07-Swahiyh Al-Bukhaariy: Kitabu Cha Tayammum - كتاب التيمم
كِتابُ التَّيمّم
07-Kitabu Cha Tayammum
(Kutia Wudhuu Kwa Kuukusudia Mchanga Juu Ya Ardhi Safi)
Tayammum: Kuukusudia Mchanga Wa Juu Ya Ardhi Kwa Ajili Ya Wudhuu Pindi Yanapokosekana Maji.
قَوْلِ اللَّهِ تَعَالَ: فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ
Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ ۚ
Kisha hamkupata maji; basi tayammamuni (ikusudieni) ardhi kwa juu panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu. [Al-Maaidah: 6]
01-Mlango
|
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، قَالَ أَخْبَرَنَا مَالِكٌ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ الْقَاسِمِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ، زَوْجِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَتْ خَرَجْنَا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي بَعْضِ أَسْفَارِهِ، حَتَّى إِذَا كُنَّا بِالْبَيْدَاءِ ـ أَوْ بِذَاتِ الْجَيْشِ ـ انْقَطَعَ عِقْدٌ لِي، فَأَقَامَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَلَى الْتِمَاسِهِ، وَأَقَامَ النَّاسُ مَعَهُ، وَلَيْسُوا عَلَى مَاءٍ، فَأَتَى النَّاسُ إِلَى أَبِي بَكْرٍ الصِّدِّيقِ فَقَالُوا أَلاَ تَرَى مَا صَنَعَتْ عَائِشَةُ أَقَامَتْ بِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَالنَّاسِ، وَلَيْسُوا عَلَى مَاءٍ، وَلَيْسَ مَعَهُمْ مَاءٌ. فَجَاءَ أَبُو بَكْرٍ وَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَاضِعٌ رَأْسَهُ عَلَى فَخِذِي قَدْ نَامَ فَقَالَ حَبَسْتِ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَالنَّاسَ، وَلَيْسُوا عَلَى مَاءٍ، وَلَيْسَ مَعَهُمْ مَاءٌ. فَقَالَتْ عَائِشَةُ فَعَاتَبَنِي أَبُو بَكْرٍ، وَقَالَ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَقُولَ، وَجَعَلَ يَطْعُنُنِي بِيَدِهِ فِي خَاصِرَتِي، فَلاَ يَمْنَعُنِي مِنَ التَّحَرُّكِ إِلاَّ مَكَانُ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَلَى فَخِذِي، فَقَامَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم حِينَ أَصْبَحَ عَلَى غَيْرِ مَاءٍ، فَأَنْزَلَ اللَّهُ آيَةَ التَّيَمُّمِ فَتَيَمَّمُوا. فَقَالَ أُسَيْدُ بْنُ الْحُضَيْرِ مَا هِيَ بِأَوَّلِ بَرَكَتِكُمْ يَا آلَ أَبِي بَكْرٍ. قَالَتْ فَبَعَثْنَا الْبَعِيرَ الَّذِي كُنْتُ عَلَيْهِ، فَأَصَبْنَا الْعِقْدَ تَحْتَهُ.
Amesimulia ‘Aaishah:
Mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Tulitoka na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika moja ya safari zake mpaka tulipofika Al-Baydaa au Dhaatul-Jaysh, kidani changu kilikatika (na kupotea). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alibakia pale akikitafuta na watu pia aliyefuatana nao (walikitafuta). Hapakuwa na maji mahali pale kwa hiyo watu walikwenda kwa Abu-Bakr Asw-Swiddiyq wakamwambia: “Umeona alichofanya ‘Aaisha? Amesababisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na watu kukaa sehemui siyokuwa na maji nao hawakuchukua maji.” Abu Bakr alifika wakati Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa amelala na kichwa chake alikiegemeza juu ya paja langu. Aliniambia: “Umemzuia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na watu mahali pasipokuwa na maji na hawakuchukua na maji.” Kwa hiyo akinishutumu na akasema aliyojaaliwa kusema na Allaah na alinipiga ubavu kwa mkono wake. Hapana kilichonizuia kusogea (kwa maumivu) isipokuwa kujilaza kwake Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) (kwenye paja langu). Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaamka kulipopambazuka na hapakuwa na maji. Basi Allaah Akateremsha Aayah ya Tayammum. Kwa hiyo wote walitayammam. Usayd bin Al-Khudhwayr alisema: “Ee Ahli wa Abu Bakr! Hii sio barakah ya kwanza kwenu.” Kisha ngamia niliyempanda alisogea na kile kidani kikaonekana chini yake.
Mjalada: 1
|
Kitabu: 7
|
Hadiyth: 330
|
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سِنَانٍ، قَالَ حَدَّثَنَا هُشَيْمٌ، ح قَالَ وَحَدَّثَنِي سَعِيدُ بْنُ النَّضْرِ، قَالَ أَخْبَرَنَا هُشَيْمٌ، قَالَ أَخْبَرَنَا سَيَّارٌ، قَالَ حَدَّثَنَا يَزِيدُ ـ هُوَ ابْنُ صُهَيْبٍ الْفَقِيرُ ـ قَالَ أَخْبَرَنَا جَابِرُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " أُعْطِيتُ خَمْسًا لَمْ يُعْطَهُنَّ أَحَدٌ قَبْلِي نُصِرْتُ بِالرُّعْبِ مَسِيرَةَ شَهْرٍ، وَجُعِلَتْ لِيَ الأَرْضُ مَسْجِدًا وَطَهُورًا، فَأَيُّمَا رَجُلٍ مِنْ أُمَّتِي أَدْرَكَتْهُ الصَّلاَةُ فَلْيُصَلِّ، وَأُحِلَّتْ لِيَ الْمَغَانِمُ وَلَمْ تَحِلَّ لأَحَدٍ قَبْلِي، وَأُعْطِيتُ الشَّفَاعَةَ، وَكَانَ النَّبِيُّ يُبْعَثُ إِلَى قَوْمِهِ خَاصَّةً، وَبُعِثْتُ إِلَى النَّاسِ عَامَّةً ".
