02-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kubainisha Yale Waliyoandaliwa Waumini na Allaah Peponi

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب بيان مَا أعدَّ اللهُ تَعَالَى للمؤمنين في الجنة

02-Mlango Wa Kubainisha Yale Waliyoandaliwa

Waumini na Allaah Jannah (Peponi)

 

 

 قَالَ الله تَعَالَى:

إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ﴿٤٥﴾ ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ آمِنِينَ﴿٤٦﴾ وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ إِخْوَانًا عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَابِلِينَ﴿٤٧﴾ لَا يَمَسُّهُمْ فِيهَا نَصَبٌ وَمَا هُم مِّنْهَا بِمُخْرَجِينَ﴿٤٨﴾

Hakika wenye taqwa watakuwa katika Jannaat na chemchemu. (Wataambiwa): Ingieni humo kwa salama mkiwa katika amani. Na Tutaondosha mafundo ya kinyongo yaliyomo vifuani mwao, wakiwa ndugu, juu ya makochi yaliyoinuliwa wakikabiliana. Hautowagusa humo uchovu nao humo hawatotolewa. [Al-Hijr: 45-48]

 

 

 يَا عِبَادِ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمُ الْيَوْمَ وَلَا أَنتُمْ تَحْزَنُونَ﴿٦٨﴾ الَّذِينَ آمَنُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا مُسْلِمِينَ﴿٦٩﴾ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ أَنتُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ تُحْبَرُونَ﴿٧٠﴾ يُطَافُ عَلَيْهِم بِصِحَافٍ مِّن ذَهَبٍ وَأَكْوَابٍ ۖ وَفِيهَا مَا تَشْتَهِيهِ الْأَنفُسُ وَتَلَذُّ الْأَعْيُنُ ۖ وَأَنتُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿٧١﴾ وَتِلْكَ الْجَنَّةُ الَّتِي أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٧٢﴾ لَكُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ كَثِيرَةٌ مِّنْهَا تَأْكُلُونَ﴿٧٣﴾

Enyi waja Wangu! Hakuna khofu juu yenu leo, na wala nyinyi hamtohuzunika. Ambao wameamini Aayaat Zetu na wakawa Waislamu. Ingieni Jannah nyinyi na wake zenu mfurahishwe. Watapitishiwa sahani za dhahabu na bilauri, na humo mna yale yanayotamani nafsi na ya kuburidisha macho, nanyi humo ni wenye kudumu. Na hiyo ni Jannah ambayo mmerithishwa kwa yale mliyokuwa mkitenda. Mtapata humo matunda mengi mtakayokuwa mnakula. [Az-Zukhruf: 68-73]

 

إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينٍ﴿٥١﴾ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ﴿٥٢﴾ يَلْبَسُونَ مِن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَقَابِلِينَ﴿٥٣﴾ كَذَٰلِكَ وَزَوَّجْنَاهُم بِحُورٍ عِينٍ﴿٥٤﴾ يَدْعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَاكِهَةٍ آمِنِينَ﴿٥٥﴾لَايَذُوقُونَ فِيهَا الْمَوْتَ إِلَّا الْمَوْتَةَ الْأُولَىٰ ۖ وَوَقَاهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ﴿٥٦﴾ فَضْلًا مِّن رَّبِّكَ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٥٧﴾

Hakika wenye taqwa wako katika mahali pa amani. Katika Jannaat na chemchemu. Watavaa hariri laini na hariri nzito nyororo wakiwa wamekabiliana. Hivyo ndivyo!  Na Tutawaozesha Mahuri (wanawake wa Jannah) wenye macho ya kupendeza. Wataagiza humo kila aina ya matunda wakiwa katika amani. Hawatoonja humo mauti isipokuwa mauti yale ya awali na (Allaah) Atawakinga na adhabu ya moto uwakao vikali mno. Ni fadhila kutoka kwa Rabb wako.  Huko ndiko kufuzu adhimu. [Ad-Dukhaan: 51-57]

 

 إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ ﴿٢٢﴾ عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ ﴿٢٣﴾تَعْرِفُ فِي وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ النَّعِيمِ ﴿٢٤﴾يُسْقَوْنَ مِن رَّحِيقٍ مَّخْتُومٍ ﴿٢٥﴾خِتَامُهُ مِسْكٌۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ ﴿٢٦﴾وَمِزَاجُهُ مِن تَسْنِيمٍ ﴿٢٧﴾عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا الْمُقَرَّبُونَ ﴿٢٨﴾

Hakika Waumini watendao wema kwa wingi  bila shaka watakuwa kwenye neema (taanasa, furaha n.k). Kwenye makochi ya fakhari wakitazama. Utatambua nyuso zao kwa nuru ya neema (taanasa, furaha). Watanyweshwa kinywaji safi na bora kabisa cha mvinyo kilichozibwa. Mwisho wake ni miski. Na katika hayo basi washindane wenye kushindana. Na mchanganyiko wake ni kutokana na Tasniym. Ni chemchemu watakayokunywa humo watakaokurubishwa (kwa Allaah).[Al-Mutwaffifiyn:22 - 28]

 

 

Hadiyth – 1

وعن جابر رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: (( يَأكُلُ أَهْلُ الجَنَّةِ فِيهَا ، وَيَشْرَبُونَ ، وَلاَ يَتَغَوَّطُونَ ، وَلاَ يَمْتَخِطُونَ ، وَلاَ يَبُولُونَ ، وَلكِنْ طَعَامُهُمْ ذَلِكَ جُشَاءٌ كَرَشْحِ المِسْكِ ، يُلْهَمُونَ التَّسْبِيحَ وَالتَّكْبِيرَ ، كَمَا يُلْهَمُونَ النَّفَسَ )) . رواه مسلم 

Na imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:  “Watu wa Jannah watakula humo, watakunywa, wala hawataenda haja kubwa, wala hawatatokwa kamasi, wala hawatakojoa, lakini chakula chao kitatoka kwa kuteuka na ikitoa harufu kama ya miski.  Watapewa ilhamu ya kumsabihi Allaah kama vile wanavyopewa ilhamu ya kupumua (bila ya shida)” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: (( قَالَ اللهُ تَعَالَى : أعْدَدْتُ لِعِبَادِي الصَّالِحِينَ مَا لاَ عَيْنٌ رَأَتْ ، وَلاَ أُذُنٌ سَمِعَتْ ، وَلاَ خَطَرَ عَلَى قَلْبِ بَشَرٍ ، وَاقْرَؤُوا إنْ شِئْتُمْ [ فَلاَ تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنِ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ] [ السجدة : 17 ] )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ . 

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amesema: "Waja Wangu wema Nimewaandalia ambayo hayajapata kuonekanwa na jicho lolote, wala hayajapatapo kusikiwa na sikio lolote wala hayajawahi kufikiriwa na moyo wowote wa  mwana Aadam. Na mkitaka someni Aayah hii: 

فَلاَ تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنِ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ 

Basi nafsi yoyote haijui yaliyofichiwa katika yanayoburudisha macho. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [As-Sajdah:17] [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( أَوَّلُ زُمْرَةٍ يَدْخُلُونَ الجَنَّةَ عَلَى صُورَةِ القَمَرِ لَيْلَةَ البَدْرِ ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ عَلَى أشَدِّ كَوْكَبٍ دُرِّيٍّ فِي السَّمَاءِ إضَاءةً ، لاَ يَبُولُونَ ، وَلاَ يَتَغَوَّطُونَ ، وَلاَ يَتْفُلُونَ ، وَلاَ يَمْتَخِطُونَ . أمْشَاطُهُمُ الذَّهَبُ ، وَرَشْحُهُمُ المِسْكُ ، وَمَجَامِرُهُمُ الأُلُوَّةُ – عُودُ الطِّيبِ – أزْوَاجُهُمُ الحُورُ العيْنُ ، عَلَى خَلْقِ رَجُلٍ وَاحِدٍ ، عَلَى صُورَةِ أَبِيهِمْ آدَمَ سِتُّونَ ذِرَاعاً فِي السَّمَاءِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية البخاري ومسلم : ((آنِيَتُهُمْ فِيهَا الذَّهَبُ ، وَرَشْحُهُمُ المِسْكُ . وَلِكُلِّ وَاحِدٍ مِنْهُمْ زَوْجَتَانِ يُرَى مُخُّ سَاقِهِمَا مِنْ وَرَاءِ اللَّحْمِ مِنَ الحُسْنِ ، لاَ اخْتِلاَفَ بَيْنَهُمْ، وَلاَ تَبَاغُضَ، قُلُوبُهُمْ قَلْبُ وَاحِدٍ ، يُسَبِّحُونَ اللهَ بُكْرَةً وَعَشِياً )) 

