01-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyeyekevu Wake: Kutokulalamika Chakula Nyumbani Kwake
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
01-Unyeyekevu Wake Wa Kutokulalamika Chakula Nyumbani
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Hakuwa mwenye makuu katika chakula, akila chochote alichopikiwa bila ya kulalamika:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ: مَا رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَابَ طَعَامًا قَطُّ كَانَ إِذَا اشْتَهَاهُ أَكَلَهُ وَإِنْ لَمْ يَشْتَهِهِ سَكَتَ . مسلم
Abuu Huraryrah amesema: “Sijapatapo kamwe kumuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akitia dosari chakula. Alikuwa anapokipenda anakila, na asipokipenda ananyamaza.” [Muslim]
Na Riwaayah nyenginezo
“Asipokipenda alikiacha.” [Al-Bukhaariy na wengineo]