Kuku Wa Tanduuri
Kuku Wa Tanduuri
VIPIMO
Kuku - 5 pounds (vipande 20 – 25)
Ukwaju - ½ pakti ( kwa kikombe kimoja cha maji)
Kitunguu saumu (thomu/galic) - 1 kijiko kikubwa cha kulia
Tangawizi - 1 kijiko kikubwa cha kulia
Uzile (binzari nyembamba ya unga) - 1 kijiko cha chai
Pilipili manga - 1 kijiko cha chai (unaweza kuongeza ukipenda)
Chumvi - kiasi
Tandoori masala - 1 kikubwa cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA .
- Watoe ngozi na wasafishe vizuri halafu wachuje.
- Loweka ukwaju na maji kiasi cha kikombe kimoja uvuruge mpake upate urojo mzito, uchuje kama tui la nazi kutoa kokwa kisha umimine urojo kwenye kuku.
- Tia vitungu saumu na tangawizi vilivyosagwa changanya vizuri na kuku na urojo wa ukwaju.
- Kisha tia pilipili manga na uzile na chumvi.(chumvi unaweza kuongeza kidogo kwani wakati wa kuchoma kuku watachuja maji hivyo weka ya kutosha).
- Tia tandoori masala changanya
- Changanya vizuri na waache wakolee kama nusu saa(dakika 30 hivi)
NAMNA YA KUWACHOMA.
- Kama una oven ya kawadia basi wapange kuku kwenye nyavu ya juu ya oven na weka treya tupu kwenye nyavu ya pili.
- Kwenye kifungo cha selector, weka grill na kwenye kifungo cha temperature weka grill vile vile na watachomeka kwa moto wa juu.
- Waache wachomeke kama dakika 25 hadi 30 hivi, huku watakuwa wanachuja maji na yatakuwa yanadongoka kwenye treya tupu.
- Wakishakauka na kubadilika rangi vizuri, ondoa treya ya maji yaliyotoka kwenye kuku.
- Kisha badilisha kifungo cha selector weka bake na kwenye kifungo cha temperature weka 350º weka kama dakika 10 hadi 15 watachomeka kwa moto wa chini.
- Kubadilisha vifungo na moto wa kuchomea kunasaidia kuku kuchomeka pande zote mbili bila ya kugeuza geuza.
- Wakishakauka vizuri watoe, panga kwenye sahani na saladi au pilipili ya kusaga, au chatine. Tayari kwa kuliwa.