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kundi la kwanza watakaoingia Jannah ni watu wenye surah za mwezi wa Arbatashara (Uliokamilika), kisha watakaowafuatia watakuwa wanag’aa kuliko nyota yoyote inayong’arisha yenye mwanga mkali mbinguni, hawakojoi, hawaendi haja kubwa, hawatemi mate, wala hawatoi kamasi.  Vitana vyao ni vya dhahabu, jasho lao ni harufu ya miski, katika vitezo vyao watafukiza aliudi, wake zao ni Huwrul-‘ayn (Wanawake wa Jannah wenye macho ya kupendeza).  Watakuwa (sawa) katika umbile la mtu mmoja, katika sura ya baba yao Aadam, dhiraa sitini kuelekea juu.[Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah nyingine ya Al-Bukhaariy na Muslim imesema: “Vyombo vyao huko Jannah ni vya dhahabu, harufu ya jasho lao ni miski.  Kila mmoja wao atakuwa ana wake wawili ambao uboho wa mifupa ya miundi yao itaonekana nje ya nyama kutokana na uzuri! Hakuna magombano kati yao wala chuki, nyoyo zao ni kama moyo wa mtu mmoja, watakuwa wakimsabihi Allaah asubuhi na jioni”.

 

 

Hadiyth – 4

وعن المغيرةِ بن شعبة رضي الله عنه ، عن رسُولِ الله صلى الله عليه وسلم ، قال : (( سألَ مُوسَى  رَبَّهُ : ما أدْنَى أهْلِ الجَنَّةِ مَنْزِلَةً ؟ قال : هُوَ رَجُلٌ يَجِيءُ بَعْدَ مَا أُدْخِلَ أهْلُ الجَنَّةِ الجَنَّةَ ، فَيُقَالُ لَهُ : ادْخُلِ الجَنَّةَ . فَيَقُولُ : أيْ رَبِّ ، كَيْفَ وَقَدْ نَزَلَ النَّاسُ مَنَازِلَهُمْ ، وأخَذُوا أَخَذَاتِهِمْ ؟ فَيُقَالُ لَهُ : أَتَرْضَى أَنْ يَكُونَ لَكَ مِثْلُ  مُلْكِ مَلِكٍ مِنْ مُلُوكِ الدُّنْيَا ؟ فَيقُولُ : رَضِيْتُ رَبِّ ، فَيقُولُ : لَكَ ذَلِكَ وَمِثْلُهُ وَمِثْلُهُ وَمِثْلُهُ وَمِثْلُهُ، فَيقُولُ في الخامِسَةِ . رَضِيْتُ رَبِّ، فَيقُولُ : هذَا لَكَ وَعَشَرَةُ أَمْثَالِهِ، وَلَكَ مَا اشْتَهَتْ نَفْسُكَ ، وَلَذَّتْ عَيْنُكَ . فَيقُولُ : رَضِيتُ رَبِّ . قَالَ : رَبِّ فَأَعْلاَهُمْ مَنْزِلَةً ؟ قالَ : أُولَئِكَ الَّذِينَ أَرَدْتُ ؛ غَرَسْتُ كَرَامَتَهُمْ بِيَدِي ، وَخَتَمْتُ عَلَيْهَا، فَلَمْ تَرَ عَيْنٌ، وَلَمْ تَسْمَعْ أُذُنٌ، وَلَمْ يَخْطُرْ عَلَى قَلْبِ بَشَرٍ )) . رواه مسلم

