Keki Ya Nanasi
Keki Ya Nanasi
Vipimo:
Unga - 2 vikombe vya chai
Sukari - 1 ½ kikombe cha chai
Mafuta - 1 ½ kikombe cha chai
Baking powder - 2 vijiko vya chai
Siagi - ¼ kikombe cha chai
Mayai - 6
Sukari ya hudhurungi (brown) - 1 ¾ kikombe cha chai
Manasi ya kopo yaliyokatwa duara - 1 kopo
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Unayeyusha sukari ya hudhurungi pamoja na siagi. Ikishayeyuka vizuri unamimina kwenye sufuria au trei ya kuchomea keki.
- Panga vipande vya nanasi kwenye hiyo sufuria/trei. Weka pembeni. Ukipenda katikati ya duara ndogo ya nanasi weka cheri moja.
- Kwenye bakuli la kuchanganyia keki la mashine, piga mayai, sukari, vanilla mpaka iwe kama malai (crème) na nzito.
- Mimina unga pamoja na baking powder, piga kidogo, mwisho mimina mafuta.
- Mimina huo mchanganyiko kwenye sufuria/trei uliyopanga vipande vya nanasi, tayari kuchoma.
- Weka moto 180 C choma kwa muda wa dakika 30 – 35.
- Ikishaiva, acha ipowe kwa muda wa dakika 7, mimina chini juu kwenya sahani, tayari kwa kuliwa.