23-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyenyekevu Wake: Akichukuwa Ushauri Kwa Swahaba Zake

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

23-Unyenyekevu Wake: Akichukuwa Ushauri Kwa Swahaba Zake

 

www.alhidaaya.com

 

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Hakujiona kuwa ni mtu bora kuliko Swahaba  juu ya kuwa yeye ni Rasuli wa Allaah, hivyo alikuwa haamui jambo peke yake bila ya kuchukua ushauri kwa Swahaba zake. Ameitikia amri ya Rabb Wake pindi Alipomuamrisha afanye hivyo kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚإِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَوكِّلِينَ ﴿١٥٩﴾

Basi wasamehe na waombee maghfirah na washauri katika mambo. Na unapoazimia basi tawakali kwa Allaah. Hakika Allaah Anapenda wanaotawakali. [Aal-‘Imraan: 159]

 

 

Hivyo alipokea ushauri kadhaa kutoka kwa Swahaba zake kama ifuatavyo:

 

 

  1. Mwanzo kabisa alipopewa Unabiy akatumiwa Wahyi kutoka kwa Allaah (عز وجل) alimtaka ushauri Mama wa Waumini Khadiyjah (رضي الله عنها).

 

  1. Pia alitaka ushauri kwa Abuu Bakr na ‘Umar (رضي الله عنهما) pindi walipopata matekwa ya vita vya Badr.

 

  1. Hubaab bin Mundhir (رضي الله عنه)  pia alimshauri katika vita vya Badr kuhusu kujaza visima vyote isipokuwa kimoja tu.

 

  1. Salmaan Al-Faarisy (رضي الله عنه) alimshauri kuhusu shimo la vita vya Khandaq (au vita vya Ahzaab). 

 

  1. Pia alitaka ushauri katika vita vya Khandaq kuhusu mazao ya Madiynah.

 

  1. Pia alimtaka ushauri Mama wa Waumini Ummu Salamah  (رضي الله عنها)  walipokuwa Hudaybiyah pindi makafiri wa Quraysh walipowazuia  kuingia Makkah. Ummu Salamah (رضي الله عنها)   Akamshauri Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) wajivue Ihraam; wakachinja na wakanyoa nywele zao.

 

  1. Na alitaka ushauri kwa Swahaba zake mara kadhaa nyenginezo na alikuwa mwenyewe akiwaomba wamshauri kama ilivyothibiti katika Hadiyth:

 

عَنِ الْمِسْوَرِ بْنِ مَخْرَمَةَ، وَمَرْوَانَ بْنِ الْحَكَمِ، يَزِيدُ أَحَدُهُمَا عَلَى صَاحِبِهِ قَالاَ خَرَجَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم عَامَ الْحُدَيْبِيَةِ فِي بِضْعَ عَشْرَةَ مِائَةً مِنْ أَصْحَابِهِ، فَلَمَّا أَتَى ذَا الْحُلَيْفَةِ قَلَّدَ الْهَدْىَ، وَأَشْعَرَهُ، وَأَحْرَمَ مِنْهَا بِعُمْرَةٍ، وَبَعَثَ عَيْنًا لَهُ مِنْ خُزَاعَةَ، وَسَارَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم حَتَّى كَانَ بِغَدِيرِ الأَشْطَاطِ، أَتَاهُ عَيْنُهُ قَالَ إِنَّ قُرَيْشًا جَمَعُوا لَكَ جُمُوعًا، وَقَدْ جَمَعُوا لَكَ الأَحَابِيشَ، وَهُمْ مُقَاتِلُوكَ وَصَادُّوكَ عَنِ الْبَيْتِ وَمَانِعُوكَ‏.‏ فَقَالَ ‏"‏ أَشِيرُوا أَيُّهَا النَّاسُ عَلَىَّ، أَتَرَوْنَ أَنْ أَمِيلَ إِلَى عِيَالِهِمْ وَذَرَارِيِّ هَؤُلاَءِ الَّذِينَ يُرِيدُونَ أَنْ يَصُدُّونَا عَنِ الْبَيْتِ، فَإِنْ يَأْتُونَا كَانَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ قَدْ قَطَعَ عَيْنًا مِنَ الْمُشْرِكِينَ، وَإِلاَّ تَرَكْنَاهُمْ مَحْرُوبِينَ ‏"‏‏.‏ قَالَ أَبُو بَكْرٍ يَا رَسُولَ اللَّهِ، خَرَجْتَ عَامِدًا لِهَذَا الْبَيْتِ، لاَ تُرِيدُ قَتْلَ أَحَدٍ وَلاَ حَرْبَ أَحَدٍ، فَتَوَجَّهْ لَهُ، فَمَنْ صَدَّنَا عَنْهُ قَاتَلْنَاهُ‏.‏ قَالَ ‏"‏ امْضُوا عَلَى اسْمِ اللَّهِ ‏"‏‏.‏