Al-Mughiyrah bin Shu’bah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Muwsaa  (‘alayhis-salaam) alimwuliza Rabb wake: “Ni mtu yupi wa Jannah atakayekuwa ana daraja ya chini zaidi?” Allaah Akamjibu: “Ni mtu ambaye atakuja baada ya kuwa watu wa Jannah wameshaingia Jannah, Ataambiwa: “Kaingie. (Jannah).” Atasema ee Rabb! Nitaingiaje ilihali watu wote wameshateremkia katika makazi yao na wameshachukua neema zao?” Ataulizwa: “Je, unaridhika upate mfano wa Ufalme wa mfalme wa duniani?” Atajibu: “Nimeridhika, Rabb wangu!” Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atamwambia: “Nimeshakupa milki hiyo na mfano wake, na mfano wake, na mfano wake na mfano wake.” Katika mara ya tano yule mtu atasema: “Nimeridhika, Rabb wangu!” Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atamwambia hayo yote ni yako na mfano wake mara kumi. Nawe utapata kila kilichotamaniwa na nafsi yako na kikaonewa ladha na jicho lako.” Atasema: “Nimeridhika, Rabb wangu!” Muwsaa (‘alayhis-salaam) akauliza: “Ee Rabb, je mwenye daraja kubwa zaidi?” Allaah Akamjibu hao ni ambao Niliwachagua Nikaotesha neema zao kwa Mkono Wangu na Nikazifunika juu yake, (neema hizo) hazijaonekanapo na jicho lolote, hazijasikiwapo na sikio lolote wala haijampitikia mwana Aadam yeyote kuzifikiria.” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 5

 وعن ابن مسعود رضي الله عنه قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( إنِّي لأَعْلَمُ آخِرَ أَهْلِ النَّارِ خُرُوجاً مِنْهَا ، وَآخِرَ أَهْلِ الجَنَّةِ دُخُولاً الجَنَّةَ . رَجُلٌ يَخْرُجُ مِنَ النَّارِ حَبْواً ، فَيقُولُ اللهُ (عزّ وجلّ) له : اذْهَبْ فادْخُلِ الجَنَّةَ ، فَيَأتِيهَا ، فَيُخَيَّلُ إلَيْهِ أَنَّهَا مَلأَى ، فَيَرْجِعُ، فَيقُولُ : يَا رَبِّ وَجَدْتُهَا مَلأَى ‍! فَيَقُولُ اللهُ (عزّ وجلّ) له: اذْهَبْ فَادْخُلِ الجَنَّةَ ، فيأتِيهَا ، فَيُخيَّلُ إليهِ أنَّها مَلأى ، فيَرْجِعُ . فَيَقولُ : يا رَبِّ وَجَدْتُهَا مَلأى ، فيقُولُ اللهُ (عزّ وجلّ) لَهُ : اذهبْ فَادخُلِ الجنَّةَ . فَإنَّ لَكَ مِثْلَ الدُّنْيَا وَعَشرَةَ أَمْثَالِهَا ؛ أوْ إنَّ لَكَ مِثْلَ عَشرَةِ أَمْثَالِ الدُّنْيَا ، فَيقُولُ : أتَسْخَرُ بِي ، أَوْ تَضْحَكُ بِي وَأنْتَ المَلِكُ )) قال : فَلَقَدْ رَأَيْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ضَحِكَ حَتَّى بَدَتْ نَوَاجِذُهُ فَكَانَ يقولُ : (( ذلِكَ أَدْنَى أهْلِ الجَنَّةِ مَنْزِلَةً )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ 

