52-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ametumwa Kubashiria Na Kuonya Walimwengu

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

52-Ametumwa Kubashiria Na Kuonya Walimwengu

 

www.alhidaaya.com

 

 

Kama ilivyotangulia fadhila ya kuwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ametumwa kwa Walimwengu wote, basi kubashiria na kuonya kwake hali kadhalika ni kwa ajili ya ulimwengu mzima na si kaumu yake tu kama ilivyokuwa desturi ya Manabii wengineo kabla yake:

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):   

 

تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَىٰ عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا ﴿١﴾

Amebarikika Ambaye Ameteremsha kwa mja Wake pambanuo (la haki na batili) ili awe muonyaji kwa walimwengu. [Al-Furqaan: 1]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

أَكَانَ لِلنَّاسِ عَجَبًا أَنْ أَوْحَيْنَا إِلَىٰ رَجُلٍ مِّنْهُمْ أَنْ أَنذِرِ النَّاسَ وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا أَنَّ لَهُمْ قَدَمَ صِدْقٍ عِندَ رَبِّهِمْ ۗ قَالَ الْكَافِرُونَ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ مُّبِينٌ﴿٢﴾

Je, imekuwa ni ajabu kwa watu kwamba Tumemfunulia Wahy mtu miongoni mwao kwamba: Waonye watu na wabashirie wale walioamini kwamba watapata cheo kitukufu mbele ya Rabb wao. Makafiri wakasema: Hakika huyu bila shaka ni mchawi bayana. [Yuwnus: 2]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَأَرْسَلْنَاكَ لِلنَّاسِ رَسُولًا ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا ﴿٧٩﴾

Na Tumekutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa watu uwe Rasuli na inatosheleza Allaah kuwa ni Mwenye kushuhudia yote. [An-Nisaa: 79]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ ۚ

Na nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayomfikia.[Al-An’aam: 19]

 

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا ﴿٤٥﴾

Ee Nabiy! Hakika Sisi Tumekutuma uwe shahidi, na mbashiriaji na mwonyaji.

 

وَدَاعِيًا إِلَى اللَّـهِ بِإِذْنِهِ وَسِرَاجًا مُّنِيرًا ﴿٤٦﴾

Na mlinganiaji kwa Allaah kwa idhini Yake; na siraji kali yenye nuru.

 

وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ بِأَنَّ لَهُم مِّنَ اللَّـهِ فَضْلًا كَبِيرًا ﴿٤٧﴾

Na wabashirie Waumini kwamba watapata kutoka kwa Allaah fadhila kubwa.

 

وَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَالْمُنَافِقِينَ وَدَعْ أَذَاهُمْ وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿٤٨﴾

Na wala usiwatii makafiri na wanafiki, na achilia mbali maudhi yao, na tawakali kwa Allaah. Na Allaah Anatosheleza kuwa Mdhamini. [Al-Ahzaab: 45-48]

 

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٦٧﴾

Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako. Na usipofanya, basi utakuwa hukubalighisha ujumbe Wake. Na Allaah Atakuhifadhi dhidi ya watu. Hakika Allaah Haongoi watu makafiri [Al-Maaidah: 67]

 

 

Bonyeza kiungo kifuatacho upate faida  inayohusiana na maudhui ya fadhila hii:

 

 

02-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ametumwa Kwa Walimwengu Wote

 

 

 

 

Share