Amesimulia Jaabir Bin ‘Abdillaah:
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nimepewa mambo matano ambayo hakupewa mwingine kabla yangu:-
i-Allaah Alinifanya mshindi kwa kuwahofisha maadui zangu, umbali wa mwendo wa safari ya mwezi mmoja.
ii-Ardhi imejaaliwa kwangu (na Ummah wangu) kuwa mahali pa kuswalia na kitu cha kufanyia Tayammum, kwa hiyo yeyote kati ya Umma wangu anaweza kuswali popote anapofikiwa na wakati wa Swalaah.
iii-Nimehalalishiwa ngawira ambapo haikuwa halaal kwa yeyote kabla yangu.
iv- Nimepewa haki Ash-Shafaa’ah (maombezi Siku Ya Qiyaamah).
v-Kila Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitumwa kwa watu wake tu lakini mimi nimetumwa kwa watu wote.”
Mjalada: 1
|
Kitabu: 7
|
Hadiyth: 331
|
02-Mlango
باب إِذَا لَمْ يَجِدْ مَاءً وَلاَ تُرَابًا Pindi Yasipopatikana Maji Wala Ardhi (Kwa Ajili Ya Mchanga)
|
حَدَّثَنَا زَكَرِيَّاءُ بْنُ يَحْيَى، قَالَ حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ نُمَيْرٍ، قَالَ حَدَّثَنَا هِشَامُ بْنُ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّهَا اسْتَعَارَتْ مِنْ أَسْمَاءَ قِلاَدَةً فَهَلَكَتْ، فَبَعَثَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم رَجُلاً، فَوَجَدَهَا فَأَدْرَكَتْهُمُ الصَّلاَةُ وَلَيْسَ مَعَهُمْ مَاءٌ فَصَلَّوْا، فَشَكَوْا ذَلِكَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَأَنْزَلَ اللَّهُ آيَةَ التَّيَمُّمِ. فَقَالَ أُسَيْدُ بْنُ حُضَيْرٍ لِعَائِشَةَ جَزَاكِ اللَّهُ خَيْرًا، فَوَاللَّهِ مَا نَزَلَ بِكِ أَمْرٌ تَكْرَهِينَهُ إِلاَّ جَعَلَ اللَّهُ ذَلِكِ لَكِ وَلِلْمُسْلِمِينَ فِيهِ خَيْرًا.
Amesimulia Baba yake ‘Urwah:
‘Aaisha amesema: “Niliazima mkufu kutoka kwa Asmaa na ulipotea. Kwa hiyo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimtuma mtu autafute na aliupata. Kisha wakati wa Swalaah ukawadia na hapakuwa na maji. Walisawli bila kutawadha na kisha wakamlalamikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha Aayah ya Tayammum.” ‘Usayd bin Hudhwayr akamwambia ‘Aaishah: “JazaakiLLaahu khayraa (Allaah Akujazi kheri) kwani wa-Allaahi linapotokea jambo usilolipenda, Allaah Hujaalia jambo hilo kwa Waislamu kuwa lina khayr ndani yake.”
Mjalada: 1
|
Kitabu: 7
|
Hadiyth: 332
|
03-Mlango
باب التَّيَمُّمِ فِي الْحَضَرِ، إِذَا لَمْ يَجِدِ الْمَاءَ، وَخَافَ فَوْتَ الصَّلاَةِ Tayammum Kwa Asiye Msafiri Inaruhusiwa Kama Hapana Maji Au Anachelea Wakati Wa Swalaah Utapita
|
وَبِهِ قَالَ عَطَاءٌ.
وَقَالَ الْحَسَنُ فِي الْمَرِيضِ عِنْدَهُ الْمَاءُ وَلاَ يَجِدُ مَنْ يُنَاوِلُهُ يَتَيَمَّمُ.
وَأَقْبَلَ ابْنُ عُمَرَ مِنْ أَرْضِهِ بِالْجُرُفِ، فَحَضَرَتِ الْعَصْرُ بِمَرْبَدِ النَّعَمِ فَصَلَّى، ثُمَّ دَخَلَ الْمَدِينَةَ وَالشَّمْسُ مُرْتَفِعَةٌ فَلَمْ يُعِدْ.
‘Atwaa aliunga mkono rai hiyo.
Na Al-Hasan amesema: “Kama mgonjwa ana maji lakini hapana mtu wa kumpa.”
Ibn ‘Umar alikuja kutoka Al-Jurf na wakati wa Swalaah ya Alasiri ulifika alipokuwa Marbad An-Na’am, kwa hiyo alitayammam, akaswali pale kisha akaingia Madiynah wakati jua lilikuwa bado juu lakini hakuirudia ile Swalaah.
حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ بُكَيْرٍ، قَالَ حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، عَنْ جَعْفَرِ بْنِ رَبِيعَةَ، عَنِ الأَعْرَجِ، قَالَ سَمِعْتُ عُمَيْرًا، مَوْلَى ابْنِ عَبَّاسٍ قَالَ أَقْبَلْتُ أَنَا وَعَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَسَارٍ، مَوْلَى مَيْمُونَةَ زَوْجِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم حَتَّى دَخَلْنَا عَلَى أَبِي جُهَيْمِ بْنِ الْحَارِثِ بْنِ الصِّمَّةِ الأَنْصَارِيِّ فَقَالَ أَبُو الْجُهَيْمِ أَقْبَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم مِنْ نَحْوِ بِئْرِ جَمَلٍ، فَلَقِيَهُ رَجُلٌ فَسَلَّمَ عَلَيْهِ، فَلَمْ يَرُدَّ عَلَيْهِ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم حَتَّى أَقْبَلَ عَلَى الْجِدَارِ، فَمَسَحَ بِوَجْهِهِ وَيَدَيْهِ، ثُمَّ رَدَّ عَلَيْهِ السَّلاَمَ.
