Buns Za Nyama Ya Kusaga (Aina Ya 2)
Buns Za Nyama Ya Kusaga (Aina Ya 2)
Vipimo
Mayai - 4
Mafuta- 1 kikombe
Maziwa - 1kikombe
Chumvi - kiasi
Hamira- 1 1/2 kijiko cha supu
Unga - kiasi
Habat suda( blackseed)- 1 kijiko cha supu
Nyama yakima kiasi ipike kama ya sambusa
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Kwenye chombo kikubwa changanya mayai, mafuta, maziwa, chumvi changanya vizuri
- Tia hamira na habat suda kisha mimina unga kidogo kidogo mpaka mchanganyiko ushikane uwe laini.
- Iwache ifure,ukisha fura kata madonge ya kiasi ujaze nyama katikati kisha ufunge iwe duwara panga kwenye sinia kisha yapake maziwa kwa juu
- Choma kwa moto wa 350 mpaka zibadilike rangi na yawive vizuri .
- Iwache ipoe kisha itakuwa tayari kuliwa .
Kidokezo: unaweza kujaza feta cheese na zaituni badala ya nyama pia inakuwa nzuri .