01-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuomba Maghfirah

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب الأمر بالاستغفار وفضله

01-Mlango Wa Kuomba Maghfirah

 

 

قَالَ الله تَعَالَى:

وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مُتَقَلَّبَكُمْ وَمَثْوَاكُمْ﴿١٩﴾

Na omba maghfirah kwa dhambi zako na kwa ajili ya Waumini wa kiume na Waumini wa kike. Na Allaah Anajua harakati zenu huku na kule na pahala penu pa kupumzikia. [Muhammad: 19]

 

وَاسْتَغْفِرِ اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٠٦﴾

Na muombe Allaah maghfirah. Hakika Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [An-Nisaa: 106]

 

فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَاسْتَغْفِرْهُۚ إِنَّهُ كَانَ تَوَّابًا ﴿٣﴾

Basi sabbih kwa Himidi za Rabb wako na muombe maghfirah; hakika Yeye daima ni Mwingi mno wa kupokea tawbah. [An-Naswr :3]

 

لِلَّذِينَ اتَّقَوْا عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَأَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ وَرِضْوَانٌ مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴿١٥﴾

Sema: Je, nikujulisheni yaliyo bora kuliko hayo? Kwa wale waliokuwa na taqwa kwa Rabb wao watapata Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo na wake waliotakasika na radhi kutoka kwa Allaah. Na Allaah ni Mwenye kuwaona waja.

 

 الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا إِنَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ﴿١٦﴾ 

Wale wasemao: Rabb wetu, hakika sisi tumeamini, basi Tughufurie madhambi yetu na Tukinge na adhabu ya moto.

 

 الصَّابِرِينَ وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنفِقِينَ وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ﴿١٧﴾

Wenye kusubiri na wasemao kweli, na watiifu, na watoaji mali katika njia ya Allaah na waombao maghfirah kabla ya Alfajiri. [Aal-‘Imraan: 15-17]

 

وَمَن يَعْمَلْ سُوءًا أَوْ يَظْلِمْ نَفْسَهُ ثُمَّ يَسْتَغْفِرِ اللَّـهَ يَجِدِ اللَّـهَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١١٠﴾

110. Na atakayetenda ovu au akajidhulumu nafsi yake; kisha akamwomba Allaah maghfirah; atamkuta Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [An-Nisaa: 110]

 

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُعَذِّبَهُمْ وَأَنتَ فِيهِمْ ۚ وَمَا كَانَ اللَّـهُ مُعَذِّبَهُمْ وَهُمْ يَسْتَغْفِرُونَ﴿٣٣﴾

33. Na Allaah Hakuwa wa kuwaadhibu na hali wewe (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uko nao. Na Allaah Hakuwa wa kuwaadhibu hali wao wanaomba maghfirah. [Al-Anfaal: 33]

 

وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٣٥﴾

135. Na wale ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao (kwa maasi), humdhukuru Allaah wakaomba maghfirah kwa madhambi yao. Na nani anayeghufuria madhambi isipokuwa Allaah. Na hawaendelei katika waliyoyafanya na wao wanajua.

[Aal-‘Imraan: 135]

 

 

              Hadiyth – 1

وعن الأَغَرِّ المزني رضي الله عنه: أنَّ رسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم قال : (( إنَّهُ لَيُغَانُ عَلَى قَلْبِي ، وإنِّي لأَسْتَغفِرُ اللهَ في اليَوْمِ مِئَةَ مَرَّةٍ )) . رواه مسلم .

Al-Agharri al-Mazany  (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: " Kwa hakika wakati mwengine huwa nikihisi moyo wangu umeghumiwa. Kwa hakika mimi humuomba Allaah maghfirah mara mia kwa siku. [Muslim]   

 

 

 Hadiyth – 2

وعن أبي هريرة رضي الله عنه، قال : سَمعتُ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم، يقولُ :  (( وَاللهِ إنِّي لأَسْتَغْفِرُ اللهَ وَأتُوبُ إلَيْهِ فِي اليَومِ أَكْثَرَ مِنْ سَبْعِينَ مَرَّةً )) رواه البخاري .

Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “NilimsIkia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Wa-Allaahi mimi namuomba Allaah maghfirah na natubia Kwake zaidi ya mara sabini kwa siku.” [Al-Bukhaariy]

 

 

 Hadiyth – 3

وعن أبي هريرة  رضي الله عنه، قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَوْ لَمْ تُذْنِبُوا ، لَذَهَبَ اللهُ تَعَالَى بِكُمْ ، وَلَجَاءَ بِقَومٍ يُذْنِبُونَ ، فَيَسْتَغْفِرُونَ اللهَ تَعَالَى ، فَيَغْفِرُ لَهُمْ )) رواه مسلم

Abu Huraiyrah amesema: “Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Naapa kwa ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake! Lau mngalikuwa hamtendi dhambi, Allaah Angaliwaondoa na Akawaleta watu wanaotenda dhambi, wakamuaomba Allaah maghfira Naye Akawasamehe.”  [Muslim]

 

 

Hadiyth – 4

وعن ابن عمر رَضِي الله عنهما ، قال : كُنَّا نَعُدُّ لرسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم في المَجْلِسِ الواحِدِ مئَةَ مَرَّةٍ : (( رَبِّ اغْفِرْ لِي وَتُبْ عَلَيَّ إنَّكَ أَنْتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ )) . رواه أبو داود والترمذي ، وقال :

(( حديث حسن صحيح غريب ))

‘Abdullah bin ‘Umar amesimulia: “Tulikuwa tukimhisabia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika kikao kimoja akisema mara mia: “Rabbighfirli watub ‘alayya innaka antattawwaburrahim [Ee Mola, Nisamehe na Unikubalie toba, hakika wewe ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu]”. [Abu Daawuud na Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth hi ni Swahiyh].

 

 

Hadiyth – 5

وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ لَزِمَ الاسْتِغْفَارَ جَعَلَ اللهُ لَهُ مِنْ كُلِّ ضِيقٍ مَخْرَجاً ، وَمِنْ كُلِّ هَمٍّ فَرَجاً ، وَرَزَقهُ مِنْ حَيثُ لاَ يَحْتَسِبُ )) . رواه أبو داود .

Abdullah bin ‘Abbas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwenye kudumisha kuleta istighfari, Allaah atamjaalia matokeo katika kila dhiki, Atamjaalia faraja kutokana na kila hamu na Atamruzuku kwa namna asiyodhania.” [Abu Dawuud]

 

Hadiyth – 6

وعن ابن مسعود رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ قَالَ : أسْتَغْفِرُ اللهَ الَّذِي لاَ إلَهَ إلاَّ هُوَ الحَيُّ القَيُومُ وَأتُوبُ إلَيهِ ، غُفِرَتْ ذُنُوبُهُ ، وإنْ كانَ قَدْ فَرَّ مِنَ الزَّحْفِ )) . رواه أبو داود والترمذي والحاكم ، وقال : (( حديث صحيح على شرط البخاري ومسلم ))

Abdullah bin Mas’ud (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwenye kusema: “Astaghfirullahalladhi la ilaha ila huwal-hayyulqayyumu wa atubu ilaih” [Namuomba msamaha Allaah Ambaye hakuna anyestahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa ni Yeye Alie Hai, Msimamia kila jambo, na natubia Kwake,] atasamehewa dhambi zake hata kama alikimbia vitani.” [Abu Dawuud, Tirmidhiy na Al-Haakim, na amesema: Hadiyth hii ni Swahiyh kwa sharti ya Bukhaariy na Muslim].