Amesimulia Abu Juhaym Al-Answaariy:
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuja akitokea upande wa Bi-ir Jamal akakutana na mtu na akamsalimu. Lakini hakujibu ile Salaam mpaka alipokwenda ukuta wa udongo mpaka akapaka mikono yake na uso wake kwa vumbi (alitayammam) kisha akaitikia Salaam.
Mjalada: 1
|
Kitabu: 7
|
Hadiyth: 333
|
04-Mlango
باب الْمُتَيَمِّمُ هَلْ يَنْفُخُ فِيهِمَا Mtu Anaweza Kupuliza Vumbi Kutoka Kwenye Mikono Yake Anapotayammam (Kabla Ya Kuipitisha Kwenye Uso Wake)
|
حَدَّثَنَا آدَمُ، قَالَ حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنَا الْحَكَمُ، عَنْ ذَرٍّ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبْزَى، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ جَاءَ رَجُلٌ إِلَى عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ فَقَالَ إِنِّي أَجْنَبْتُ فَلَمْ أُصِبِ الْمَاءَ. فَقَالَ عَمَّارُ بْنُ يَاسِرٍ لِعُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ أَمَا تَذْكُرُ أَنَّا كُنَّا فِي سَفَرٍ أَنَا وَأَنْتَ فَأَمَّا أَنْتَ فَلَمْ تُصَلِّ، وَأَمَّا أَنَا فَتَمَعَّكْتُ فَصَلَّيْتُ، فَذَكَرْتُ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " إِنَّمَا كَانَ يَكْفِيكَ هَكَذَا ". فَضَرَبَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بِكَفَّيْهِ الأَرْضَ، وَنَفَخَ فِيهِمَا ثُمَّ مَسَحَ بِهِمَا وَجْهَهُ وَكَفَّيْهِ.
Amesimulia ‘Abdurrahmaan bin Abzaa:
Kutoka kwa baba yake kwamba alikuja kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab na akamwambia: “Niko katika hali ya janaba lakini hapakuwa na maji.” ‘Ammaar bin Yaasir alimwambia ‘Umar bin Al-Khattwaab: “Je, umekumbuka kuwa wewe na mimi (sote tulikuwa na janaba) tulipokuwa safarini pamoja nawe hukuswali lakini mimi nilijibiringisha juu ya ardhi na nikaswali? Nikamtajia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu hilo akasema: “Hakika ilikuwa inatosha kwako kufanya hivyo.” Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipiga kwa wepesi juu ya udongo kwa mikono yake, kisha akapuliza vumbi na akapaka mikono yake juu ya uso na mikono.”
Mjalada: 1
|
Kitabu: 7
|
Hadiyth: 334
|
05-Mlango
باب التَّيَمُّمُ لِلْوَجْهِ وَالْكَفَّيْنِ Tayammum Ni Kwa Uso Na Mikono Miwili
|
حَدَّثَنَا حَجَّاجٌ، قَالَ أَخْبَرَنَا شُعْبَةُ، أَخْبَرَنِي الْحَكَمُ، عَنْ ذَرٍّ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبْزَى، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ عَمَّارٌ بِهَذَا، وَضَرَبَ شُعْبَةُ بِيَدَيْهِ الأَرْضَ، ثُمَّ أَدْنَاهُمَا مِنْ فِيهِ، ثُمَّ مَسَحَ وَجْهَهُ وَكَفَّيْهِ. وَقَالَ النَّضْرُ أَخْبَرَنَا شُعْبَةُ عَنِ الْحَكَمِ قَالَ سَمِعْتُ ذَرًّا يَقُولُ عَنِ ابْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبْزَى قَالَ الْحَكَمُ وَقَدْ سَمِعْتُهُ مِنِ ابْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَنْ أَبِيهِ قَالَ قَالَ عَمَّارٌ.
Amesimulia Sa’iyd bin Amesimulia ‘Abdirrahmaan bin Abzaa:
Kutoka kwa baba yake aliyesema: “Ammaar alisema hivyo (kauli ya hapo juu). Na Shu’bah alipiga kwa wepesi udongo kwa mikono yake na akaileta karibu na mdomo wake (akapuliza vumbi) na akapaka uso kisha akapaka mokono yake.” ‘Ammaar alisema: “Wudhuu (hapa ina maana Tayammum) inatosha kwa Muislamu iwapo hapana maji.”
Mjalada: 1
|
Kitabu: 7
|
Hadiyth: 335
|
حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، قَالَ حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنِ الْحَكَمِ، عَنْ ذَرٍّ، عَنِ ابْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبْزَى، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّهُ شَهِدَ عُمَرَ وَقَالَ لَهُ عَمَّارٌ كُنَّا فِي سَرِيَّةٍ فَأَجْنَبْنَا، وَقَالَ تَفَلَ فِيهِمَا.
Amesimulia ‘Abdurrahmaan bin Abzaa:
Kutoka kwa baba yake kwamba alipokuwa pamoja na ‘Umar, ‘Ammaar alimwambia ‘Umar: “Tulikuwa tumejitenga na tukawa katika janaba na nilipatiza vumbi kwenye mikono yangu (niligaragara juu ya vumbi na nikaswali).”
Mjalada: 1
|
Kitabu: 7
|
Hadiyth: 336
|
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، أَخْبَرَنَا شُعْبَةُ، عَنِ الْحَكَمِ، عَنْ ذَرٍّ، عَنِ ابْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبْزَى، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، قَالَ قَالَ عَمَّارٌ لِعُمَرَ تَمَعَّكْتُ فَأَتَيْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ " يَكْفِيكَ الْوَجْهُ وَالْكَفَّانِ ".
