Keki Ya Walnut (Jozi) Na Mdalasini
Keki Ya Walnut (Jozi) Na Mdalasini
Vipimo:
Unga mweupe - 1 ½ kikombe
Siagi - 10 vijiko vya supu
Sukari ya brown (soft brown sugar)- ½ kikombe
Baking powder - 1 ¾ kijiko cha chai
Mayai - 2
Maziwa - ¼ kikombe
Walnut zilokatwakatwa (chopped) - 1 kikombe
Mdalasini wa unga - 1 kijiko cha chai
Chumvi - ¼ kijiko cha chai
Vanilla- ½ kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Weka siagi nje iwe laini (katika room temperature)
- Washa jiko la oveni kiasi cha 350°
- Weka siagi katika bakuli ipige hadi iwe laini.
- Tia mayai uendelee kupiga
- Tia vitu vikavu vyote .
- Tia maziwa kisha walnuts
- Paka siagi katika treya ya kupikia keki iwe size ya kiasi inchi 8 au 9
- Mimina mchanganyiko wa keki
- Pika kwa muda wa dakika 35-40, iangalie kama imeiva kwa kutia kijiti na kukitoa ikiwa kavu tayari, epua na iache ipoe.