Vitumbua Vya Kuku Vya Mboga Na Jibini (Cheese)
Vitumbua Vya Kuku Vya Mboga Na Jibini (Cheese)
Vipimo
Kidari cha kuku – kilo 1
Tangawizi na kitunguu thomu ilosagwa – 1 kijiko cha supu
Paprika – 1 kijiko cha chai
Jira (bizari ya cumin) – 1 kijiko cha chai
Bizari ya mchuzi – 1 kijiko cha chai
Kitunguu maji – 2 katakata
Karoti – 1 moja katakata nyembamba
Pilipili (capsicum) kubwa la kijani – kiasi katakata
Pilipili kubwa (capsicum) jekundu – kiasi katakata
Jibini (Cheese) ya cheddar – ilokunwa – kiasi
Mayai – 3 au 4
Baking powder – 1 ikijiko cha chai
Unga wa dengu – 1 kijko ukihitajika (ikiwa mchanganyiko umekuwa wa majimaji)
Chumvi – kiasi
Mafuta ya kuchomea
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Chemsha kuku kwa bizari zote, tia chumvi, kitunguu thomu na tangawizi
- Weka katika machine la kukatia kidogodogo (Chopper) usage kiasi. Kama huna chopper tumia blender lakini usisage mpaka ikavurugika mno.
- Mimina katika bakuli.
- Tia vitunguu na mboga zote zilobakia changanya vizuri
- Tia jibini (cheese)
- Piga mayai katika kibakuli kisha changanya.
- Tia baking powder. Ikiwa mchanganyiko umekuwa majimaji tia unga wa dengu kiasi changanya. Ikiwa mzito, ongezea yai.
- Weka chuma cha vitumbua uchome kama unavyopika vitumbua
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)