24-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyenyekevu Wake: Akichukia Kusimamiwa
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
24-Unyenyekevu Wake Akichukia Kusimamiwa
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ ، قَالَ لَمْ يَكُنْ شَخْصٌ أَحَبَّ إِلَيْهِمْ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ وَكَانُوا إِذَا رَأَوْهُ لَمْ يَقُومُوا لِمَا يَعْلَمُونَ مِنْ كَرَاهِيَتِهِ لِذَلِكَ . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ غَرِيبٌ مِنْ هَذَا الْوَجْهِ
Kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه) amesema: “Hakuweko mtu aliyekuwa kipenzi zaidi kwao kuliko Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).” Akasema: Lakini hawakuwa wakimsimamia pindi wanapomuona kwa sababu walijua jinsi gani alivyokuwa akichukia hivyo (kusimamiwa). [Adab Al-Mufrad, At-Tirmidhiy, ameisahihisha Al-Albaaniy – Swahiyh At-Tirmidhiy (2754),
Shaykhul-Islaam ibn Taymiyyah (حمه الله) amesema: “Maswahaba (رضي الله عنهم) hawakuwa wakimsimamia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa vile walijua kuchukiwa kwake hivyo, wala hawakuwa wakisimamiana wao kwa wao.” [Mukhtaswar Al-Fataawaa Al-Miswriyyah (2/26-27)]
Imaam Ibn Baaz (حمه الله) amesema: “Maswaahaba walikuwa wanapokutana naye Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) walikuwa wakimwamkia kwa kumpa mikono na hawakuwa wakibusu mkono wake…” [Fataawaa Nuwr Alad-Darb ukanda 488)]