Muffins (Vikeki) Vya Ndizi

Muffins (Vikeki) Vya Ndizi

Vipimo

Unga -  2 vikombe vya unga  

Ndizi -  3  

Yai -  1 

Siagi -  ½ kiombe  

Sukari ya brown -  1 kikombe 

Maziwa ya kopo ya chai -  2 vijiko vya supu 

Baking powder -  1 ½ kijiko cha chai 

Baking soda - 1 ½ kijiko cha chai 

Vanila - 1 kijiko cha chai 

Mdalasini  - ½  kijiko cha chai 

Chumvi -  ½ kijiko cha chai                                                  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Washa jiko (oveni) kiasi ya moto wa 350F.
  2. Paka siagi mashimo ya treya utakayochomea vikeki. Nyunyizia unga. 
  3. Katika bakuli, tia unga, baking powder, baking soda, chumvi, mdalasini uchanganye vizuri. 
  4. Katika kibakuli kingine, piga yai, sukari ya brown na siagi. 
  5. Tia ndizi ulizozipondaponda (mashed), tia maziwa na vanilla na uchanganye vizuri.
  6. Changanya pamoja na mchanganyiko wa unga. 
  7. Chota utie katika mashimo ya treya uliyotayarisha kisha pika (bake) katika oven kwa muda wa dakika 20 takriban. 
  8. Epua acha zipoe zikiwa tayari.

 

Share