Amesimulia ‘Abdurrahmaan bin Abzaa:
‘Ammaar alimwambia ‘Umar: “Niliiviringisha katika vumbi na nikaenda kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye alisema: “Kupitisha mikono yenye vumbi juu ya uso na migongo ya mikono inatosheleza.”
Mjalada: 1
|
Kitabu: 7
|
Hadiyth: 337
|
حَدَّثَنَا مُسْلِمٌ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنِ الْحَكَمِ، عَنْ ذَرٍّ، عَنِ ابْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، قَالَ شَهِدْتُ عُمَرَ فَقَالَ لَهُ عَمَّارٌ. وَسَاقَ الْحَدِيثَ.
Amesimulia ‘Ammaar:
Kama Hadiyth ya hapo juu.
Mjalada: 1
|
Kitabu: 7
|
Hadiyth: 338
|
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ بَشَّارٍ، قَالَ حَدَّثَنَا غُنْدَرٌ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنِ الْحَكَمِ، عَنْ ذَرٍّ، عَنِ ابْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبْزَى، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ قَالَ عَمَّارٌ فَضَرَبَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بِيَدِهِ الأَرْضَ، فَمَسَحَ وَجْهَهُ وَكَفَّيْهِ.
Amesimulia ‘Ammaar:
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipiga ardhi kwa mikono yake kisha akapaka uso wake na migongo ya mikono yake (alipokuwa akielekeza Tayammum).”
Mjalada: 1
|
Kitabu: 7
|
Hadiyth: 339
|
06-Mlango
باب الصَّعِيدُ الطَّيِّبُ وَضُوءُ الْمُسْلِمِ ، يَكْفِيهِ مِنَ الْمَاءِ Udongo Ulio Safi Unatosha Kwa Muislamu Kuwa Badala Ya Maji Katika Kutawadha (Kama Maji Hayatopatikana)
|
Al-Hasan alisema: “Tayammum inatosheleza isipokuwa kwa mwenye Hadath.”
Yahyaa bin Sa’iyd alisema: “Hapana ubaya kuswali juu ya mbuga (ardhi kavu yenye chumvi) na kutayammam kwayo.”
حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، قَالَ حَدَّثَنِي يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، قَالَ حَدَّثَنَا عَوْفٌ، قَالَ حَدَّثَنَا أَبُو رَجَاءٍ، عَنْ عِمْرَانَ، قَالَ كُنَّا فِي سَفَرٍ مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم وَإِنَّا أَسْرَيْنَا، حَتَّى كُنَّا فِي آخِرِ اللَّيْلِ، وَقَعْنَا وَقْعَةً وَلاَ وَقْعَةَ أَحْلَى عِنْدَ الْمُسَافِرِ مِنْهَا، فَمَا أَيْقَظَنَا إِلاَّ حَرُّ الشَّمْسِ، وَكَانَ أَوَّلَ مَنِ اسْتَيْقَظَ فُلاَنٌ ثُمَّ فُلاَنٌ ثُمَّ فُلاَنٌ ـ يُسَمِّيهِمْ أَبُو رَجَاءٍ فَنَسِيَ عَوْفٌ ـ ثُمَّ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ الرَّابِعُ، وَكَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم إِذَا نَامَ لَمْ يُوقَظْ حَتَّى يَكُونَ هُوَ يَسْتَيْقِظُ، لأَنَّا لاَ نَدْرِي مَا يَحْدُثُ لَهُ فِي نَوْمِهِ، فَلَمَّا اسْتَيْقَظَ عُمَرُ، وَرَأَى مَا أَصَابَ النَّاسَ، وَكَانَ رَجُلاً جَلِيدًا، فَكَبَّرَ وَرَفَعَ صَوْتَهُ بِالتَّكْبِيرِ، فَمَا زَالَ يُكَبِّرُ وَيَرْفَعُ صَوْتَهُ بِالتَّكْبِيرِ حَتَّى اسْتَيْقَظَ لِصَوْتِهِ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَلَمَّا اسْتَيْقَظَ شَكَوْا إِلَيْهِ الَّذِي أَصَابَهُمْ قَالَ " لاَ ضَيْرَ ـ أَوْ لاَ يَضِيرُ ـ ارْتَحِلُوا ". فَارْتَحَلَ فَسَارَ غَيْرَ بَعِيدٍ ثُمَّ نَزَلَ، فَدَعَا