 ‘Abdullaah bin Mas’ud (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema : “Hakika, mimi namjua mtu wa mwisho wa motoni atakayetoka motoni na mtu wa mwisho wa Jannah atakayeingia Jannah. Mtu wa mwisho atatoka motoni kwa kutosa. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atamwambia “Nenda ukainigie Jannah.”  Ataenda atadhani kuwa Jannah imejaa, atarejea. Atasema: “Ee Rabbi, nimekuta kumeshajaa!” Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atamwambia: “Nenda ukaingie Jannah” Ataenda, atadhani kuwa Jannah imejaa, atarejea. Atasema “Ee Rabbi, nimekuta kumeshajaa!” Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atamwambia: “Nenda ukaingie Jannah hakika nimekupa mithili ya dunia na mfano wake mara kumi.” Yule mtu atasema “Wanifanyia maskhara Nawe ni Mfalme?” ‘Abdullaah bin Mas’uwd akasema: “Hakika nilimuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akicheka mpaka meno yake yakaonekana!” Akawa anasema “Huyo ndiye mwenye daraja ya chini zaidi Jannah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 6

وعن أبي موسى رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم  قال : (( إنَّ لِلمُؤْمِنِ فِي الجَنَّةِ لَخَيْمَةً مِنْ لُؤْلُؤَةٍ وَاحِدَةٍ مُجَوَّفَةٍ طُولُها في السَّمَاءِ سِتُّونَ مِيلاً . لِلمُؤْمِنِ فِيهَا أَهْلُونَ يَطُوفُ عَلَيْهِمُ المُؤْمِنُ فَلاَ يَرَى بَعْضُهُمْ بَعْضاً )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Abuu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema : “Hakika, Muumini Jannah atakuwa ana hema la lulu ambalo liko mviringo, urefu wake ni maili sitiini kwenda juu. Muumini atakuwa na familia yake humo. Muumini atakuwa akiwazunguka humo nao hawaonani (Jinsi lilivyo kubwa).”  [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 7

وعن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قال : (( إنَّ في الجَنَّةِ شَجَرَةً يَسِيرُ الرَّاكبُ الجَوَادَ المُضَمَّرَالسَّريعَ مِئَةَ سَنَةٍ مَا يَقْطَعُها )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

وروياه في الصحيحين أيضاً من رواية أبي هريرة رضي الله عنه قال: (( يَسيرُ الرَّاكِبُ في ظِلِّها مئةَ سَنَةٍ مَا يَقْطَعُها ))

Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika Jannah kuna mti ambao mpanda farasi mwenye kasi kubwa atatembea chini ya kivuli chake miaka mia (100) wala hamalizi.”[Al-Bukhaariy na Muslim] 

Riwaayah nyingine ya Al-Bukhaariy na Muslim imesema:  “…mpanda farasi atatembea chini ya kivuli chake miaka mia (100) wala hakimalizi.”

 

 

 

Hadiyth – 8

وعن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم قال : (( إنَّ أهْلَ الجَنَّةِ لَيَتَرَاءوْنَ أَهْلَ الغُرَفِ مِن فَوْقِهِمْ كَمَا تَرَاءوْنَ الكَوْكَبَ الدُّرِّيَّ .الغَابِرَ فِي الأُفُق مِنَ المَشْرِقِ أو المَغْرِبِ لِتَفَاضُلِ مَا بَيْنَهُمْ )) قالُوا : يا رسول الله ؛ تِلْكَ مَنَازِلُ الأنبياء لاَ يَبْلُغُها غَيْرُهُمْ قال : (( بَلَى والَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ ، رِجَالٌ آمَنُوا بِاللهِ وَصَدَّقُوا المُرْسَلِينَ ))  مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy  (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika watu wa Jannah watawaona wenye maghorofa kwa juu yao kama vile nyinyi mnavyoziona nyota zinga’razo zinazotembea mbinguni Mashariki au Magharibi, (hili ni) kwa kuzidiana kwao.” Maswahaba wakauliza ee Rasuli wa Allaah! Hayo ni majumba ya Manabii ambayo hakuna mwengine  Atakayeyafikia?” Akawaambia: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake, hao ni watu waliomwamini Allaah na wakawasadikisha Rusuli”.  [Al-Bukhaariy na Muslim] 

 

         

 

Hadiyth – 9

وعن أبي هريرة: رضي الله عنه أنَّ رسولَ اللهِ  صلى الله عليه وسلم قال : (( لَقَابُ قَوْسٍ في الجَنَّةِ خَيْرٌ مِمَّا تَطْلُعُ عَلَيْهِ الشَّمْسُ أو تَغْرُبُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ 