 

Hadiyth – 7

وعن شَدَّادِ بْنِ أَوسٍ رضي الله عنه ، عن النبيّ صلى الله عليه وسلم ، قال : (( سَيِّدُ الاسْتِغْفَارِ أَنْ يَقُولَ العَبْدُ : اللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لاَ إلهَ إلاَّ أنْتَ خَلَقْتَنِي وَأَنَا عَبْدُكَ ، وَأنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ ، أعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ ، أبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ ، وأبُوءُ بِذَنْبِي ، فَاغْفِرْ لِي ، فَإنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إلاَّ أنْتَ . مَنْ قَالَهَا مِنَ النَّهَارِ مُوقِناً بِهَا ، فَمَاتَ مِنْ يَوْمِهِ قَبْلَ أَنْ يُمْسِي ، فَهُوَ مِنْ أهْلِ الجَنَّةِ ، وَمَنْ قَالَهَا مِنَ اللَّيْلِ ، وَهُوَ مُوقِنٌ بِهَا ، فَمَاتَ قَبْلَ أنْ يُصْبِحَ ، فَهُوَ مِنْ أهْلِ الجَنَّةِ )) . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Shaddaad bin Aws (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Sayyidul Istighfaar ni mja kusema: Allaahumma Anta Rabbiy Laa ilaaha illa Anta Khalaqtaniy wa Ana 'Abduka wa ana 'alaa 'Ahdika wa Wa'dika mastatwa'tu A'uwdhu bika min sharri maa swana'tu abuu` laka bini'matika 'alayya wa abuu` bidhambi Faghfirliy Fa`innahu laa Yaghfirudh dhunuwba illa Anta (Ee Mola wangu! Wewe Ndiye Rabb wangu, hakuna muabudiwa isipokuwa Wewe. Wewe Ndiye Uliyeniumba nami ni mtumwa Wako, nami niko katika kutekeleza ile ahadi na agano langu Nawe ninavyoweza. Ninajilinda Kwako kwa shari ya yale ninayofanya. Na hakika natambua neema Zako kwangu na ninakubali kwa dhambi (ninazofanya). Hivyo, nisamehe kwani hapana anayesamehe dhambi isipokuwa Wewe). Mwenye kusema hayo mchana kwa yakini nayo na akafa katika siku yake hiyo kabla hakujakucha, atakuwa ni miongoni mwa watu wa Peponi. Na mwenye kusema usiku, akiwa na yakini nayo (maneno hayo), akafa kabla  kupambazuka (katika usiku wake huo), atakuwa miongoni mwa watu wa Peponi." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 8

وعن ثوبان رضي الله عنه قال : كانَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم إذَا انْصَرَفَ مِنْ صَلاَتِهِ، اسْتَغْفَرَ اللهَ ثَلاَثاً وَقَالَ : (( اللَّهُمَّ أنْتَ السَّلاَمُ ، وَمِنْكَ السَّلاَمُ ، تَبَارَكْتَ يَاذَا الجَلاَلِ وَالإكْرَامِ )) قيلَ لِلأوْزَاعِيِّ – وَهُوَ أَحَدُ رُوَاتِهِ - : كَيفَ الاسْتِغْفَارُ ؟ قال : يقُولُ : أسْتَغْفِرُ اللهَ ، أسْتَغْفِرُ اللهَ . رواه مسلم .

Amesema Thawbaan (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anapomaliza Swalaah yake akileta Istighfaar mara tatu (Astaghfiru Allaah), kisha anasoma: "Allaahumma Antas Salaamu wa Minkas Salaamu Tabaarakta yadgal Jalaal wal Ikraam (Ee Rabb! Wewe Ndiwe Amani, na Amani yatokana Nawe, Umetukuka Ee Mwenye Enzi na Mwenye Kustahiki Kuheshimika)." Awzaa'iyy mmoja wa wapokezi aliulizwa: "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akileta Istighfaar vipi?" Akajibu: "Alikuwa anasema: Astaghfiru Allaah, Astaghfiru Allaah." [Muslim]

 

Hadiyth – 9

وعن عائشة رضي اللهُ عنها ، قالت : كان رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم يُكْثِرُ أَنْ يَقُولَ قَبْلَ مَوْتِهِ : (( سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ ، أسْتَغفِرُ اللهَ ، وأتوبُ إلَيْهِ )) متفق عليه .

Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikithirisha kusema kabla ya kuaga dunia: "Subhaana Allaahi wa Bihamdihi Astaghfiru Allaah wa Atuubu Ilayhi (Ametakasika Allaah na sifa zote Anastahiki Yeye, nakuomba maghfira na natubia Kwako)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 10

وعن أنس رضي الله عنه قال : سمعتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( قَالَ اللهُ تَعَالَى: يَا ابْنَ آدَمَ، إنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لكَ عَلَى مَا كَانَ مِنْكَ وَلاَ أُبَالِي ، يَا ابْنَ آدَمَ ، لَوْ بَلَغَتْ ذُنُوبُكَ عَنَانَ السَّمَاءِ ، ثُمَّ اسْتَغْفَرْتَنِي ، غَفَرْتُ لَكَ وَلاَ أُبَالِي ، يا ابْنَ آدَمَ ، إنَّكَ لَوْ أَتَيْتَنِي بِقُرَابِ الأَرْضِ خَطَايَا ، ثُمَّ لَقِيتَنِي لا تُشْرِكُ بِي شَيْئاً ، لأَتَيْتُكَ بِقُرابِهَا مَغْفِرَةً )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: Allaah Ta'aalaa Amesema: "Ee bin Aadam, hakika wewe kila unapoendelea kuniomba na kunitarajia, basi Nitakusamehe dhambi ulizonazo wala sijali. Ee bin Aadam, lau zafika dhambi zako mpaka mawinguni, kisha ukaniomba msamaha, Nitakughufuria. Ee bin Aadam, hakika wewe lau wanijia na makosa yenye kujaa ardhi kisha ukanikabili Mimi na hali hunishirikishi na kitu chochote, basi Nitakupa mfano wake maghfira." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 11

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قال : (( يا مَعْشَرَ النِّسَاءِ تَصَدَّقْنَ ، وأكْثِرْنَ مِنَ الاسْتِغْفَارِ ؛ فَإنِّي رَأَيْتُكُنَّ أَكْثَرَ أَهْلِ النَّارِ )) قالت امرأةٌ مِنْهُنَّ : مَا لَنَا أَكْثَرَ أَهْلِ النَّارِ ؟ قَالَ : (( تُكْثِرْنَ اللَّعْنَ ، وَتَكْفُرْنَ العَشِيرَ ، مَا رَأَيْتُ مِنْ نَاقِصَاتِ عَقْلٍ وَدِينٍ أغْلَبَ لِذِي لُبٍّ مِنْكُنَّ )) قالت : ما نُقْصَانُ العَقْلِ وَالدِّينِ ؟ قال : (( شَهَادَةُ امْرَأتَيْنِ بِشَهَادَةِ رَجُلٍ، وَتَمْكُثُ الأَيَّامَ لاَ تُصَلِّي )). رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Enyi kongamano la wanawake, toeni Swadaqah na muzidishe kuleta Istighfaar, kwani nimewaona wengi wa watu wa motoni ni nyinyi.: Akasema mwanamke mmoja miongoni mwao: "Tuna nini mpaka tukawa wengi miongoni mwa watu wa motoni?" Akasema: "Nyinyi munalaani sana na munawaasi waume zenu, sijaona walio na upungufu wa akili na Dini kuwaliko nyinyi." Yule mwanamke akauliza tena: "Nini maana ya upungufu wa akili na Dini?" Akamjibu: "Ushahidi wa wanawake wawili kwa mwanaume mmoja na munakaa kwa siku kadhaa pasi na kuswali." [Muslim]

 

 

 

 
 
Share