Keki Ya Tende Ya Mdalasini
Keki Ya Tende Ya Mdalasini
Vipimo
Unga - 5 ½ vikombe
Tende (toa kokwa na katatkata) - 2 ½ vikombe
Mayai - 10
Siagi - 400 gms
Sukari ilosagwa - 3 vikombe
Baking powder - 3 vijiko vya chai
Bicarbonate soda - 1 kijiko cha chai
Maziwa ya unga - 3 vijiko vya kulia
Mtindi (yoghurt) - 1 kikombe
Mafuta - ¼ kikombe
Vanilla - 1 kijiko cha chai
Mdalasini wa unga - 1 kijiko cha chai
Hiliki - ½ kijiko cha chai
Chumvi - ½ kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Washa oveni mapema kiasi.
- Roweka tende katika kibakuli kwa kutia maji ya moto ya kuchemka kiasi vikombe 2 vya maji. Changanya na bicarbonate soda kuilainisha. Roweka dakika chache.
- Changanya na mtindi, upige vizuri mpaka mchanganyiko uwe nyororo.
- Katika bakuli jengine, changanya siagi, mafuta, sukari pamoja upige kwa mashine au kwa mkono mpaka iwe creamy na nyeupe.
- Tia mayai uliyoyapiga pembeni uchanganye pamoja na vanilla, mdalasini na hiliki.
- Tia mchanganyiko wa tende ukoroge ichaganyike.
- Tia unga kidogokidogo huku ukichaganya na baking powder. Kisha tia maziwa uchaganye.
- Mimina katika treya ya kuokea katika oven (baking trayer) uoke (bake) katika oen kiasi moto wa 360 Degrees kwa muda wa ½ saa takriban. Hakikisha imewiva. Epua ikiwa tayari.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)
Kidokezo: Unaweza kutoa keki mbili kutegemea na saizi ya treya unazotumia.