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika baina ya upinde na upinde Jannah ni bora kuliko vyote vilivyochomozewa na jua au kuchwelewa.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

  

 

Hadiyth – 10

وعن أنس رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قال : (( إنَّ في الجَنَّةِ سُوقاً يَأتُونَهَا كُلَّ جُمُعَةٍ . فَتَهُبُّ رِيحُ الشَّمَالِ ، فَتَحْثُو في وُجُوهِهِم وَثِيَابِهِمْ ، فَيَزدَادُونَ حُسناً وَجَمَالاً فَيَرْجِعُونَ إلَى أَهْلِيهِمْ ، وَقَد ازْدَادُوا حُسْناً وَجَمَالاً ، فَيقُولُ لَهُمْ أَهْلُوهُمْ : وَاللهِ لقدِ ازْدَدْتُمْ حُسْناً وَجَمَالاً ! فَيقُولُونَ : وَأنْتُمْ وَاللهِ لَقَدِ ازْدَدْتُمْ بَعْدَنَا حُسْناً وَجَمالاً ! )) . رواه مسلم

Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika Jannah kutakuwa kuna mjumuiko watu wakienda kila Ijumaa (wiki). Upepo wa kaskazi utavuma, utatawanyika katika nyuso na nguoni mwao, kwa ajili hiyo watazidi uzuri na urembo, watarejea kwa familia zao zitawaambia: “Wa-Allaahi mumezidi kuwa wazuri na warembo!” Wao watawaambia: ”Nanyi pia, wa-Allaahi  mumezidi baada ya sisi kuondoka uzuri na urembo!” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 11

وعن سهل بن سعد رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قال : (( إنَّ أهْلَ الجَنَّةِ لَيَتَراءونَ الغُرَفَ فِي الجَنَّةِ كَمَا تَتَرَاءونَ الكَوكَبَ فِي السَّمَاءِ )) متفق عليه 

Sahl bin Sa’d (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika watu wa Jannah watawaona wenye maghorofa huko Jannah kama vile nyinyi mnavyoziona nyota mbinguni.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 12

وعن سهل بن سعد رضي الله عنه ، قال : شَهِدْتُ مِنَ النبيّ صلى الله عليه وسلم مَجْلِساً وَصَفَ فِيهِ الجَنَّةَ حَتَّى انْتَهَى ، ثُمَّ قَالَ في آخِرِ حَدِيثِهِ : (( فيهَا مَا لاَ عَينٌ رَأَتْ ، وَلاَ أُذُنٌ سَمِعَتْ ، وَلاَ خَطَرَ عَلى قَلْبِ بَشَرٍ )) ثُمَّ قَرَأَ : تَتَجَافَى جُنُوبُهُمْ عَنِ المَضَاجِعِ ] إلى قوله تعالى : [ فَلاَ تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ ] [ السجدة: 16 - 17 ] . رواه البخاري

Sahl bin Sa’d (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesimulia: “Siku moja nilishuhudia kikao fulani cha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambapo ndani yake aliisifu Jannah mpaka akamaliza. Mwisho wa mazungumzo yake alisema: “Ndani yake mna ambayo hayajaonekanapo na jicho lolote, wala hayajasikiwa na sikio lolote wala hayajawahi kufikiriwa na moyo wowote wa mwana Aadam.” Kisha akasoma:

تَتَجَافَىٰ جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿١٦﴾

Mbavu zao zinatengana na vitanda, wanamuomba Rabb wao kwa khofu na matumaini, na katika yale Tuliyowaruzuku wanatoa.

فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَّا أُخْفِيَ لَهُم مِّن قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٧﴾

Basi nafsi yoyote haijui yaliyofichiwa katika yanayoburudisha macho. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [As-Sajdah 17 – 18] [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 13 

وعن أبي سعيد وأبي هريرة رضي الله عنهما : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال : (( إذَا دَخَلَ أهْلُ الجَنَّةِ الجَنَّةَ يُنَادِي مُنَادٍ : إنَّ لَكُمْ أنْ تَحْيَوْا ، فَلاَ تَمُوتُوا أَبَداً ، وإنَّ لَكُمْ أنْ تَصِحُّوا ، فلا تَسْقَمُوا أبداً ، وإنَّ لَكمْ أنْ تَشِبُّوا فلا تَهْرَمُوا أبداً ، وإنَّ لَكُمْ أَنْ تَنْعَمُوا ، فَلاَ تَبْأسُوا أَبَداً )) .   رواه مسلم .

Abu Sa’iyd na Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) wamesimulia: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Watu wa Jannah watakapoingia Jannah, atanadi mwenye kunadi: “Hakika nyinyi mtaishi milele wala hamtakuwa wagonjwa, nanyi mtakuwa barobaro milele wala hamtazeeka, nanyi mtaneemeka milele wala hamtapata shida.” [Muslim] 

 

 

Hadiyth – 14

وعن أبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال : (( إنَّ أدْنَى مَقْعَدِ أَحَدِكُمْ مِن الجَنَّةِ أنْ يَقُولَ لَهُ : تَمَنَّ ، فَيَتَمَنَّى وَيَتَمَنَّى فَيقُولُ لَهُ : هَلْ تَمَنَّيتَ ؟ فيقولُ : نَعَمْ ، فيقُولُ لَهُ : فَإنَّ لَكَ ما تَمَنَّيتَ وَمِثْلَهُ  مَعَهُ )) . رواه مسلم

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika daraja ya chini mno ya mmoja wenu Jannah, ni kuwa Allaah Atamwambia: “Tamani.” Atatamani kila atakalo. Allaah Atamuuliza: “Umeshamaliza kutamani?” Atajibu: “Ndio.” Allaah Atamwambia: “Nimekupa ulichotamani na Nimekupa kama hicho.” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 15

وعن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه: أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قال : (( إنَّ الله  (عزّ وجلّ) يَقُولُ لأَهْلِ الجَنَّةِ : يَا أهْلَ الجَنَّةِ ، فَيقولُونَ : لَبَّيكَ رَبَّنَا وَسَعْدَيْكَ ، وَالخَيْرُ في يَديْكَ ، فَيقُولُ : هَلْ رَضِيتُم ؟ فَيقُولُونَ : وَمَا لَنَا لاَ نَرْضَى يَا رَبَّنَا وَقَدْ أَعْطَيْتَنَا مَا لَمْ تُعْطِ أحداً مِنْ خَلْقِكَ ، فَيقُولُ : ألاَ أُعْطِيكُمْ أفْضَلَ مِنْ ذلِكَ ؟ فَيقُولُونَ : وَأيُّ شَيءٍ أفْضَلُ مِنْ ذلِكَ ؟ فَيقُولُ : أُحِلُّ عَلَيكُمْ رِضْوَانِي فَلاَ أسْخَطُ عَلَيْكُمْ بَعْدَهُ أبَداً )) . متفق عليه 

Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika Allaah ('Azza wa Jalla) atawaambia watu wa Jannah: “Enyi watu wa Jannah.” Wataitikia: “Labbayka Rabb wetu, Utukufu ni Wako na Kheri imo Mkononi Mwako.” Atawauliza: “Mmeridhika?” Watajibu: “Kwa nini tusiridhike ee Rabb wetu ilhali Umetupa ambayo Hukumpa yeyote katika viumbe Vyako!” Allaah atawauliza: “Je, niwape kilicho bora kuliko hicho Nilichowapa?” Watasema “Ni kitu gani kilicho bora kuliko hicho?” Allaah atawaambia: “Nimewateremshia Radhi Yangu Sitawakasirikia milele baada ya leo.” [Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 16

وعن جرير بن عبد الله رضي الله عنه، قال: كُنَّا عِندَ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم فَنَظَرَ إلَى القَمَرِ لَيْلَةَ البَدْرِ، وَقَالَ : (( إنَّكُمْ سَتَرَوْنَ رَبَّكُمْ عَيَاناً كما تَرَوْنَ هَذَا القَمَرَ ، لاَ تُضَامُونَ فِي رُؤْيَتِهِ )) متفق عليه

