Buns Za Jibini Na Shira
Buns Za Jibini Na Shira
Vipimo
Unga wa ngano - 3 ½Vikombe visivyojaa
Maziwa - 1 Kikombe
Maji - 1½ Kikombe
Yai - 1
Sukari - 2 ½Vijiko vya supu
Siagi au mafuta - ½Kikombe
Hamira - 1 Kijiko cha chai
Chumvi - ¼Kijiko cha chai
Jibini ya malai (cream cheese) - Kiasi utakavyotumia kujaza
Shira
Sukari - 2 Vikombe
Maji - 1 ½Vikombe
Zaafarani (iroweke) - ½Kijiko cha chai
Namna ya kutayarisha na kupika
- Roweka hamira kwenye maji ya uvuguvugu (warm).
- Kisha changanyia vipimo vyote isipokuwa jibini ya malai na shira.
- Kanda kidogo tu kulainisha unga uwe mlaini.
- Paka siagi kwenye treya ya kuchomea yenye vishimo vidogo.
- Halafu fanya viduara vidogo na tia ndani yake jibini ya malai (cream cheese) kwa kutumia kijiko cha chai, na uvifunge viduara vizuri na kuvipanga ndani ya ile treya.
- Iwache iimuke (ifure) Kisha ipike kwenye oveni moto wa 350°F kwa muda wa dakika 20 - 25, Kisha washa moto wa juu kidogo tu ili uwive na kugeuka rangi.
- Toa katika oveni na mwagia shira na itakuwa tayari kuliwa.