26-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyenyekevu Wake: Akitembelea Wagonjwa Hata Wasio Waislamu

 

 

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

26-Unyenyekevu Wake  Akitembelea Wagonjwa Hata Wasio Waislamu

www.alhidaaya.com

 

 

 عَنْ ثَابِتٍ عَنْ أَنَسٍ رَضِي اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: كَانَ غُلَامٌ يَهُودِيٌّ يَخْدُمُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَمَرِضَ، فَأَتَاهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَعُودُهُ فَقَعَدَ عِنْدَ رَأْسِهِ، فَقَالَ لَهُ: أَسْلِمْ فَنَظَرَ إِلَى أَبِيهِ وَهُوَ عِنْدَهُ فَقَالَ لَهُ: أَطِعْ أَبَا الْقَاسِمِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَسْلَمَ فَخَرَجَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ يَقُولُ: الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَنْقَذَهُ مِنَ النَّارِ ((البخاري

Kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas (Radhwiya-Allaahu ‘anhu) amesema:  Alikuweko mtoto wa ki-Yahudi akimhudumia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawa anaumwa. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimtembelea. Akaketi karibu ya kichwa chake na akamtaka asilimu. Yule mtoto akamtazama baba yake ambaye alikuwa ameketi karibu yake. Basi baba huyo akamwambia (mwanawe) amtii Abdul-Qaasim, na mtoto akatii na kusilimu. Kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatoka nje akisema: ((AlhamduliLLaah Ambaye Amemkinga na moto)) [Al-Bukhaariy]

 

Share