Uji Wa Kunde
Uji Wa Kunde
Vipimo
Kunde Kavu - 2 Vikombe
Tui - 1 Kikombe
Sukari - 1 Kikombe
Maji - 7 Vikombe
Garam masala - ½ Kijiko cha chai
Hiliki - Kiasi
Karafuu - 3-4 Chembe
Pilipili manga - ½ Kijiko cha chai
Chumvi - Chembe kidogo
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Chemsha kunde kavu bila yakuroweka kwa maji vikombe 4 na sukari kikombe kimoja kwa moto kiasi mpaka ziwive
- Kisha mimina vitu vyote vilivyobakia pamoja na maji vikombe 3 vilivyobaki na acha ichemke taratibu mpaka maji yapunguke uji uwe mzito.
- Epua mimina kwenye bakuli ukiwa tayari