بِالْوَضُوءِ، فَتَوَضَّأَ وَنُودِيَ بِالصَّلاَةِ فَصَلَّى بِالنَّاسِ، فَلَمَّا انْفَتَلَ مِنْ صَلاَتِهِ إِذَا هُوَ بِرَجُلٍ مُعْتَزِلٍ لَمْ يُصَلِّ مَعَ الْقَوْمِ قَالَ " مَا مَنَعَكَ يَا فُلاَنُ أَنْ تُصَلِّيَ مَعَ الْقَوْمِ ". قَالَ أَصَابَتْنِي جَنَابَةٌ وَلاَ مَاءَ. قَالَ " عَلَيْكَ بِالصَّعِيدِ، فَإِنَّهُ يَكْفِيكَ ". ثُمَّ سَارَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَاشْتَكَى إِلَيْهِ النَّاسُ مِنَ الْعَطَشِ فَنَزَلَ، فَدَعَا فُلاَنًا ـ كَانَ يُسَمِّيهِ أَبُو رَجَاءٍ نَسِيَهُ عَوْفٌ ـ وَدَعَا عَلِيًّا فَقَالَ " اذْهَبَا فَابْتَغِيَا الْمَاءَ ". فَانْطَلَقَا فَتَلَقَّيَا امْرَأَةً بَيْنَ مَزَادَتَيْنِ ـ أَوْ سَطِيحَتَيْنِ ـ مِنْ مَاءٍ عَلَى بَعِيرٍ لَهَا، فَقَالاَ لَهَا أَيْنَ الْمَاءُ قَالَتْ عَهْدِي بِالْمَاءِ أَمْسِ هَذِهِ السَّاعَةَ، وَنَفَرُنَا خُلُوفًا. قَالاَ لَهَا انْطَلِقِي إِذًا. قَالَتْ إِلَى أَيْنَ قَالاَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم. قَالَتِ الَّذِي يُقَالُ لَهُ الصَّابِئُ قَالاَ هُوَ الَّذِي تَعْنِينَ فَانْطَلِقِي. فَجَاءَا بِهَا إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم وَحَدَّثَاهُ الْحَدِيثَ قَالَ فَاسْتَنْزَلُوهَا عَنْ بَعِيرِهَا وَدَعَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بِإِنَاءٍ، فَفَرَّغَ فِيهِ مِنْ أَفْوَاهِ الْمَزَادَتَيْنِ ـ أَوِ السَّطِيحَتَيْنِ ـ وَأَوْكَأَ أَفْوَاهَهُمَا، وَأَطْلَقَ الْعَزَالِيَ، وَنُودِيَ فِي النَّاسِ اسْقُوا وَاسْتَقُوا. فَسَقَى مَنْ شَاءَ، وَاسْتَقَى مَنْ شَاءَ، وَكَانَ آخِرَ ذَاكَ أَنْ أَعْطَى الَّذِي أَصَابَتْهُ الْجَنَابَةُ إِنَاءً مِنْ مَاءٍ قَالَ " اذْهَبْ، فَأَفْرِغْهُ عَلَيْكَ ". وَهْىَ قَائِمَةٌ تَنْظُرُ إِلَى مَا يُفْعَلُ بِمَائِهَا، وَايْمُ اللَّهِ لَقَدْ أُقْلِعَ عَنْهَا، وَإِنَّهُ لَيُخَيَّلُ إِلَيْنَا أَنَّهَا أَشَدُّ مِلأَةً مِنْهَا حِينَ ابْتَدَأَ فِيهَا، فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " اجْمَعُوا لَهَا ". فَجَمَعُوا لَهَا مِنْ بَيْنِ عَجْوَةٍ وَدَقِيقَةٍ وَسَوِيقَةٍ، حَتَّى جَمَعُوا لَهَا طَعَامًا، فَجَعَلُوهَا فِي ثَوْبٍ، وَحَمَلُوهَا عَلَى بَعِيرِهَا، وَوَضَعُوا الثَّوْبَ بَيْنَ يَدَيْهَا قَالَ لَهَا " تَعْلَمِينَ مَا رَزِئْنَا مِنْ مَائِكِ شَيْئًا، وَلَكِنَّ اللَّهَ هُوَ الَّذِي أَسْقَانَا ". فَأَتَتْ أَهْلَهَا، وَقَدِ احْتَبَسَتْ عَنْهُمْ قَالُوا مَا حَبَسَكِ يَا فُلاَنَةُ قَالَتِ الْعَجَبُ، لَقِيَنِي رَجُلاَنِ فَذَهَبَا بِي إِلَى هَذَا الَّذِي يُقَالُ لَهُ الصَّابِئُ، فَفَعَلَ كَذَا وَكَذَا، فَوَاللَّهِ إِنَّهُ لأَسْحَرُ النَّاسِ مِنْ بَيْنِ هَذِهِ وَهَذِهِ. وَقَالَتْ بِإِصْبَعَيْهَا الْوُسْطَى وَالسَّبَّابَةِ، فَرَفَعَتْهُمَا إِلَى السَّمَاءِ ـ تَعْنِي السَّمَاءَ وَالأَرْضَ ـ أَوْ إِنَّهُ لَرَسُولُ اللَّهِ حَقًّا، فَكَانَ الْمُسْلِمُونَ بَعْدَ ذَلِكَ يُغِيرُونَ عَلَى مَنْ حَوْلَهَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ، وَلاَ يُصِيبُونَ الصِّرْمَ الَّذِي هِيَ مِنْهُ، فَقَالَتْ يَوْمًا لِقَوْمِهَا مَا أُرَى أَنَّ هَؤُلاَءِ الْقَوْمَ يَدَعُونَكُمْ عَمْدًا، فَهَلْ لَكُمْ فِي الإِسْلاَمِ فَأَطَاعُوهَا فَدَخَلُوا فِي الإِسْلاَمِ.
