyah mama wa mtoto wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Ibraahiym alikuwa bado yu hai. Alikuwa ni mtumwa wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Kwa kuwa alikuwa mama wa mtoto wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), alikuwa huru baada ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kufariki. Lengo la kutaja Hadiyth hii ni kuwa Ummul-Walad (mtumwa wa kike aliyemzalia bwana wake), anakuwa huru baada ya kufariki bwana mwenyewe.

Share