Basbusa 1 (Shaam)
Basbusa 1 (Shaam)
Vipimo
Unga wa Semolina - 2 Vikombe
Nazi ya chenga 1 kikombe
Siagi (butter) au samli - 3/4 kikombe
Sukari - 3/4 kikombe
Mtindi (Yoghurt au buttermilk) - 1 1/4 kikombe
Vanila- 1-2 kijiko cha chai
Baking powder - 1 kijiko cha chai
Baking soda- 1 1/2 kijiko cha chai
Lozi zilizomenywa maganda kwa ajili ya kupambia.
Shira
Sukari - 1 kikombe
Maji - 1 kikombe
Ndimu ya maji - 1 kijiko cha chai
Pika shira mapema. Chemsha kwa muda wa dakika 20-25 itakapopoa iwe nzito kidogo sio nyepesi sana.
Namna Ya Kutayarusha Na Kupika
- Washa oveni moto wa 350ºF
- Yayusha siagi au samli na iache ipowe.
- Changanya sukari na mtindi katika bakuli kubwa.
- Changanya semolina, nazi, vanila, baking powder, baking soda katika bakuli jengine.
- Tia mchanganyiko wa semolina katika bakuli lenye mchanganyiko wa sukari na mtindi na changanya vizuri.
- Paka siagi katika sinia ya oveni (baking tray) ya saizi 11" x 7 " au 13" x 9" na tandaza mchanganyiko.
- Weka alama ya kukata vipande vipande vya mraba (square) na katika kila kipande weka lozi moja juu yake kupambia.
- Iache kwa muda wa dakika 15-20 kabla ya kuipika.
- Pika (bake) kwa muda wa dakika 30 au zaidi kidogo hadi iwive na igeuke rangi.
- Epua katika oveni na mwagia shira wakati bado imoto na shira iwe iliyopoa baridi.
Kidokezo:
Ikiwa basbusa ni imoto basi shira iwe baridi, na ikiwa basbusa ni ibaridi basi shira iwe imoto.