53-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Amepewa Ummah Bora Kabisa
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
53-Amepewa Ummah Bora Kabisa
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿١١٠﴾
Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. Na lau wangeliamini Ahlul-Kitaabi ingelikuwa ni bora kwao, miongoni mwao wanaoamini na wengi wao ni mafasiki [Aal-‘Imraan: 110]
Na Hadiyth zinathibitisha na kufafanua zaidi:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَة َ رضى الله عنه ((كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ)) قَالَ خَيْرَ النَّاسِ لِلنَّاسِ، تَأْتُونَ بِهِمْ فِي السَّلاَسِلِ فِي أَعْنَاقِهِمْ حَتَّى يَدْخُلُوا فِي الإِسْلاَمِ.
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kuhusu:
كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ
"Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu"
Kasema: “Watu bora kabisa kati ya watu, mtawajia kwa minyororo katika shingo zao mpaka waingie Uislamu.” [Al-Bukhaariy]
تَأْتُونَ بِهِمْ فِي السَّلاَسِلِ فِي أَعْنَاقِهِمْ حَتَّى يَدْخُلُوا فِي الإِسْلاَمِ
Maana ya: “Mtawajia kwa minyororo katika shingo zao mpaka waingie Uislamu.”
“Ni matekwa waliokamatwa na Waislamu, basi Allaah huwaongoza na kuingia katika Uislaam kwa hivyo wanafaidika na kuingia Peponi. Hii ni katika neema adhimu na fadhila za Allaah juu ya matekwa kisha wakaingia Uislamu na hawakuuawa na makafiri.” [Imaam Ibn Baaz – Sharh Riyaadhw Asw-Swaalihiyn]
Na pia:
عَنْ بَهْزِ بْنِ حَكِيمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ فِي قَوْلِهِ كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ قَالَ " إِنَّكُمْ تُتِمُّونَ سَبْعِينَ أُمَّةً أَنْتُمْ خَيْرُهَا وَأَكْرَمُهَا عَلَى اللَّهِ "
Kutoka kwa Bahz bin Haakim, kutoka baba yake, kutoka kwa babu yake kwamba kamsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema kuhusu kauli ya Allaah:
كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ
Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu
Nyinyi ni umaliziaji wa mataifa sabini, nyie ndiye bora zaidi, na ndiyo (Ummah) mtukufu bora mbele ya Allaah. [Hadiyth Hasan At-Tirmidhiy]
Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ
Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu na awe Rasuli shahidi juu yenu. [Al-Baqrah: 143]