 

Al-Miswaar bin Makhramah na Marwaan bin Hakam (رضي الله عنهما) Wamesema, (mmoja wao kasema zaidi kulikoni swahibu yake) Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka mwaka wa Al-Hudaybiyah pamoja na Swahaba wapatao elfu moja. Walipofika Dhul-Hulayfah akamtia kigwe[1] Hady wake (mnyama wa kuchinja kwa ajili ya Hajj), akaingia hapo Ihraam kwa ajili ya ‘Umrah  kisha akamtuma mpelelezi kutoka kabila la Khuzaa’ah. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaendelea mpaka akafika (kijiji cha) Ghaadiyr Al-Ashtwaatw. Akamjia mpelelezi wake akasema: “Hakika Maquraysh wamejumuika mjumuiko mkubwa dhidi yako na wamekusanya Wahabashia wawe dhidi yako na watapigana nawe na watakuzuia kuingia Al-Ka’bah.”  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم) Akasema:   “Nishaurini enyi watu! Je, mnanishauri niangamize ahli zao na vizazi vyao hao watu wanaotaka kutuzia kuingia Al-Ka’bah?  Kwani wakitujia kwa (amani) basi Allaah (عزّ وجلّ)  Ataangamiza jasusi wa makafiri, laa sivyo tutawaacha katika hali mbaya wakiwa  wamesulibiwa.”  Abuu Bakr akasema?  “Ee Rasuli wa Allaah, umetoka ukiwa na niyyah ya kuzuru Nyumba (Ka’bah) na hutaki kuua mtu wala kupigana vita na mtu. Basi endelea kuiendea (Ka’bah) na yeyote atakayetuzuia kuingia humo tutapigana nao.”  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  akasema: “Endeleeni kwa Jina la Allaah.”  [Al-Bukhaariy]

 

  1. Pia aliwataka Swahaba wamshauri kuhusu kuvunja Al-Ka’bah na kulijenga upya aliposema kuwaambia Swahaba:

 

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ أَشِيرُوا عَلَىَّ فِي الْكَعْبَةِ أَنْقُضُهَا ثُمَّ أَبْنِي بِنَاءَهَا أَوْ أُصْلِحُ مَا وَهَى مِنْهَا؟ قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ: فَإِنِّي قَدْ فُرِقَ لِي رَأْىٌ فِيهَا أَرَى أَنْ تُصْلِحَ مَا وَهَى مِنْهَا وَتَدَعَ بَيْتًا أَسْلَمَ النَّاسُ عَلَيْهِ وَأَحْجَارًا أَسْلَمَ النَّاسُ عَلَيْهَا وَبُعِثَ عَلَيْهَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم

“Enyi watu! Nishaurini kuhusu Nyumba (Ka’bah). Je, niivunje kisha kuijenga upya kuanzia msingi wake au nitengeneze kilichoharibiwa?” Ibn ‘Abbaas akasema:  “Imenijia rai kwamba nnavyoona sawa, ni utengeneze tu (sehemu) ziloharibika na uiache Nyumba (Ka’bah) katika hali yake ile ile pindi watu walipoingia Uislamu (na uache) mawe (katika hali yake ile ile) pindi watu walipoingia Uislamu na katika hali ile ile ulipotumwa (na Allaah) kuja kama Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).  [Hadiyth ya ‘Atwaa ameirekodi Imaam Muslim]

 

 

[1]  Kama kidani cha chuma kwa ajili ya alama kujulikana kuwa ni mnyama wa Hady yaani kuchinjwa katika Hajj. 

Share