Amesimulia ‘Imraan:
Siku moja tulikuwa tukisafiri na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) tukaendelea na safari mpaka katikati ya usiku na tukatua pahali na tukalala usingizi mzito. Hapana kitu kitamu kama usingizi wa msafiri kipindi cha mwisho cha usiku. Kwa hiyo ni joto la jua tu ndio lililotuamsha na kuanza kuamka alikuwa fulani, kisha fulani kisha fulani (msimulizi ‘Awf alisema kuwa Abu Rajaa-a alimweleza majina yao lakini aliyasahau) na mtu wa nne kuamka alikuwa ‘Umar bin Al-Khattwaab. Na wakati wowote Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipolala, hapana mtu aliyemwamsha mpaka alipoamka mwenyewe kwani hatakujua kilichokuwa kinatokea (akipewa Wahy) usingizini. Kwa hiyo ‘Umar aliamka na kuiona hali ya watu, na alikuwa mtu makini sana. Akasema: “Allahu Akbar!” Akapandisha sauti yake kwa Takbiyr, na akaendelea kusema kwa sauti mpaka Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaamka. Alipoamka, watu walimwarifu juu ya yale yaliyowatokezea. Akasema: “Hapana madhara.” Au “Haidhuru, ondokeni!” Kwa hiyo waliondoka kutoka eneo lile, baada ya kwenda masafa kidogo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisimama na akataka maji ya kutawadhia. Kwa hiyo alitawadha na kukaadhiniwa na akaswalisha. Baada ya kutoa Salaam, alimwona mtu amekaa kimya ambaye hakuswali nao. Akasema: “Ee fulani bin fulani! Nini kimekuzuia kuswalia pamoja nasi?” Akajibu: “Nina janaba na hapana maji.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Tayammum kwa udongo safi na hiyo inatosheleza.” Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliendelea na watu wakamlalamikia kiu. Alishuka wakati huo huo na alimwita mtu (msimulizi ‘Awf anasema kuwa Abu Rajaa-a alitaja jina lake lakini alilisahau) na ‘Aliy aliwaamuru wakatafute maji. Hivyo walikwenda kutafuta maji na walimkuta mwanamke juu ya ngamia wake katikati mlikuwa na viriba viwili vya maji. Walimwuliza: “Tunaweza kupata wapi maji?” Alijibu: “Nilikuwa jana katika sehemu yenye maji muda huu na watu wangu wako nyuma yangu.” Walimwomba wafuatane naye. Aliuliza. “Wapi?” Walijibu “Kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)” Akasema: “Mna maana mtu anayeitwa Asw-Swaabiyy (mwenye dini mpya)?” Wakasema: “Ndiyo mtu huyo huyo unayemaanisha, basi twende.! Wakampeleka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na wakasimulia kisa kizima. Akasema: “Msaidieni ateremke mnyama wake.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaomba mtungi kisha akafungua midomo ya viriba na akamiminia maji mtunguni. Kisha alifunga uwazi mkubwa na kufungua uwazi mdogo na akawataka watu wanywe na kuwanywisha wanyama wao maji. Kwa hivyo wote waliwanywesha wanyama wao na wao pia wote wakakata kiu chao na pia wakawapa maji wengineo. Wa mwisho ni Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye alimpa mtungi mzima yule aliyekuwa na janaba na alimwambia ajiwagie mwili mzima. Yule mwanamke alikuwa amesimama akiangalia waliyoyafanyia maji yake. Wa-Allaahi viriba vyake viliporejeshwa vilionekana kujaa kuliko mwanzo (miuujiza wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akatuamuru tumkusanyie zawadi. Hivyo basi tende, unga na sawyiq (aina ya chakula cha shayiri) vilikusanywa na kufungwa kwenye kipande cha nguo. Alisaidiwa kumpanda mnyama wake na vyakula viliwekwa mbele yake kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Hatujachukua maji yako lakini Allaah Ndiye Aliyetunywesha.” Mwanamke huyo akarejea nyumbani akiwa amechelewa. Jamaa zake wakamwuliza. ”Ee fulani! Nini kimekuchelewesha? Akajibu: “Jambo la kustaajabisha! Watu wawili walikutana nami na wakanipeleka kwa Asw-Swaabiyy na alifanya kadha na kadha. Wa-Allaahi hakika ima yeye ni mchawi mkubwa kati ya hiki na hiki (akionyesha kwa vidole vyake juu mbinguni akiashiria mbingu na ardhi) au yeye ni Rasuli wa kweli.”
Baadaye Waislamu waliwashambulia mapagani waliokuwa majirani naye lakini hawakugusa kijiji chake. Siku moja akawaambia watu wake: “Nadhani hawa watu wanakuacheni kwa lengo maalumu. Je mna mwelekeo katika Uislamu?” Walimtii na wote wakasilimu.
Abu ‘Abdillaah alisema: Neno Asw-Swaabiyy maana yake ni: “Mtu aliyeacha dini yake ya zamani na kuingia katika dini mpya.
‘Abdul-Aaliyah alisema: Asw-Swaabiyy ni madhahebu ya watu wa kitabu ambao wanasoma Kitabu cha Zabuwr.”
Mjalada: 1
|
Kitabu: 7
|
Hadiyth: 340
|
07-Mlango
باب إِذَا خَافَ الْجُنُبُ عَلَى نَفْسِهِ الْمَرَضَ أَوِ الْمَوْتَ أَوْ خَافَ الْعَطَشَ، تَيَمَّمَ Mwenye Janaba Anaweza Kutayammum Iwapo Anachelea Maradhi, Kifo Au Kiu
|
وَيُذْكَرُ أَنَّ عَمْرَو بْنَ الْعَاصِ أَجْنَبَ فِي لَيْلَةٍ بَارِدَةٍ فَتَيَمَّمَ وَتَلاَ: {وَلاَ تَقْتُلُوا أَنْفُسَكُمْ إِنَّ اللَّهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا} فَذَكَرَ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَلَمْ يُعَنِّفْ.
Inasemekana kuwa wakati mmoja ‘Amri bin ‘Aasw alipata janaba usiku kwenye baridi kali. Alitayammam na akasoma:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُم بَيْنَكُم بِالْبَاطِلِ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً عَن تَرَاضٍ مِّنكُمْ ۚ وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا ﴿٢٩﴾
Enyi walioamini! Msiliane mali zenu kwa ubatilifu, isipokuwa iwe biashara kwa kuridhiana baina yenu. Wala msijiue. Hakika Allaah ni Mwenye kuwarehemuni. [An-Nisaa: 29]
حَدَّثَنَا بِشْرُ بْنُ خَالِدٍ، قَالَ حَدَّثَنَا مُحَمَّدٌ ـ هُوَ غُنْدَرٌ ـ عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ، عَنْ أَبِي وَائِلٍ، قَالَ قَالَ أَبُو مُوسَى لِعَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ إِذَا لَمْ يَجِدِ الْمَاءَ لاَ يُصَلِّي. قَالَ عَبْدُ اللَّهِ لَوْ رَخَّصْتُ لَهُمْ فِي هَذَا، كَانَ إِذَا وَجَدَ أَحَدُهُمُ الْبَرْدَ قَالَ هَكَذَا ـ يَعْنِي تَيَمَّمَ وَصَلَّى ـ قَالَ قُلْتُ فَأَيْنَ قَوْلُ عَمَّارٍ لِعُمَرَ قَالَ إِنِّي لَمْ أَرَ عُمَرَ قَنِعَ بِقَوْلِ عَمَّارٍ.
