Mahamri -Maandazi Ya Kuoka (baked)
Mahamri -Maandazi Ya Kuoka (baked)
Vipimo
Unga - 3 Magi
Maziwa ya vuguvugu (warm) - 1 Magi
Sukari - ½ Magi
Maziwa ya unga - ½ Magi
Iliki ya unga - ¼ Kijiko cha chai
Baking powder - 1 Kijiko cha chai
Siagi iliyoyeyushwa - 1 Kikombe cha kahawa
Mafuta - 1 Kikombe cha kahawa
Viini vya mayai (yolks) - 2
Siagi au mafuta zaidi ya kupakiza
Vipimo Vya Hamira
Hamira - 2 Vijiko vya supu
Unga wa ngano - 1 Kijiko cha supu
Maji- 1 ½ Vikombe vya kahawa
Sukari - 1 Kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katika kibakuli changanya hamira, unga, maji na sukari kwa kijiko na iache iimuke kama dakika 5 hivi.
- Changanya vipimo viliyobakia ( isipokuwa baking powder) Katika bakuli la mashine. Kisha tia ule mchanganyiko wa hamira na uendelee kuchanganya kwa muda wa dakika 8. Halafu tia baking powder na changanya tena dakika 3 zaidi.Funika na iaache kwa dakika 5.
- Chukuwa treya na uipake siagi au mafuta kisha nyunyizia unga kidogo tu.
- Paka mikono yako mafuta ukishika mchanganyiko wa unga kwani utakuwa unanyata mara ya kwanza.
- Gawanya donge la unga mara 8 sawa sawa.
- Kisha funika na iiache dakika 10.
- Halafu Sukuma kila kidonge kwa kadri ya mviringo wa nchi 5 kwa upana kisha kata mara nne.
- Panga mahamri katika treya na uwache nafasi ya kiasi baina kila moja.
- Iache iimuke pahali penye joto kwa muda wa masaa mmoja na nusu hivi.
- Oka (bake) katika oveni iliyokwisha kupata moto wa 180°C kwa muda wa dakika 8 au hadi igeuke rangi ya hudhurungi isiyokolea.