Shurba Ya Nyama Ya Mbuzi Ya Sosi Ya Nyanya
Shurba Ya Nyama Ya Mbuzi Ya Sosi Ya Nyanya
Vipimo
Nyama ya mbuzi ya mifupa – 1 kilo
Mafuta - 2 vijiko vya supu
Vitunguu maji (vikate vidogo vidogo) - 2
Nyanya (kata ndogo ndogo) - 5
Kitunguu saumu (thomu/garlic) – kijiko cha supu
Tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
Bizari ya pilau ya unga (Jeera) - 1 kijijo cha chai
Gilgilani ya unga (Dania) - ½ kijiko cha chai
Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai
Mdalasini wa unga - ¼ kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Siki ya zabibu - 3 vijiko vya supu
Shayiri* /Hariys - 2 vikombe
* Shayiri ni aina ya ngano (oats) ila ni tofauti kidogo na ngano. Baadhi ya maduka inajulikana kama ni 'hariys'
Kidokezo:
Ikiwa shayiri nzima nzima, basi roweka kwa muda wa masaa na uchemshe mpaka ziive.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Weka nyama katika sufuria, tia chumvi, tangawizi, thomu, bizari kidogo, changanya na uweke motoni kidogo ichanganyike na ikolee viungo.
- Tia maji, chemsha mpaka iwive.
- Katika sufuria nyengine, weka mafuta na kaanga vitunguu kidogo tu vilainike, usiviwache kugeuka rangi.
- Tia nyanya, endelea kukaanga, malizia bizari zote.
- Mimina sosi ya nyanya katika supu.
- Changanya shayiri na maji katika kibakuli, koroga kisha tia katika shurba.
- Iwache ichemke kidogo tu ngano ziwive.
- Tia siki na tayari kuliwa.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)