Mkate Mtamu Laini Wa Kuoka (Baked)
Mkate Mtamu Laini Wa Kuoka (Baked)
Vipimo
Unga mweupe - 3 Vikombe vikubwa (mugs)
Sukari - 1/3 mug (chini ya nusu mug)
Maji - ¾ mug
Maziwa ya unga - ½ mug
Mafuta - ¼ mug
Mtindi - 1 kijko cha kulia
Hamira (instant) - 2 vijiko vya kulia
Yai - 1
Hiliki - 1 kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Koroga maziwa ya unga katika maji.
- Ikiwa hamira ni ya chengachenga, weka katika kikombe kidogo cha kahawa, tia chembe sukari na maji iuumuke. Ama ikiwa ya instant changanya moja kwa moja katika unga.
- Changanya vitu vyote katika bakuli, ukande vizuri sana mpaka uwe laini. Ukiwa na mashine ya kukandia ndio vizuri zaidi.
- Ukishalainika, funika kwa muda mpaka uumuke kidogo.
- Washa oveni moto mdogo mdogo (kiasi 150 degrees) Unaweza kuchoma katika mkaa pia.
- Pakaza siagi katika treya za kuokea (baking trayers) weka tayari.
- Fanya madonge saizi upendavyo kisha weka madonge kiasi ya kutosheleza treya zako. Huenda ukatumia treya zaidi ya mbili kulingana na ukubwa wa treya na wingi wa madonge.
- Funika treya uumuke tena vizuri.
- Weka katika oveni upike kwa muda robo saa takriban hadi ugeuke rangi ya hudhurungi (golden brown).
- Epua ukishapoa, toa katika treya panga katika sahani ukiwa tayari.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)