Amesimulia Abu Waail:
Abu Muwsaa alimwambia ‘Abdullaah bin Mas’uwd: “Endapo mtu hatopata maji ya kutawadhia anaweza kuacha kuswali?” ‘Abdullaah akasema: ”Ukiwapa ruhusa ya Tayammum watatayammam (kisha wataswali) hata kama maji yapo ikiwa watayahisi ni ya baridi. Abu Muwsaa akasema: “Vipi kauli ya ‘Ammaar kwa Umar?” ‘Abdullaah Akajibu: “Umar hakuridhika na kauli hii.”
Mjalada: 1
|
Kitabu: 7
|
Hadiyth: 341
|
حَدَّثَنَا عُمَرُ بْنُ حَفْصٍ، قَالَ حَدَّثَنَا أَبِي قَالَ، حَدَّثَنَا الأَعْمَشُ، قَالَ سَمِعْتُ شَقِيقَ بْنَ سَلَمَةَ، قَالَ كُنْتُ عِنْدَ عَبْدِ اللَّهِ وَأَبِي مُوسَى فَقَالَ لَهُ أَبُو مُوسَى أَرَأَيْتَ يَا أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ إِذَا أَجْنَبَ فَلَمْ يَجِدْ، مَاءً كَيْفَ يَصْنَعُ فَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ لاَ يُصَلِّي حَتَّى يَجِدَ الْمَاءَ. فَقَالَ أَبُو مُوسَى فَكَيْفَ تَصْنَعُ بِقَوْلِ عَمَّارٍ حِينَ قَالَ لَهُ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " كَانَ يَكْفِيكَ " قَالَ أَلَمْ تَرَ عُمَرَ لَمْ يَقْنَعْ بِذَلِكَ. فَقَالَ أَبُو مُوسَى فَدَعْنَا مِنْ قَوْلِ عَمَّارٍ، كَيْفَ تَصْنَعُ بِهَذِهِ الآيَةِ فَمَا دَرَى عَبْدُ اللَّهِ مَا يَقُولُ فَقَالَ إِنَّا لَوْ رَخَّصْنَا لَهُمْ فِي هَذَا لأَوْشَكَ إِذَا بَرَدَ عَلَى أَحَدِهِمُ الْمَاءُ أَنْ يَدَعَهُ وَيَتَيَمَّمَ. فَقُلْتُ لِشَقِيقٍ فَإِنَّمَا كَرِهَ عَبْدُ اللَّهِ لِهَذَا قَالَ نَعَمْ.
Amesimulia Shaqiyq Bin Salamah:
Nilikuwa pamoja na ‘Abdullaah na Abu Muwsaa; wa mwisho alimwuliza wa mwanzo: “Yaa Abaa ‘Abdirrahmaam! Je, vipi iwapo mtu atakuwa na janaba na hapana maji?” ‘Abdullaah Akajibu: “Usiswali mpaka maji yapatikane.” Abu Muwsaa akasema: “Je, unasemaje kuhusu kauli ya ‘Ammaar (aliyeamrishwa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم atayammam?). Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwambia: “Tayammam na hilo linatosheleza.” ‘Abdullaah akasema: “Huoni kuwa ‘Umar hakuridhika na kauli ya ‘Ammaar?” Abu ‘Ammaar akasema: “Sawa, acheni kauli ya ‘Ammaar, lakini atasema nini juu ya Aayah (ya Tayammum)?” ‘Abdullaah alinyamaza kisha akasema: “Kama tungeliwaruhusu hivyo, bila shaka wangetayammam hata kama maji yangelikuwepo, iwapo mmoja wao angeona maji ya ubaridi.” Msimulizi aliongeza: Nilimwambia Shaqiyq: “Kwa hiyo ‘Abdullaah alichukia Tayammum kwa sababu hii tu?” Akajibu: “Naam.”
