Mikate Ya Ajemi
Mikate Ya Ajemi
Vipimo
Unga - 3 mugs
Mtindi (yogurt) - 1 mug
Chumvi - 1 kijiko cha chai
Baking Soda - ¼ kijiko cha supu
Hamira - 1 kijiko cha supu
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Changanya pamoja unga, chumvi, hamira, baking soda, mtindi na mafuta. Uchanganye unga na ukande uwe mlaini vizuri.
- Fanya madonge kama 8 kwa hicho kipimo cha unga.
- Sukuma kila donge na upake samli na ukunje kama chapatti.
- Acha mpaka ikisha kuumuka. Sukuma duara isiwe myembamba kama chapatti iwe kidogo nene
- Choma kwenye jiko juu kama chapatti upande mmoja usigeuze. Epua na uutie kwenye oven, uwashe moto wa juu mpaka uwe rangi ya hudhurungi (brown).
- Tayari kuliwa na chai au mchuzi au kitu chochote.