Keki Ya Chokoleti Ilokoza Na Kahawa
Keki Ya Chokoleti Ilokoza Na Kahawa
Vipimo
Unga - 2 vikombe
Sukari - 2 vikombe
Mafuta - ½ kikombe
Mayai - 2
Kaukau (cocoa) - ¾ kikombe
Kahawa ya unga - 2 vijiko vya supu
Baking powder - 1 kijiko cha chai
Baking soda - 2 vijiko vya chai
Maziwa - 1 ¾ kikombe
Chumvi - ½ kijiko cha chai
Namna Kupika:
- Washa jiko la oveni moto wa 350° - 375° F
- Paka mafuta treya ya kupikia keki ya saizi 9” x 13” ikiwa ni yenye shimo la wazi kama ilivyo katika picha. Ikiwa huna treya hiyo, tumia ya kawaida.
- Katika bakuli, tia unga, sukari, kaukau, unga wa kahawa, baking powder, baking soda, chumvi.
- Piga mayai katika kibakuli kidogo kisha changanya katika unga pamoja na mafuta na maziwa.
- Mimina katika treya ya kupikia keki, pika katika oveni kwa muda wa dakika 35 takriban.
- Epua ipoe kisha ikate saizi ya vipande upendavyo.