02-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyeyekevu Wake: Alikiri Kuwa Manabii Wengineo Ni Bora Kuliko Yeye
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
02-Unyeyekevu Wake Alikiri Kuwa Manabii Wengineo Ni Bora Kuliko Yeye
Juu ya kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Nabiy wa mwisho na ndiye ambaye Allaah (عزّ وجلّ) Amejaalia fadhila nyingi kulikoni Manabii na Rusuli wengineo; mfano yeye ndiye aliyewasalisha Manabii wote alipofika Masjid Al-Aqswaa katika safari ya Al-Israa wal Mi’raaj, lakini hakujiona kuwa yeye ni mbora kuliko wengineo, kwa sababu ya unyenyekevu wake aliwafadhilisha Manabii wengineo kama ilivyokuja katika Hadiyth:
عنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضى الله عنه قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ مِنَ الْيَهُودِ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَدْ لُطِمَ وَجْهُهُ وَقَالَ: يَا مُحَمَّدُ إِنَّ رَجُلاً مِنْ أَصْحَابِكَ مِنَ الأَنْصَارِ لَطَمَ وَجْهِي. قَالَ: ((ادْعُوهُ)) فَدَعَوْهُ قَالَ: ((لِمَ لَطَمْتَ وَجْهَهُ)) قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي مَرَرْتُ بِالْيَهُودِ فَسَمِعْتُهُ يَقُولُ وَالَّذِي اصْطَفَى مُوسَى عَلَى الْبَشَرِ. فَقُلْتُ: وَعَلَى مُحَمَّدٍ، وَأَخَذَتْنِي غَضْبَةٌ فَلَطَمْتُهُ. قَالَ: ((لاَ تُخَيِّرُونِي مِنْ بَيْنِ الأَنْبِيَاءِ، فَإِنَّ النَّاسَ يَصْعَقُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَأَكُونُ أَوَّلَ مَنْ يُفِيقُ، فَإِذَا أَنَا بِمُوسَى آخِذٌ بِقَائِمَةٍ مِنْ قَوَائِمِ الْعَرْشِ، فَلاَ أَدْرِي أَفَاقَ قَبْلِي أَمْ جُزِيَ بِصَعْقَةِ الطُّورِ))
Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) amehadithia: Alikuja Myahudi mmoja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye alipigwa kibao usoni akasema: “Ee Muhammad! Mmoja kati ya Maswahaba zako wa ki-Answaariy amenipiga kibao!” Akasema: ((Mwiteni!)). Akaitwa akamuuliza: (Kwanini umempiga kibao usoni?)) Akasema: “Ee Rasuli wa Allaah, mimi nilipita kwa Myahudi nikamsikia Anasema: Naapa kwa Ambaye Amechagua Muwsaa kuliko walimwengu wote.” Nikamwambia: “Bali Muhammad (kuliko wote).” Basi nikaghadhibika nikampiga kibao usoni.” Akasema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Msinifadhilishe juu ya Manabii wengineo, kwani hakika Siku ya Qiyaamah watu watazimia na nitakuwa mimi ni wa kwanza kupata fahamu. Kisha nitamuona Muwsaa akikamata nguzo moja ya ‘Arsh. Sitojua kama kama alipata fahamu kabla yangu au ni mshtuko ulimtosheleza alioupata katika Mlima (alipomuomba Allaah amtazame alipokuwa hai)) [Al-Bukhaari]
Na akamfadhilisha Nabiy Ibraahiym (عليه السلام) katika Hadiyth:
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: يَا خَيْرَ الْبَرِيَّةِ! فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((ذَاكَ إِبْرَاهِيمُ عَلَيْهِ السَّلَام)) مسلم
Kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه) amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Ee kiumbe bora kabisa!” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamjibu: “Huyo ni Ibraahiym ((عليه السلام [Muslim]
Na akamfadhilisha Nabiy Yuwnus (عليه السلام) katika Hadiyth:
عن أبي هريرة رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((؟مَا يَنْبَغِى لِعَبْدٍ أَنْ يَقُولَ أَنَا خَيْرٌ مِنْ يُونُسَ بْنِ مَتَّى عَلَيْهِ السَّلاَمُ))
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Haipasi mja yeyote aseme kuwa mimi ni mbora kuliko Yuwnus ibn Mattaaعليه السلام (( [Al-Bukhaariy]
Na akamfadhilisha Nabiy Yuwsuf (عليه السلام) :
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قِيلَ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم: مَنْ أَكْرَمُ النَّاسِ قَالَ: ((أَكْرَمُهُمْ أَتْقَاهُمْ)) قَالُوا يَا نَبِيَّ اللَّهِ، لَيْسَ عَنْ هَذَا نَسْأَلُكَ. قَالَ: ((فَأَكْرَمُ النَّاسِ يُوسُفُ نَبِيُّ اللَّهِ ابْنُ نَبِيِّ اللَّهِ ابْنِ نَبِيِّ اللَّهِ ابْنِ خَلِيلِ اللَّهِ)) قَالُوا لَيْسَ عَنْ هَذَا نَسْأَلُكَ. قَالَ: ((فَعَنْ مَعَادِنِ الْعَرَبِ تَسْأَلُونِي)) قَالُوا نَعَمْ. قَالَ: ((فَخِيَارُكُمْ فِي الْجَاهِلِيَّةِ خِيَارُكُمْ فِي الإِسْلاَمِ إِذَا فَقِهُوا)) البخاري
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia: Watu walimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Nani aliye mtukufu zaidi kati ya watu?” Akasema: ((Aliye mtukufu zaidi ni ambaye mwenye taqwa zaidi)). Wakasema: “Ee Nabiy wa Allaah, hatukuulizi kuhusu hivyo!” Akasema: ((Basi aliye mtukufu zaidi kati ya watu ni Yuwsuf ambaye ni Nabiy wa Allaah, mwana wa Nabiy wa Allaah, mwana wa Nabiy wa Allaah, mwana wa Khaliyl wa Allaah)). Wakasema: “Hatukuulizi kuhusu hivyo!” Akasema: ((Basi hivyo mnataka kuniuliza kuhusu majadi wa Kiarabu?)) Wakasema: “Naam.” Akasema: ((Wale waliokuwa wabora kabisa katika Ujaahiliyyah (kabla ya Uislaam) ndio wabora kabisa katika Uislaam, ikiwa watakuwa na ufahamu wa kina (wa Dini yao)) [Al-Bukhaariy]
Faida: Nabiy Yuwsuf (عليه السلام) ni mwana wa Nabiy Ya’quwb (عليه السلام) mwana wa Nabiy Is-haaq (عليه السلام) mwana wa Nabiy Ibraahiym (عليه السلام).