Vibibi
Vipimo
Mchele - 2 Vikombe
Tui la nazi - 1 1/2 Kikombe
Mafuta - 1 kijiko cha supu
Hamira - 2 Vijiko vya chai
Unga wa ngano - 1 kijiko cha supu
Hiliki - kiasi upendavyo
Sukari - ¾ au 1 Kikombe
Namna Ya Kupika Na Kutayarisha
- Osha na roweka mchele usiku mzima ndani ya maji baridi.
- Mimina vifaa vyote isipokuwa sukari , ndani ya mashine ya kusagia (blender) na usage mpaka mchele uwe laini.
- Mimina ndani ya bakuli na ufinike , kisha weka pahali penye joto ili mchanganyiko ufure.
- Ukishafura , mimina sukari na changanya vizuri ; ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.
- Weka chuma kipate moto.
- Paka mafuta au samli kidogo kwenye chuma kisha mimina mchanganyiko kiasi kuunda duara na ufunike.
- Utazame ikishaiva upande mmoja , geuza upande wa pili mpaka iwe tayari.
- Endelea Mpaka umalize mchanganyiko wote; panga kwenye sahani na tayari kuliwa.
Kidokezo
Unaweza kutumia chuma kisichoganda ( non stick ) ; nacho hakitaraji kutiwa mafuta.
|