Mjalada: 1
|
Kitabu: 7
|
Hadiyth: 342
|
08-Mlango
باب التَّيَمُّمُ ضَرْبَةٌ Tayammum Kwa Pigo Moja Jepesi Juu Ya Udongo
|
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سَلاَمٍ، قَالَ أَخْبَرَنَا أَبُو مُعَاوِيَةَ، عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ شَقِيقٍ، قَالَ كُنْتُ جَالِسًا مَعَ عَبْدِ اللَّهِ وَأَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ فَقَالَ لَهُ أَبُو مُوسَى لَوْ أَنَّ رَجُلاً أَجْنَبَ، فَلَمْ يَجِدِ الْمَاءَ شَهْرًا، أَمَا كَانَ يَتَيَمَّمُ وَيُصَلِّي فَكَيْفَ تَصْنَعُونَ بِهَذِهِ الآيَةِ فِي سُورَةِ الْمَائِدَةِ {فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ لَوْ رُخِّصَ لَهُمْ فِي هَذَا لأَوْشَكُوا إِذَا بَرَدَ عَلَيْهِمُ الْمَاءُ أَنْ يَتَيَمَّمُوا الصَّعِيدَ. قُلْتُ وَإِنَّمَا كَرِهْتُمْ هَذَا لِذَا قَالَ نَعَمْ. فَقَالَ أَبُو مُوسَى أَلَمْ تَسْمَعْ قَوْلَ عَمَّارٍ لِعُمَرَ بَعَثَنِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي حَاجَةٍ فَأَجْنَبْتُ، فَلَمْ أَجِدِ الْمَاءَ، فَتَمَرَّغْتُ فِي الصَّعِيدِ كَمَا تَمَرَّغُ الدَّابَّةُ، فَذَكَرْتُ ذَلِكَ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ " إِنَّمَا كَانَ يَكْفِيكَ أَنْ تَصْنَعَ هَكَذَا ". فَضَرَبَ بِكَفِّهِ ضَرْبَةً عَلَى الأَرْضِ ثُمَّ نَفَضَهَا، ثُمَّ مَسَحَ بِهَا ظَهْرَ كَفِّهِ بِشِمَالِهِ، أَوْ ظَهْرَ شِمَالِهِ بِكَفِّهِ، ثُمَّ مَسَحَ بِهِمَا وَجْهَهُ فَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ أَفَلَمْ تَرَ عُمَرَ لَمْ يَقْنَعْ بِقَوْلِ عَمَّارٍ وَزَادَ يَعْلَى عَنِ الأَعْمَشِ عَنْ شَقِيقٍ كُنْتُ مَعَ عَبْدِ اللَّهِ وَأَبِي مُوسَى فَقَالَ أَبُو مُوسَى أَلَمْ تَسْمَعْ قَوْلَ عَمَّارٍ لِعُمَرَ إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بَعَثَنِي أَنَا وَأَنْتَ فَأَجْنَبْتُ فَتَمَعَّكْتُ بِالصَّعِيدِ، فَأَتَيْنَا رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَأَخْبَرْنَاهُ فَقَالَ " إِنَّمَا كَانَ يَكْفِيكَ هَكَذَا ". وَمَسَحَ وَجْهَهُ وَكَفَّيْهِ وَاحِدَةً
Amesimulia Al-A’mash
Kutoka kwa Shaqiyq amesema: Nilipokuwa nimekaa na ‘Abdullaah na Abu Muwsaa Al-Ash’ariyy, wa pili alimwuliza wa mwanzo: “Iwapo mtu atakuwa na janaba na asipate maji kwa mwezi mmoja, anaweza kutayammam na akasawli?’ (Alikanusha) Abu Muwsaa akasema: “Unasemaje juu ya Aayah hii katika Suwrah Al-Maaidah:
فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا
Kisha hamkupata maji; basi tayammamuni (ikusudieni) ardhi kwa juu [Al-Maaidah: 6]
‘Abdullaah alijibu: “Kama tungeliruhusu basi wangetayammam kwa udongo safi hata kama maji yangekuwepo lakini ya ubaridi.” Nikamwambia Shaqiyq: “Kwa hiyo ulichukia kutayammam kwa sababu hii?” Shaqiyq Akajibu: “Naam.” (Shaqiq aliongeza: “Abu Muwsaa alisema: “Hujasikia kauli ya ‘Ammaar kwa ‘Umar? Alisema: Nilitumwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kufanya kazi fulani na nikawa katika janaba na hapakuwa na maji hivyo nikajibiringisha kwenye vumbi (safi) kama afanyavyo mnyama, na nilipomtajia jambo hilo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: “Hakika inakutosheleza kufanya hivi:” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akapiga pigo jepesi juu ya ardhi kwa mkono wake mara moja na kuipuliza, kisha akapitisha mkono wake (kushoto) juu ya mgongo wa mkono wake wa kulia au mkono wake (kulia) juu ya mgongo wa mkono wa kushoto kisha akapaka juu ya uso wake. Kwa hiyo ‘Abdullaah alimwambia Abu Muwsaa: “Je, hivi hujui kuwa ‘Umar hakuridhishwa na kauli ya ‘Ammaar?”
Shaqiyq akasimulia: Nilipokuwa na ‘Abdullaah na Abu Muwsaa, wa pili alimwambia na mwanzo, “Hujasikia kauli ya ‘Ammaar kwa ‘Umar? Alisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alinituma mimi na wewe na nikapata janaba na nikajibiringisha katika vumbi (safi) (kwa tayammum). Tuliporejea kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nilimjulisha akasema: “Hakika inakutosheleza kufanya hivyo.” Kupitisha mikono yake juu ya uso wake na migongo ya mikono yake mara moja tu.
Mjalada: 1
|
Kitabu: 7
|
Hadiyth: 343
|
09-Mlango
|
حَدَّثَنَا عَبْدَانُ، قَالَ أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ، قَالَ أَخْبَرَنَا عَوْفٌ، عَنْ أَبِي رَجَاءٍ، قَالَ حَدَّثَنَا عِمْرَانُ بْنُ حُصَيْنٍ الْخُزَاعِيُّ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم رَأَى رَجُلاً مُعْتَزِلاً لَمْ يُصَلِّ فِي الْقَوْمِ فَقَالَ " يَا فُلاَنُ مَا مَنَعَكَ أَنْ تُصَلِّيَ فِي الْقَوْمِ ". فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَصَابَتْنِي جَنَابَةٌ وَلاَ مَاءَ. قَالَ " عَلَيْكَ بِالصَّعِيدِ فَإِنَّهُ يَكْفِيكَ ".
Amesimulia ‘Imraan bin Huswayn Al-Khuzaa’iy:
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwona mtu amejitenga na hakuswali na watu. Alimwuliza: “Ee fulani! Nini kilichokuzuia kuswali na watu wengine?” Akajibu: “Ee Rasuli wa Allaah! Nina janaba na hakuna maji.” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Tayammam kwa udongo safi na hilo litakutosheleza.”
Mjalada: 1
|
Kitabu: 7
|
Hadiyth: 344
|