Mikate Ya Maji Ya Vitunguu Na Kotimiri
Mikate Ya Maji Ya Vitunguu Na Kotimiri
Vipimo
Unga mweupe - 2 vikombe vikubwa
Mayai - 2
Vitunguu - 2
Kotimiri - 1 msongo (bunch)
Maziwa - 3 vijiko vya kulia
Maji - 3 Vikombe
Chumvi - 1 kijiko cha chai
Samli ya kupikia
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Changanya maziwa ya unga katika maji kikombe kimoja. Tia yai changanya vizuri.
- Katika bakuli, weka unga, chumvi. Kisha changanya na maji upige kwa mchapo wa mkono. Ongezea mchanganyiko wa maziwa na yai uendelee kuchanganya.
- Tazama uzito wa unga, ukipenda mikate mepesi ongeza maji kidogo tu kama robo kikombe uchanganye.
- Katakata vitunguu slaisi kisha vichambue.
- Katakata kotimiri kisha changanya vyote katika unga ukoroge vizuri.
- Weka kikaangio kikubwa katika moto, kisha teka mteko kwa upawa wa duara utandaze mkate. Teka tena uweze kupika vijikate viwili vitatu katika kikaangio kimoja. Kikaangio kiwe kisichongandisha (non-stick).
- Acha unga ukauke upande mmoja, na uive ugeuke rangi kisha geuza upande wa pili.
- Acha uive kisha tia samli kijiko kimoja cha kulia ukaange mkate hadi uive na kugeuka rangi ya hudhurungi (golden brown)
- Epua ikiwa tayari.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)
Kidokezo:
Ukipenda pika katika kikaangio cha kutoa mkate mmoja.