03-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyeyekevu Wake: Akifanya Kazi Za Nyumbani Kwake Na Kuwahudumia Ahli Wake

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

03-Unyenyekevu Wake: Akifanya Kazi Za  Nyumbani Kwake Na Kuwahudumia Ahli Wake

 

www.alhidaaya.com

 

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisaidia kazi za nyumba kama kufagia na usafi mwingine wa nyumba na akijihudumia mwenyewe na kuwahudumia ahli wake, kwa dalili zifuatazo:

 

 

  عَنِ الأَسْوَدِ، قَالَ سَأَلْتُ عَائِشَةَ مَا كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَصْنَعُ فِي بَيْتِهِ قَالَتْ كَانَ يَكُونُ فِي مِهْنَةِ أَهْلِهِ ـ تَعْنِي خِدْمَةَ أَهْلِهِ ـ فَإِذَا حَضَرَتِ الصَّلاَةُ خَرَجَ إِلَى الصَّلاَةِ‏.‏

 

Kutoka kwa Al-Aswad ambaye amesema:  Nilimuuliza ‘Aaishah  (رضي الله عنها): Je, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akifanya nini nyumbani kwake? Akajibu:  “Alikuwa akijishughulisha kuwahudumia ahli wake, na inaponadiwa Swalaah hutoka kwenda kuswali.”  [Al-Bukhaariy na wengineo]

 

 

Pia:

 

عن عائشةَ قالت : سأَلها رجُلٌ : هل كان رسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم يعمَلُ في بيتِه ؟ قالت : نَعم كان رسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم يخصِفُ نعلَه ويَخيطُ ثوبَه ويعمَلُ في بيتِه كما يعمَلُ أحَدُكم في بيتِه

 

‘Aaishah  (رضي الله عنها) amesema:  Mtu mmoja alimuuliza: Je, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akifanya kazi nyumbani kwake?  Akajibu:  “Naam. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akitengeneza viatu vyake na  akishona viraka vya nguo zake na akifanya kazi kama afanyavyo kazi mmoja wenu nyumbani mwake.”  [Ahmad, Adab Al-Mufrad, Ibn Hibban na ameipa daraja ya Swahiyh Al-Albaaniy katika Takhriyj Mishkaat Al-Maswaabiyh [5759]

 

Pia:

 

 وقد سئلت عَائِشَة رضي الله عنها : " مَا كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَعْمَلُ فِي بَيْتِهِ؟ فقَالَتْ: كَانَ بَشَرًا مِنَ الْبَشَرِ يَفْلِي ثَوْبَهُ ، وَيَحْلُبُ شَاتَهُ، وَيَخْدُمُ نَفْسَهُ  .
رواه أحمد (26194) ، وصححه الألباني في "الصحيحة(671) .

Aliulizwa ‘Aaishah  (رضي الله عنها): Je, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akifanya kazi nyumbani kwake? Akajibu:  Yeye ni bin Aadam kama walivyo wana Aadam, wengineo; alikuwa akisafisha nguo zake, akikamua maziwa mbuzi wake, na akijihudumia mwenyewe.”  [Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Asw-Swahiyhah [671]

 

 

 

 

Share