Jariyr bin Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesimulia: “Tulikuwa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akautizama mwezi usiku wa arbatashara, akatuambia: “Hakika mtamuona Rabb wenu waziwazi kama mnavyouwona mwezi huu, hamtapata shida katika kumuona.” [Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 17

وعن صُهيب رضي الله عنه: أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قال : (( إذا دَخَلَ أهْلُ الجَنَّةِ الجَنَّةَ يَقُولُ اللهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى : تُريدُونَ شَيئاً أَزيدُكُمْ ؟ فَيقُولُونَ : ألَمْ تُبَيِّضْ وُجُوهَنَا ؟ ألَمْ تُدْخِلْنَا الجَنَّةَ وَتُنَجِّنَا مِنَ النَّارِ ؟ فَيَكْشِفُ الحِجَابَ ، فَمَا أُعْطُوا شَيْئاً أَحَبَّ إلَيْهِمْ مِنَ النَّظَرِ إلَى رَبِّهِمْ )).رواه مسلم .

Swuhaib (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Watu wa Jannah watakapokuwa wameshaingia Jannah, Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Atawauliza: “Mnataka Niwazidishie chochote?” Watasema: “Si Umezing’arisha nyuso zetu? Si Umetuingiza Jannah na Umetuepusha na moto?” (Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa) Ataondoa pazia.  Basi watakuwa hakuna walichopewa kinachowapendeza mno kuliko kumtazama Rabb wao!” [Muslim] 

 

قال الله تعالى : [ إنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ يَهْدِيهِمْ رَبُّهُمْ بِإِيمَانِهِمْ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهِمُ الأَنْهَارُ في جَنَّاتِ النَّعِيمِ دَعْوَاهُمْ فيها سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وَتَحِيَّتُهُمْ فِيهَا سَلاَمٌ وَآخِرُ دَعْوَاهُمْ أَنِ الحَمْدُ للهِ رَبِّ العَالَمِينَ ] [ يونس : 9 - 10 ] 

Hakika wale walioamini na wakatenda mema, Rabb wao Atawaongoza kwa iymaan zao. Zitapita chini yao mito katika Jannaat za neema. Wito wao humo ni: Utakasifu ni Wako ee Allaah. Na maamkizi yao humo ni Salaamun! Na wito wao wa mwisho ni AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Rabb wa walimwengu. [Yuwnus: 9-10]

 

 

الحَمْدُ للهِ الَّذِي هَدَانَا لِهَذَا وَمَا كُنَّا لِنَهْتَدِي لَوْلاَ أَنْ هَدَانَا اللهُ . اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ عَبْدِكَ وَرَسُولِكَ النَّبيِّ الأُمِّيِّ ، وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ وَأزوَاجِهِ وَذُرِّيَّتِهِ ، كما صَلَّيْتَ عَلَى إبْرَاهِيمَ وعلى آلِ إبْراهِيمَ ، وَبَارِكْ عَلَى مُحَمَّدٍ النَّبيِّ الأُمِّيِّ ، وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ وَأزْوَاجِهِ وَذُرِّيَّتِهِ ، كما بَاركْتَ عَلَى إبْرَاهِيمَ وَعَلَى آل إبراهيم في العالَمِينَ إنَّكَ حَمِيدٌ مَجِيدٌ .

Sifa zote njema Anastahiki Allaah ambaye kwamba Ametuongoza katika hili na hatungekuwa ni wenye kuongoka lau si kuongozwa na Allaah. Ee Rabb wangu Mrehemu Muhammad na jamaa za Muhammad kama ulivyo Mrehemu Ibraahiym na jamaa za Ibraahiym. Na Mbariki Muhammad na jamaa za Muhammad kama ulivyo Mbariki Ibraahiym na jamaa za Ibraahiym, hakika Wewe ni Mwingi wa Kusifiwa na Uliyo Mtukufu.

 

 

Share