Keki Ya Karoti
Keki Ya Karoti
Vipimo
Unga - 1 Kikombe cha chai
Baking soda - 1 Kijiko cha chai
Iliki ya unga - ½ Kijiko cha chai
Chumvi - ½ Kijiko cha chai
Mayai - 2
Mafuta - ¼ Kikombe cha chai
Sukari - ½ Kikombe cha chai
Sukari ya hudhurungi (brown sugar) - ⅓Kikombe cha chai
Mtindi (yogurt) - ⅓ Kikombe cha chai
Karoti iliyokaruzwa - 1 Kikombe cha chai (kama karoti 2)
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Washa oveni moto wa 350°F.
- Paka mafuta chombo utakayopikia keki, kisha nyunyiza unga na gonga iliyozidi.
- Kwenye bakuli la kiasi, changanya pamoja unga, baking soda, iliki, na chumvi weka kando.
- Katika bakuli nyengine, piga mayai, sukari, mtindi, na mafuta mpaka ilainike.
- Polepole changanya mchanganyiko wa mayai kwenye wa unga hadi ilainike; kisha tia karoti.
- Mimina kwenye chombo uliyo tayarisha na uvumbike kwa dakika 40 - 45.
- Kisha iache ipoe kwenye sufuria dakika 15 halafu pindua na iache ipoe kabisa.
- Tengeneza sukari laini (icing sugar) ½ kikombe na vijiko 2 vya maji na unyunyizie juu; na ikisha kauka itakuwa tayari kuliwa.