25-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyenyekevu Wake Katika ‘Ibaadah Akivaa Nguo Duni
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
25-Unyenyekevu Wake Katika ‘Ibaadah Akivaa Nguo Duni
حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا وَكِيعٌ، عَنِ الرَّبِيعِ بْنِ صَبِيحٍ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ أَبَانَ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ حَجَّ النَّبِيُّ ـ صلى الله عليه وسلم ـ عَلَى رَحْلٍ رَثٍّ وَقَطِيفَةٍ تُسَاوِي أَرْبَعَةَ دَرَاهِمَ أَوْ لاَ تُسَاوِي ثُمَّ قَالَ " اللَّهُمَّ حِجَّةٌ لاَ رِيَاءَ فِيهَا وَلاَ سُمْعَةَ " .
Anas bin Maalik (رضي الله عنه) amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitekeleza Hajj akiwa katika kipando chake cha mnyama, alivaa joho lilokuwa na thamani ya dhirham nne au chini yake. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ee Allaah, (nakuomba iwe) Hajj isiyokuwa na riyaa-a (kujionyesha) wala umaarufu.” [Ibn Maajah, ameisahihisha Al-Albaaniy: Swahiyh Ibn Maajah (2355), Swahiyh At-Targhiyb (1122)]