Buns Tamu Za Ufuta
Buns Tamu Za Ufuta
Vipimo
Unga - 4 Vikombe vya chai
Sukari - 4 vijiko vya supu
Chumvi - 1 Kijiko cha chai
Hamira - 1 Kijiko cha supu
Baking powder - 1 Kijiko cha chai
Siagi - ¼ Kikombe cha chai
Maziwa - 1 ½ Vikombe vha chai
Yai - 1 Moja
Ufuta - Kiasi ya kunyunyizia juu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katika bakuli changanya vipimo vyote isipikuwa ufuta.
- Kisha ukande unga huku unanyunyizia unga ukiwa unashika.
- Funika mchanganyiko na weka pahali penye joto hadi iimuke.
- Halafu fanya viduara na viweke kwenye treya ya kuchomea iliyopakwa siagi.
- Ziache pahali penye joto hadi zimuuke kwa mara ya pili.
- Washa oveni moto wa 350°.
- Pakiza (brush) Yai uliopiga au maziwa juu ya vile vidonge kisha nyunyizia ufuta juu.
- Kisha vumbika kwenye oveni kwa muda wa dakika 15 hivi na kuweka moto wa juu hadi ziive na kugeuka rangi na zitakuwa tayari kuliwa.
